Huu ndio uhuru wa maoni au | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndio uhuru wa maoni au

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 27, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tumekuwa tunalalamika sana kuhusu watangazaji wa baadhi ya vituo vya redio na televisheni kutumia lugha chafu ambazo haziendani na maadili ya utangazaji bila vituo hivi wala tangangazaji hawa na wahariri wao kuchukuliwa hatua zozote zile za kinidhamu na waajiri au vyombo vinavyosimamia taaluma hizi .

  Wiki iliyopita katika kuto cha Clouds mmoja watangazaji maarufu wa kutuo hicho Bwana Gerald Hando aliamua kuendelea kuvunja maadili haya kwa mara nyingi kwa kujiamini na kwa kurudiarudia kauli zake kama vile wanaosikiliza ni wa upande wake peke yake au hata haieleweki alikuwa ujumbe huo anawapelekea wakina nani haswa .

  Kulikuwa na msikilizaji mmoja aliuliza , hivi chuo cha mafisadi kiko wapi ? nataka kusomea na mimi niwe fisadi , jamaa Gerald akaibuka akasema kiko kule ukivuka bahari kama unaenda Zanzibar alimaanisha kigamboni , mwenye kujua kule kule kigamboni kuna chuo gani atakuwa anajua kimeongelewa nini hapo .

  Ajue kwamba radio ile inasikilizwa na watu wengi sana watu wenye umri mbali mbali na vyama mbali mbali vya siasa , kijamii na vya kidogo anavyotoa kauli kama zile ni uchokozi na ukosefu wa nidhamu ya utangazaji na kudhalilisha wanaokimiliki chuo hicho , hata hao wanaotajwa mafisadi hakuna hata mmoja aliyefikishwa mahakamani mpaka sasa hivi kwa tuhuma hizo kwahiyo yeye sio hakimu aanze kuhukumu watu .

  Pili akaja na kituko kingine msikilizaji aliuliza swali kuhusu hadhi ya zanziber kama ni nchi , akasema yeye haitambui Zanzibar hata kidogo yeye anaitambua Tanganyika , na pale alipo yuko Tanganyika sio Tanzania msimamo wake ni huo huo wenzake wakaanza kucheka na kumshangilia kama vile alivyofanya ni sahihi kabisa .

  Baada ya hili kuna kutuo kimoja cha radio kwa jina la radio kheri nacho kimekuwa kikiruhusu wachambuzi wa dini na wanazuoni wake kutumia lugha chafu na uchochezi dhidi ya dini nyingine bila hatua zozote zile kuchukuliwa na wasimamizi wa vituo hivi au taasisi ya mawasiliano .

  Kama uhuru wenyewe wa habari ndio huu basi , njia tunayoelekea sio hii hata kidogo , tunataka kujenga jamii zinazoheshimika na kuheshimu jamii za wenzao na kuvumiliana tunataka kuona watangazaji wasiokuwa na upande wowote wa chama au dini wakati wa kuwasilisha mada na makala zao zingine kama wao ni wanachama wa chama Fulani au dini Fulani basi waweke wazi tujue misimamo yao ndio hiyo na hiyo ni misimamo vya vituo vyao na wahariri wa vyombo hivyo wamekubali hivyo
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sina shaka unaelewa fika kwamba ufisadi umekuwa sehemu ya maisha yetu,na hata serikali yenyewe inaelewa na kukiri kwamba mafisadi wapo.Wanaolea ufisadi huo ni viongozi wetu,na kwa kupitia kwenye ufisadi huo,watanzania wanadhalilika na kufedheheka vibaya.Si tetei kwamba alichofanya mtangazaji yule ni halali la hasha.Ninalosema hata hivyo ni kwamba,kwa kufumbia macho ufisadi au kushiriki kwenye ufisadi,viongozi wetu ndio walioanza kutudhalilisha.Inawezekana mtangazaji anayetajwa kafikia hatua hiyo baada ya kukata tamaa na kukasirishwa mno na tabia za mafisadi.La msingi hata hivyo ni kwamba,tutoe kwanza vibanzi machoni mwetu ndio tuweze kutoa vibanzi vilivyoko kwenye macho ya wenzetu.

  Kwa lile la kituo cha radio cha dini kutumia lugha za uchochezi, hata mimi si liungi mkono na lina stahili kukemewa kwa nguvu zote.

   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mimi binafasi nawapongeza sana kwa kujiamini kwao na uchapaji kazi wao kwa uwazi tena bila kuficha kitu.

  wewe ulitaka afiche??afiche nini?awefiche mafisadi?awaoneee huruma wao ni akina nani?
  Niku waumbua tu mpaka watakapo acha tabia hii mbaya ya ubinafsi nakujiona wao ndo wao.
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  SHY Hata mahakamani huwezi mshida huyu Gerad yeye kasema ukivuka bahari kuelekea zanzibar wewe ulifikiri ni kipi?Kauli yake haimfungi hata kwa mlenda.

  Mawazo yako na maoni ndio yanaweza kukufunga...kwanini wewe ndio umesema hayp yeye wala hajataja chuo chochote....kumbuka wakati wa fina na masoud nao walikuwa wajasiri kweli...sio kwamba walikuwa hawajui wanachofanya...ni watu wenye akili timamu.

  I am stand to be corrected
   
 5. P

  Paullih Member

  #5
  Sep 29, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Buswelu, you are stand to be corrected... I support you fully ha ha ha
   
 6. E

  E Hazard Senior Member

  #6
  Nov 26, 2014
  Joined: Nov 6, 2014
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Welcome to where we dare to talk openly. I guess so
   
Loading...