Huu ndio mwisho wa Jonas Malhero Savimbi maarufu kama "Savimbi a' fantoche".

DEMBA

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,176
2,000
HUU NDIO MWISHO WA JONAS MALHERO SAVIMBI MAARUFU KAMA "SAVIMBI a' FANTOCHE".

Copyright reserved C&P
NA Comred Mbwana Allyamtu

Jonas Malheiro Savimbi, Moja ya Vibaraka wa karne hapa Afrika,.Wakati ule Augustino Neto na MPLA wakiwa wamefanikiwa kuikomboa Angola kutoka kwenye Ukoloni wa Wareno ndipo akaibuka Savimbi akipambana na Nchi yake Mwenyewe kutokea Msituni kwa miaka 26 akisaidia Makaburu kupora dhahabu.

Inasemekana Savimbi akiwa porini alipata kila kitu, kuanzia Silaha na starehe zote alizozitaka yeye na kikosi chake cha wanamgambo wa chama chake maarufu kama UNITA,...aliletewa Silaha za kisasa kutoka Ulaya na hata Fedha akapambana mwanzo mwisho dhidi ya Taifa lake Mwenyewe akijiita Kamanda Jenerali.

Mwisho wa Ubaya aibu, umdhaniaye siye kumbe ndiye, Savimbi aliuawa Kinyama 22 feb 2002 akiwa na miaka 67, aliuawa huku akilindwa na walinzi wake 21 (body guards) huko porini jirani na Mto Luvuei ktk Jimbo la Moxico.

Kwa Miaka yote ya Utumishi Wa U-Kibaraka haikuwa rahisi kumkamata Savimbi, kwani kabla ya hapo alikuwa ameshakwepa Majaribio 12 ya kumuua, alisharipotiwa amekufa mara 15 lakini anaibuka, ila ajabu ni kwamba siku hii aliyouawa Operation ilikuwa Rahisi sana....kwanza kabisa alidhoofishwa kwa Mawasiliano yake yote kukatwa, redio zikawa kimya,..Kisha akavamiwa na majeshi akiwa amejipumzisha, haya yalikuwa ni mashambulizi ya kushtukiza sana..Savimbi alipigwa Risasi 15...Risasi Moja ya Koromeo.. Mbili za kichwa..na zingine 12 zikatawanywa Miguuni, Mikononi na Kifuani..Akafa na bunduki Mkononi, akazikwa huko huko chini ya Mti.

Kifupi Majeshi ya Angola yalishamshindwa Savimbi, Kufa kwake inasemekana aliuawa na wale wazungu aliowasaidia kupora Dhahabu ya Angola... Walipotosheka wakammaliza.. Vibaraka aina ya Savimbi wamejaa Afrika, Wapo Kila Nchi, Kuwajua hawa ni rahisi tu..Gusa Mambo ya Msingi na hasa hasa Rasilimali.
 
cmases

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
1,611

Bora huko alikuwa mpinzani, hapa kwetu wanaochukua mali zetu na kupeleka nje ni watawala wa nchi yetu walioshika dola.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom