Huu ndio uhuni uliotokea Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndio uhuni uliotokea Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Froida, Dec 22, 2010.

 1. F

  Froida JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  a
  [​IMG]


  Samson Mwigamba

  [​IMG]
  KWA ruhusa yenu wasomaji naomba nianze kwa kuwashukuru sana kwa mrejesho mlioufanya juu ya makala yangu ya wiki iliyopita. Ni imani yangu kwamba Waziri Kombani ameisoma ile makala na kama si yeye basi wasaidizi wake wameisoma na watamweleza na kama si wasaidizi wake basi angalau mawaziri wenzake watamwambia na hata kama si mawaziri wenzake na watumishi wenzake serikalini basi makada wenzake wa CCM.
  Ujumbe wenu mfupi wa simu, barua pepe na simu nilizopigiwa, vyote vimeonyesha kwamba lugha yetu kama watanzania sasa ni moja. Tunahitaji katiba mpya na hakuna yeyote atakayezuia hilo. Nawashukuru sana.
  Mniwie radhi kwamba nisingeweza kujibu kila ujumbe mfupi wa simu kwa kuwa zilikuwa ni nyingi mno. Lakini niwahakikishie kwamba nawashukuru sana wote mliowasiliana nami na wale ambao mliosoma lakini kwa sababu moja ama nyingine hamkuweza kuwasiliana nami.
  Leo niruhusuni niongee na wale tunaoweza kuwaita wapenzi wa JK. Nahitaji kuwauliza swali moja lenye maelezo marefu yatakayoambatana na mifano kadhaa. Awali ya yote naomba nitangulie kufafanua kwamba ninaowauliza ni wapenzi wa Rais Kikwete wale waliotamani achaguliwe tena kuwa rais na wale wanaopenda aendelee kuwa rais wa nchi hii.
  Lakini zaidi sana napenda kuwauliza wale ambao hawajali Kikwete kaingiaje madarakani mwaka huu, kwao cha muhimu ni kwa mpendwa wao huyo kuwa rais. Wapenzi ni watu wanaopenda kitu au mtu fulani. Hivyo wapenzi wa JK ni wale wanaompenda Kikwete.
  Na katika hili naomba niwe wazi kabisa kwamba kuna wana CCM wanaompenda Kikwete na wanaofurahia yeye kuwa rais kwa sasa bila kujali aliingiaje madarakani. Vivyo hivyo kuna wana CHADEMA (walio chini ya Mbowe), wana CUF (chini ya Lipumba), wana TLP (chini ya Mrema), wana NCCR (chini ya Mbatia) na wengine kutoka kwenye vyama vya akina Dovutwa na wenzake na hata wasio na vyama ambao wako kwenye kundi la wapenzi wa Kikwete.
  Swali lenyewe linasema, Ni nini tofauti kati ya Tanzania na Ivory Coast?
  Ndugu zangu ufafanuzi wa swali unafuata. Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo alishindana na mshindani wake mkuu kwenye uchaguzi wa rais na mpinzani wake Allasane Ouatara akashinda. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, matokeo ya urais hutangazwa na Tume ya Uchaguzi na huthibitishwa na mahakama ya katiba, mahakama ambayo mkuu wake ni swahiba mkubwa wa Gbagbo na kimsingi kateuliwa na Gbagbo kushika wadhifa huo.
  Katika hali ambayo haikutarajiwa, mahakama hiyo badala ya kuthibitisha ushindi wa Ouatara ikapindua matokeo na kumtangaza Gbagbo kama rais halali. Leo kuna marais wawili Ivory Coast, mmoja anafanya kazi zake akiwa Ikulu mwingine akiwa hotelini.
  Tanzania nayo ilifanya uchaguzi Oktoba mwaka huu. Kilichotokea hapa tunaweza kwa lugha nyepesi kabisa kukielezea kama ifuatavyo. Kwamba kwa mujibu wa katiba na sheria ya uchaguzi katika nchi hii, matokeo ya urais hujumlishwa na wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo na hutangazwa rasmi na Mwenyekiti Taifa wa Tume ya Uchaguzi, mwenyekiti ambaye kimsingi kateuliwa na rais wa nchi kushika wadhifa huo.
  Lakini katika hali ambayo haikutarajiwa, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi badala ya kutangaza matokeo yaliyoletwa kwake na wasimamizi wa majimbo kwamba Dk. Willibrod Peter Slaa ameshinda urais yeye akapindua matokeo na kumtangaza Kikwete.
  Naweza kusema kama alivyopata kusema Mzee wangu Ndimara Tegambwage kwamba leo kuna marais wawili Tanzania, mmoja (Kikwete) anafanya kazi zake akiwa Ikulu mwingine (Slaa) akiwa mioyoni mwa Watanzania.
  Gazeti hili wiki iliyopita tu limeandika habari ambayo hadi leo haijakanushwa na Ikulu wala usalama wa taifa wala CCM kwamba siri imevuja kwamba Slaa alishinda.
  Tanzania ilifahamika vema kwenye medani ya kimataifa enzi za mwalimu Nyerere. Ilikuwa mstari wa mbele na kutoa misimamo ya wazi ya kukemea vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora. Lakini leo wakati Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na serikali za nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika zimetoa matamko ya wazi ya kutomtambua Rais Gbagbo, serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya diplomasia ya kimya.
  Rais Jakaya Kikwete hajatamka hadharani kumtambua Alassane Ouattara kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Ivory Coast na kulaani vitendo vinavyofanywa na Gbagbo na wafuasi wake. Rais Kikwete amezungumzia kidogo sana matatizo ya Ivory Coast wakati akihutubia Mkutano wa Kimataifa wa Amani katika eneo la Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika hivi karibuni nchini Zambia.
  Katika mkutano huo Rais Kikwete alieleza kwamba suala la Ivory Coast linashughulikiwa na mikono salama na akaonyesha matumaini yake kwamba pande mbili zenye mgogoro zitafikia makubaliano. Mwisho wa kauli ya mkuu wa nchi hii.
  Natoa mfano mwingine, angalieni wabunge waliotangazwa majimboni kuwa wabunge kupitia vyama vya upinzani hasa Tanzania bara. Arusha mjini, Mwanza mjini, Musoma, Dar es salaam, Lindi mjini, Kigoma na kwingineko.
  Hakuna mahali ambapo nguvu ya umma haikutumika kushinikiza matokeo hayo. Mwanza umma ulilazimika kuvunja mageti ya halmashauri kwenda kushinikiza akina Wenje na Hainess kutangazwa kama washindi.
  Kuna rafiki yangu aliwahi kunipigia simu akanieleza kwamba watu waliokuwa wakisubiria matokeo ya ubunge kwenye chumba cha kujumlishia matokeo jimbo la Segerea walimsikia msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo akiongea kwenye simu ya mkononi akisema, “Ndiyo mheshimiwa, natangaza”.
  Ikiashiria kwamba wasimamizi hao ambao ni watumishi wa serikali na kisheria huteuliwa na rais, walikuwa wakitangaza matokeo kwa maelekezo. Nikiwa sina uhakika kama kweli kauli hiyo ilisikika nauliza kama hadi leo rais anapozungumza anakemea udini (ambao wengine hatuuoni) na kudai kuponya makovu ya uchaguzi bila kutoa kauli kali kwa wasimamizi wa uchaguzi waliojaribu na waliofanikiwa kuchakachua matokeo utazuiaje watu kuwa na hisia kama hizo?
  Kama hiyo haijatosha, sikiliza hii kali ya mwaka. Katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, katika jimbo la Arusha mjini CHADEMA ilipata mbunge wa kuchaguliwa na madiwani wa kuchaguliwa wanane. Aidha tume ya taifa ya uchaguzi iliwapa madiwani watatu wa viti maalum na wabunge wa viti maalum wawili waliotokea Arusha.
  Jumla ya wabunge na madiwani wa chama hicho kwenye halmashauri hiyo wakawa 14. Kwa upande wao CCM walipata madiwani 10 wa kuchaguliwa, watatu wa viti maalum, mbunge mmoja wa viti maalum aliyetokea Arusha mjini na wakamwongeza mbunge mmoja wa viti maalum kutoka Monduli na kufikisha jumla wa wabunge na madiwani 15. TLP walipata diwani mmoja wa kuchaguliwa.
  Tarehe 17 mwezi huu ukaitishwa uchaguzi wa Meya na Naibu wake kwenye ukumbi wa halmashauri saa 4 asubuhi. Magari ya halmashauri yalikuwa yametutangazia wananchi wa kawaida tujumuike pale halmashauri kusikiliza mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani. Lakini tulipofika hapakuwa na vipaza sauti nje ya ukumbi na wachache tulifanikiwa kupenya na kuketi ndani ya ukumbi. Lakini walipoanza tu mkurugenzi wa halmashauri alitutimua kwa maelezo kwamba wanabaki wabunge, madiwani na maofisa wa halmashauri pekee ili waweke utaratibu wa vikao vyao.
  Matokeo utaratibu haukuwekwa na badala yake madiwani wakaapishwa na hatimaye kuingia kwenye uchaguzi. Lakini madiwani wa CHADEMA wakagomea kitendo cha Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, kuingizwa kwenye orodha ya wabunge wa viti maalum wa CCM katika halmashauri ya Jiji la Arusha ilhali yeye kapata ubunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Tanga.
  Hilo likaleta zogo mpaka kikao kikafungwa jioni bila muafaka. Kesho yake ilikuwa ni Jumamosi na madiwani wote wa CCM na yule wa TLP walipewa barua za mwaliko wa kikao kingine cha uchaguzi wa Meya kwenye ukumbi wa halmashauri saa 4 asubuhi ya Jumamosi, isipokuwa wa CHADEMA tu ndio hawakupewa barua.
  Siku hiyo ya Jumamosi wakiwa peke yao ndani ya ukumbi pamoja na yule wa TLP (jumla 16) bila madiwani 14 wa CHADEMA, wakapiga kura na kumchagua Gaudence Lyimo wa CCM kuwa Meya na Kivuyo wa TLP kuwa Naibu Meya.
  Madiwani wa CHADEMA walishtuliwa na diwani mmoja wa CCM ndipo wakaelekea ukumbini ambako walikuta uchaguzi umekwishafanyika kinyume na sheria na kanuni ambazo zinataka akidi ya madiwani watakaochagua meya iwe theluthi mbili. Wao walikuwa kama nusu tu ya madiwani wote.
  Katika mazingira hayo, CHADEMA nao wakataka kufanya uchaguzi wao wa meya ndani ya ukumbi ule ule. Na wakamwomba mgombea wao wa umeya apite mbele na kuomba kura. Hapo ndipo Lyimo (meya feki) alipokimbilia kwenye kiti cha umeya na kuvaa joho na kuamuru polisi kumtoa nje mgombea umeya wa CHADEMA.
  Ikumbukwe kwamba tangu uchaguzi feki wa madiwani wa CCM unafanyika, askari polisi wenye silaha walikuwa ndani ya ukumbi wa halmashauri kinyume na sheria. Kwa maneno mengine, CCM waliamua kuchagua meya kinyume cha kanuni chini ya ulinzi wa polisi wakiongozwa na OCD.
  Mbunge wa Arusha mjini alipojaribu kupinga kwamba diwani wake hawezi kutolewa ndani ya ukumbi kwa sababu hana kosa lolote na sheria inamlinda kutokamatwa na polisi ndani ya ukumbi, ikatolewa tena amri nyingine na meya yule yule asiyetambuliwa na sheria kwamba “kamata na mbunge toa nje”.
  Hapo ndipo sakata lilipozidi baada ya kuanza kwa mapambano kati ya madiwani wa CHADEMA na polisi ambapo madiwani walikuwa wakizuia mbunge wao asikamatwe kinyume cha sheria huku polisi waking’ang’ania kumkamata.
  Sakata hilo lilikwenda hadi nje ya ukumbi baada polisi kuwazidi nguvu madiwani ndani ya ukumbi na kuwatoa nje. Kule nje mbunge alitupiwa ndani ya gari la polisi na kupelekwa kituoni ambapo aliachiwa baadaye na ndipo alipoishiwa nguvu na kuanguka chini na kuzimia na viongozi wa chama wakampeleka hospitali ya mkoa Mount Meru . Hivi sasa anaendelea vizuri kiafya.
  Huu ni uhuni uliopitiliza na ikumbukwe kwamba uhuni huu umekwamisha upatikanaji wa mameya na wenyeviti halali kila halmashauri ambako CCM ina hali mbaya ikiwa imezidiwa idadi kidogo tu. Arusha, Mwanza, Hai, Kigoma, kwa kutaja maeneo machache. Msomaji waweza kusema ninatumia lugha kali sana.
  Lakini fikiria hivi. Mjini Arusha CHADEMA walikubali mbunge wa viti maalum kutoka Monduli aingie kwenye orodha ya madiwani wa CCM kwa sababu yuko ndani ya mkoa huo huo, lakini wakapinga kitendo cha kuchukua mbunge kutoka Tanga ili mradi tu kuipa CCM ushindi.
  CCM wanadai ni haki yao kutoa mbunge wa viti maalum kutoka sehemu yoyote ya Tanzania ili aje kufanya kazi halmashauri ya Arusha na hivyo kupiga kura ya umeya.
  Lakini CCM hiyo hiyo, hadi leo imekataa kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai kwa maelezo kwamba CHADEMA imewahamisha Lucy Owenya kutoka Moshi mjini na Grace Kiwelu kutoka Moshi vijijini na kuwahamishia wilaya ya Hai.
  Kwa maelezo ya CCM Hai, ni kinyume cha sheria. Kwa hiyo CCM inasema Arusha mjini kwa kuwa wao wana madiwani wachache ni ruksa kisheria kuhamisha mbunge wa viti maalum kutoka Tanga kuja Arusha ili awapigie kura. Lakini CCM hiyo hiyo inasema kwa kuwa Hai wao wana madiwani wengi ni kinyume cha sheria kwa CHADEMA kuhamisha wabunge wake wa viti maalum kutoka halmashauri nyingine ndani ya mkoa huo huo na kuwapeleka Hai.
  Halafu vitendo hivi vinaungwa mkono kwa wazi kabisa na mawaziri wa Kikwete na yeye mwenyewe wala waziri mkuu wake wala makamu wake hawazungumzi chochote. Nani atatuzuia kuamini kwamba viongozi wa CCM wa mikoa na wilaya wanaelewa fika kwamba ushindi wao wote kuanzia taifa hadi kwenye vitongoji hupatikana kwa kuchakachua? Na kwamba wanafanya uhuni unaoendelea kwenye halmashauri mbalimbali wakijua watalindwa na viongozi wote wa serikali na vyombo vya dola? Hivi kama unajua baba yako mzazi ama mlezi ni jambazi na kwamba nyumbani kwenu kila kitu mnachotumia kuanzia furniture hadi chakula kimepatikana kwa ujambazi, utakuwa na wasiwasi kuiba hela ya mfukoni? Unaweza kweli kuogopa kwamba utagombezwa na baba kwa kuiba? Huna wasiwasi, maana unajua kauli ya ukali kabisa ambayo baba yako anaweza kukukanya nayo ni: “mwanangu, unapoiba uwe makini usionekane”. Ndivyo ilivyo kwa vigogo wetu wa CCM na wadogo zao wa mikoani na wilayani
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mwigamba is a very smart guy.
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  I salute you Mwigamba!!!!
   
 4. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Naipenda hii
  Kinachoumiza ni kwamba ujumbe huu unatufikia wachache
  Inatakiwa tuamshe hamasa kwa wengine pia hata kama tutaweza andamana poa lakini kilichoandikwa ni maudhi ngoja nitafute ndovu niikumbuke Tanzania vizuri
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nimekuelewa. CCM ni wezi na siku zote ni wezi na hawajawahi kutokuwa wezi.
   
 6. semango

  semango JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  daah!asante sana mkuu, umetupa picha kamili ya matukio yalivyokua.ngoja nikapige zangu ulabu tu maana moyo wote umekufa ganzi.nchi yenyewe kumbe imefikia hivyo!!no wonder watu wanaamua kuvamia mapenzi tu maana wanaona siasa inaweza kuwaua kwa mawazo.
   
 7. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nakupa :A S thumbs_up: "Kweli itafika wakati watanzania watasema BASI INATOSHA!
   
 8. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duuh inasikitisha, inaudhi, inakasirisha sana.
   
 9. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  kaka andika makala hii kwenye magazeti ya TZ, itasaidia kuamsha wananchi juu ya uhuni unaofanywa na CCM
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280

  Kama hizo nilizozihighlight ni sahihi basi CCM walipigwa mueleka wa nguvu, huku Bara na kule Zanzibar. Lakini wakasimamia kwa nguvu ya dola kauli yao, « Ushindi ni lazima,mapinduzi daima ».

  Tanzania itakuwa ni zaidi ya Ivory coast, CCM Itakuwa imejitwalia ushindi kiharamia katika chaguzi kuu mbili.
  Halafu wanawaita wenzao wapenda madaraka ! Nyani haoni.................... !

  Ving'ang'anizi bwana!!??

  Dr, Slaa nakuona upo online,hebu tuthibitishie hilo katika Red, jee ni kweli kutokana na taarifa zenu kuwa Ulishinda? au Kikwete alishinda lakini kiwango cha ushindi kikaongezwa? nimeona taarifa nyingi zinazokinzana sijui niamini ipi!
   
 11. o

  olng'ojine Senior Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata hatuna voingozi waadilifu..ni genge la majambazi tuu.
   
 12. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu.
   
 13. p

  paul p raia Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hili la Arusha ngoja tuone mwisho wake maana watu wa Arusha hawapendi kuburuzwa.
   
 14. S

  Subira Senior Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tafadhali nisaidie sheria inasemaje maana huyumary chatanda ni mkazi wa arusha na nikatibu waccm wa mkoa, kisha ni mbunge wavitimaalum je anatakiwa akapigie kura wapi?
   
 15. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Hivi mantiki ya kukiita cha cha siasa ati ni "Chama Cha Mapinduzi" ilikuwa ni nini? Walimpindua nani 1977?
   
 16. I

  ISIMAN Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  stay blessed what u said is true
   
 17. I

  ISIMAN Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yanafanywa mambo ya kijinga sana
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwanza tuliangalie hili suala la Mbunge wa Viti maalum Mh Chatanda

  Pili, bado naona hii vita ni rahisi sana kwa Chadema kushinda...........kama watu waliitisha mkutano bila wao kushirikishwa......mbona Majambazi CCM wanajiaibisha tu.................kwanini CDM mnakuwa na wasiwasi?
   
 19. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Watu hawa hawana amani na uongozi wao. Guilty conscious inawatafuna. The only consolation waliyo nayo ni ubabe na virungu. Mioyo yao inawashtaki.
   
 20. A

  Adoniki Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm ni waasi wakubwa sana ona walichofanya karagwe watu wamewtia umaskni kwa sababu ya upumbavu wao wasubiri 2015 cha moto watakiona
   
Loading...