Huu ndio msingi wa haya yatayotokea leo na pia ni msingi wa yatatokea siku zijazo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,998
144,338
Tunaweza kuwa tunaimiza vichwa juu ya haya yanayoendelea na pengine tukawa hazipati majibu na tunashindwa kuwaelewa hawa watu tuliowapa dhamana kwanini wanafanya au kutenda haya.

Naomba niwaambie sababu kubwa ni hii:

"Chama cha siasa au Mtawala ambae yuko madarakani kwa muda mrefu au mfupi, lakini teyari ametenda dhambi au maovu mengi, dhambi na maovu hayo ndio huongoza nchi na si tena busara,maarifa wala hekima ya kiongozi au chama chake"..
 
"Chama cha siasa au Mtawala ambae yuko madarakani lakini teyari ametenda dhambi au maovu mengi, dhambi na maovu hayo ndio huongoza nchi na si tena busara,maarifa wala hekima ya kiongozi au chama chake"..
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , kwanza asante kwa uzi huu, pili naheshimu mawazo yako, mwisho naomba kutofautiana na wewe, hoja yako hii sio kweli !.
  1. Mungu huweka tawala zote za mataifa na tawala hizo zinaongozwa na watu.
  2. Dhambi au maovu yoyote hayajitendi yenyewe, yanatendwa na watu, hivyo sii kweli kuwa uovu au dhambi ndio unaongoza nchi na sio kiongozi.
  3. Kuna baadhi ya dhambi au uovu ambao kwa macho ya kibinaadamu ndio tunaona kama dhambi au ni uovu, kumbe ni mpango wa Mungu mwenyewe ameruhusu dhambi hiyo au uovu huo utendeke ili baadae autumie kudhihirisha ukuu wa Mungu, hivyo mtenda dhambi huyo au mtenda uovu huo ataendelea kubarikiwa kwasababu huo ndio mpango wa Mungu.
  4. Na iwapo dhambi hiyo au uovu huo sio mpango wa Mungu, then ni Mungu mwenyewe ndio hutoa hukumu kwa kila mtenda dhambi au mtenda uovu na sio kweli dhambi au uovu ndio huongoza.
  5. Na sasa nimalizie hapa kwa faida ya wengine, nchi yetu hapa ilipo, tunakwenda vizuri, so far so good, kiongozi aliyepo hajatenda dhambi yoyote, au uovu wowote kustahili hukumu yoyote ya Mungu.
Mungu Ibariki Tanzania.

P
 
Hiki chama CCM kimeshapoteza uhalali wa kuiongiza nchi,kilichopo Sasa Ni kufanya Kila aina ya ufisadi na ufuska ili kujihalalishia uongozi.mwaka 2019 kilivuruga uchaguzi,mwaka 2020 kilibaka demokrasia,mwaka 2021 wanazalishwa kina HAMZA ,Hamza Ni matokeo ya utawala uliokosa ridhaa ya wananchi.CCM itazalisha kina Hamza wengi watakao amua kujitafutia haki yao mkononi.Haiwezekani miaka 60 ya uhuru taifa bado linasumbuka na shida zisizo na kichwa Wala miguu,
Maji hakuna NCHINI.
Shule mbovu
Barabara mbovu
Wizi na utaperi serikalini.
Viongozi wabovu.
Unyang'anyi umeshamiri.
Haki hakuna mahakamani.
Chuki zimetawala.
Ajira za kujuana serikalini.
Hospital dawa hakuna.
Walimu hawatoshi .

Siku tukifanikiwa kuitoa CCM MADARAKANI Kila mtanzani lazima afaidi matunda kamili na ya kweli ya uhuru,keki kubwa ya taifa itawgawanywa kea Kila maskini na mnyonge w taifa Hili.

Neno USIOGOPE kwenye Bible limetajwa Mara 366 hivyo watanzaia tusiogope kuitoa CCM MADARAKANI.
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip , kwanza asante kwa uzi huu, pili naheshimu mawazo yako, mwisho naomba kutofautiana na wewe, hoja yako hii sio kweli !.
  1. Mungu huweka tawala zote za mataifa na tawala hizo zinaongozwa na watu.
  2. Dhambi au maovu yoyote hayajitendi yenyewe, yanatendwa na watu, hivyo sii kweli kuwa uovu au dhambi ndio unaongoza nchi na sio kiongozi.
  3. Kuna baadhi ya dhambi au uovu ambao kwa macho ya kibinaadamu ndio tunaona kama dhambi au ni uovu, kumbe ni mpango wa Mungu mwenyewe ameruhusu dhambi hiyo au uovu huo utendeke ili baadae autumie kudhihirisha ukuu wa Mungu, hivyo mtenda dhambi huyo au mtenda uovu huo ataendelea kubarikiwa kwasababu huo ndio mpango wa Mungu.
  4. Na iwapo dhambi hiyo au uovu huo sio mpango wa Mungu, then ni Mungu mwenyewe ndio hutoa hukumu kwa kila mtenda dhambi au mtenda uovu na sio kweli dhambi au uovu ndio huongoza.
  5. Na sasa nimalizie hapa kwa faida ya wengine, nchi yetu hapa ilipo, tunakwenda vizuri, so far so good, kiongozi aliyepo hajatenda dhambi yoyote, au uovu wowote kustahili hukumu yoyote ya Mungu.
Mungu Ibariki Tanzania.

P
Ni aibu kwa mtu mwenye uelewa kutumia muda wake kutetea uovu na waovu eti ni mapenzi ya mungu!
Kuvuruga Uchaguzi
Kukiuka katiba na sheria
Na mengine mengi yote ni mapenzi ya mungu?

Kama ni hivyo tutabaki masikini na watumwa milele.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom