Huu ndio msimu,tuwapeleke watoto wetu jando,sio kila kitu mpaka kwa Msaada wa watu wa Marekani

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

"Wanyamlusi" wa Kabila la Kigogo wakiwa tayari kwa kuogeshwa baada ya kumaliza siku zao za jando la kimila.



Huko nyumbani kwa sasa ni msimu wa baridi,tena ile baridi kaliiii.Ukitembelea mikoa ya nyanda za juu kusini na kule Kaskazini wa Tanganyika,ni baridi kali isiyo na huruma.

Hata katika mikoa mingine yenye joto la wastani katika vipindi vingine vya mwaka,sasa ni majira ya baridi,baridi ya kushawishi kuoga maji ya moto.

Huu ndio msimu mzuri kuwapeleka watoto na wajukuu jando (Sun'a).Ni msimu mzuri sababu majira ya mwaka yanatoa msaada wa watoto kupona haraka,lakini pia ni msimu mzuri sababu vijana wengi wanakuwa wamefunga shule kutoka muhula wa nusu ya kwanza ya mwaka kwenda nusu ya pili ya mwaka.

Imekuwa ni aibu kwa miaka ya karibuni mpaka kutoa govi kwa watoto tunasubiri msaada wa watu wa Marekani chini ya shirika la USAID.Unasikia kabisa matangazo katika radio na Tv,ukiwa mbele ya watoto na wajukuu kuwa kuna "kampeni" ya kutoa govi kwa msaada wa Watu wa Marekani.

Hivi kweli hata kutoa hiyo ngozi mpaka msaada wa watu wa Marekani?Unakuta Tangazo kubwa barabarani limeandikwa "Ondoa Mkono Sweta,Kwa msaada wa Watu wa Marekani".

Wazazi na walezi,tuwapeleke watoto jando wangali vijana wadogo,ili kuwaepusha na magonjwa na hali ya kutojiamini wakiwa na wenza wao wakati wa ukubwa wao.Mkono sweta huondoa kujiamini na furaha.

Makabila kama Wagogo na Wamasai jambo hili hubeba mila na desturi zao.Ni sehemu ya utamaduni wao na hufanyika katika msimu kama huu.Niliwahi tembelea maeneo ya Dodoma miaka ya 90,nikashuhudia vijana wanaopelekwa jando,wao wakiwaita "Wanyamlusi".

Kwa asili hawa "Wanyamlusi" hupelekwa porini na kukaa huko mpaka wapone.Hupewa fimbo ndogo ngumu,hizi hufahamika kama "sungururu".Kazi yake ni kujipiga sehemu za enka ya mguu pale ambapo "Abdalah kichwa wazi" anasimama.Maana kusimama simama kwa "Abdalah" kunasababisha kidonda kisipone haraka.Ile "Sungururu" hutumika kujipiga sehemu za enka ili kutuliza mzuka wa "Abdalah",na kisha "Abdalah" hulala kwa upole.

Hawa "Wanyamlusi" wakati wa jando hupakwa udongo katika mwili,siku akija ogeshwa(tena anaogeshwa na bibi kizee), ngozi yake inakuwa nyororo sana, kisha anapakwa tilazi(ile siagi ya maziwa ya ng'ombe ambayo haijachemshwa, haijawa samli), hapo anakuwa anang'aa, ngozi laini,ameshapona,anaitwa Mwinzalu.

Hapo anavalishwa kanga au kitenge kipya, na nguo mpya nyingne,anatembea na fimbo yake, hakuna kucheka na mwanamke, anakuwa amenuna, hadi apewe pesa au zawadi nyingne, ndiyo anaongea au kucheka(ni hii ina apply hadi kwa mama na dada zako).

Siku hii huwa ni sherehe kubwa,na hapo kijana huwa tayari hata kurusiwa kuanza kuchunga ng'ombe wakubwa badala ya ndama na mbuzi.

Sasa zama zimebadilika,si lazima kupitia hatua zote hizo za kijadi,bali vijana wanaweza kupelekwa jando kwa njia za "kisasa" na kufikia lengo la kuondokana na mkono sweta.

Ni aibu,hata baada ya miaka 50 ya Uhuru,bado kuna mambo yahusuyo afya,tunasubiri pesa na msaada wa mashirika kama USAID ili tuweze kuyafanikisha.

Unapopita na mgeni wako asiyejua Kiswahili,anasoma bango barabarani limeandikwa "Ondoa Mkono Sweta,Kwa msaada wa Watu wa Marekani",anapoomba tafsiri,inakuwa aibu kuona mpaka kutoa govi(mkono sweta) tunasubiri kodi na msaada wa watu wa marekani kupitia USAID.
 
Nadhani kadiri miaka inavyoenda jamii kubwa inakua na utayari wa kufanyia tohara watoto wa kiume. Nakumbuka miaka ya tisini mwanzoni nikiwa dogo tu nilienda kijijini kwa babu kanda ya ziwa huko, baada ya kuchunga ng'ombe na wenzangu tukapiganisha madume ya ng'ombe then madogo tukaingia kuoga bwawani, wale wenzangu madogo kama sita hivi walikua hawajakata govi wakawa wananishangaa nimekata nikastaajabu wananicheka koz nimekata nami nikashangaa why hawajakata, nikamwambia mdingi ile ishu akanambia huko kijijini kukata sio mila. Serikali ihamasishe tu watu wakate mkono wa sweta.
 
tena uwaambie kabisa wawapeleke jando za kimila...hizo za hospitali zinasababisha mashine zinakuwa na manundu manundu (ujumbe huu umeletwa kwa hisani ya wana beijing)
 
Wiki kesho nitakuwa nyumbani kwa Sherehe za jando ya Vijana wa mwisho kabisa kabla kisu hakijafungwa.

Huko kwetu umasaini, pamoja na kuhitaji sana misaada lakini hatuwezi kuingiliwa mpaka vya ndani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom