Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 572
- 356
Wakati huu ambao Mheshimiwa rais ana fanya kazi ya kutumbua majipu, ni wajibu wetu raia kumsaidia kumuonesha majipu mengine ambayo hayaonekani kwa urahisi. Wizara ya elimu na labda wizara nyingine kuna majipu ambayo yamejificha hayaonekani kutokana na walimu kuwa na malalamiko mengi ya mishahara duni, kucheleweshewa mishara, malimbikizo, mazingira duni ya kazi nk. Pamoja na matatizo yote hayo walimu wengi wanafanya kazi yao kwa bidii na kwa moyo wa hali ya juu kuelimisha taifa hili. Hata hivyo wapo walimu wachache wanaowaachia wenzao mizigo huku wao wakilipwa bila kufanya kazi serikalini. Ufisadi wanaoufanya baadhi ya walimu hao ni huu.
Kuna baaadhi ya walimu ambao wanaomba ruhusa ya kwenda kusoma wakisingizia wamepata vyuo. Wakipewa ruhusa wanakwenda kufanya kazi katika shule za binafsi huku wakipokea mishahara miwili yaani ule wa serikali na ule wa shule binafsi anakofanya kazi huko kwa mwajiri wake akidhaniwa yuko chuoni. Walimu wa aina hii wamezagaa sana mijini hasa Dsm ambako kutokana na umbali kutoka mikoani walikotoka huwa hawagunduliki kiurahasi. Muda wa kozi aliyoomba ukiisha anarudi kituoni na kuongeza miaka mingine akidai anachukua post graduate au masters. Haya yanafanyika sana na ukiwauliza wanakwambia akirudi kazini haulizwi vyeti na asipopeleka hawana shida kwani labda uwe na kimbele mbele cha kupandishwa madaraja au cheo. Sasa kwakuwa wanajua ulikuwa ni uongo wana minya na kutafuta mwanya mwingine wa kutoka.
Haya yote yanatokea kwakuwa hakuna ufuatiliaji wa karibu kujua mwalimu kasajiliwa chuo gani na namba yake ya usajili ili kuona kama kweli anasoma huko aliko. Wakati mwingine haya hufanyika kwa kula njama na wakuu wa shule ambao humegewa kidogo kutoka katika mshahara wa mwl fisadi kila mwezi hivyo kumfichia siri. Nashauri serikali ifanye uchunguzi wa walimu wote walioomba ruhusa ya kwenda kusoma kama kweli wanasoma na ni vyuo gani na kupata uhakika kutoka vyuoni. Wale wote ambao wamerudi waamriwe kuwasilisha vyeti vyao vya kuhitimu ili kujiridhisha kuwa kweli walikuwa vyuoni vinginevyo warudishe mishahara yote waliyolipwa kwa kisingizio cha kuwa vyuoni na kisha kufukuzwa kazi na kushitakiwa kwa udanganyifu. Hili linafanyika sana upande wa sekondari.
Ujanja mwingie wanaotumia walimu ni kuondoka vituoni wakidai wanauguliwa na wazazi wao mbali hivyo huongea na mkuu wa shule ili awekwe dei waka ambaye atakuwa analipwa na mwalimu aliyepo "kuuguza" wakati si kweli wanakuwa wapo shule nyingine wakipiga mzigo. Utashangaa mwalimu anakuwa kuuguza kwa miaka miwli. kwakuwa huku nyuma kaweka dei waka kwa mapatano na mkuu wa shule akilimlipa laki moja kutoka katika mshahara wake wa labda laki 400,000 anabaki na 300,000 akijumlisha labda na ule anaolipwa private wa labda 500,000 anajikuta ana laki 800,000 na zaidi. Haya yanafanyika sana na kuwaathiri watoto wetu mashuleni kwani baadhi ya madei waka huwa hawana uwezo kwa kuwa huwa sio walimu na ni chipu leba.
Kwakuwa serikali sasa ina maafisa elimu sekondari kila wilaya ni vema ikafanya uchunguzi wa walimu wote waliowahi kuomba ruhusa za kwenda kusoma kama kweli walikwenda kwa kuthibisha vyuo walivyokwenda na namba zao za usajili huko na wa wasilishe vyeti vya kuhitimu. Kisha wathibitishe kupitia vyuo hivyo kama ni kweli waliwasajili na kusoma na kisha kuhitimu katika vyuo hivyo. Waliopo vyuoni nao wafuatiliwe kama wako huko kweli vinginevyo watimuliwe ili washitakiwe, warudishe mishahara yote waliyolipwa wakijidai wako vyuoni na kisha wabaki huko private na badala yake serikali iajiri walimu ambao watawajibika ambao wamejaa mitaani.
Jamani dawa ya majipu ni kuyatumbua na siyo kuyakuna. Watu wafanye kazi sio kulipwa wakati hawafanyi kazi.