Huu Ndio Mpango Wa CCM Kuiba Kura Zanzibar

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Na Mwandishi Wetu
"SERIKALI imara (adilifu), vyombo imara vya habari, taasisi imara za kidola, ni nyenzo muhimu katika kujenga jamii ya haki na inayojali demokrasia," anasema Rais Barrack Hussein Obama wa Marekani.
Obama anaamini taasisi za kidola zinazosaidia kutoa na kutunza haki, zina mchango mkubwa katika kujenga jamii ya kistaarabu kwa maana ya inayofuata misingi ya utawala bora.
Ni kaulimbiu yake kwa mataifa ya Afrika. Ameihimiza nchini Ghana mwishoni mwa wiki alipohutubia bunge, akiwa katika ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu achaguliwe kuongoza taifa tajiri zaidi na lenye nguvu kubwa zaidi za kijeshi duniani.
Tume ya Uchaguzi ni moja ya taasisi zinazolengwa na kiongozi huyu. Uimara wa taasisi hizi una umuhimu mkubwa kwa sababu unachochea ujenzi wa taifa imara na linalojali haki ya kila mtu.
Ya Obama ni falsafa ambayo ingekuwa haitambuliki kwa viongozi wa kisiasa wa Zanzibar, akiwemo Rais Amani Abeid Karume, nisingewalaumu. Ningeielimisha kwao.
Wanaijua falsafa hii. Wapo miongoni mwao wasomi. Wanaisema na kuirudia kila wapatapo nafasi. Wanashuhudiwa wakithubutu kuieleza wanapokutana na maofisa wa kibalozi na wageni wengine.
Kujua kitu na usikitekeleze kwa utashi tu wa kibinafsi ni tatizo. Viongozi wa SMZ wanajua lakini hawajali. Matendo yao kiuongozi, yanawasuta. Wanatenda na kupanga kwa kujua matokeo.
Walipobuni mradi wa kuwapa Wazanzibari kitambulisho cha ukaazi, walijua wanachokitaka. Walijua kitalalamikiwa kuwa si kitu chema. Walijua.
Siyo tu hawakusikiliza, walikitetea kitambulisho hiki kwa nguvu kubwa. Walijua kina maslahi makubwa kwao kuliko kitakavyosaidia kujenga jamii imara inayopenda haki na kujali demokrasia. Ile anayoihimiza Obama.
Kwa viongozi wa Zanzibar, maslahi ni yale yao, si ya nchi na watu wanaowaongoza.
Makala nyingi ziliandikwa kuhusu kitambulisho cha ukaazi kwa Mzanzibari. Binafsi niliandika si moja. Nakumbuka niliandika hata SMZ iliposema kupitia kwa wakala wake, Ali Mwinyikai, mimi si mwandishi.
SMZ ilinifungia kufanya kazi ya uandishi mwaka 2005 kwa sababu sikuwa na kitambulisho kinachotolewa na Idara ya Habari (MAELEZO). Bahati wenye huruma na umma walipiga kelele mpaka ikapiga magoti; kifungo kilidumu kwa siku 11 tu.
Nilisema kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi ni mpango wa hujuma. Kimeletwa ili kuzuia watu kufaidi haki yao ya msingi na kikatiba: kuchagua viongozi watakao.
Ilielezwa kwamba kitambulisho hiki ni ushetani kama ule wa uliokuwepo wakati wa milipuko ya mabomu. Hii niliipa jina la "milipuko ya kishetani" kwa sababu ni kama vile ikilipuliwa na shetani.
Dakika tatu tu baada ya mlipuko walifika wana Usalama wa Taifa na Polisi. Ilikuwa milipuko ambayo mara zote haikufikia ilipolengwa, bali hugusa tu. Haikuwa milipuko ya kweli, mbinu tu ya kupata kushughulikia wapinzani.
Ili kuthibitisha hivo, hadi leo Jeshi la Polisi lililomtuma kachero wake namba moja, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, sasa Kamishna Robert Manumba, halikutoa ripoti baada ya kuichunguza.
Taarifa zinasema walibaini ikitegwa na kulipuliwa na wana usalama wenyewe na mawakala wao wakiwemo wana habari wanaokula nao.
Sasa kitambulisho ambacho kwa mujibu wa sheria ni lazima kwa Mzanzibari, na asipokuwa nacho akishitakiwa ametenda kosa la jinai linalostahili afungwe na kulipa faini, kinatumika vilevile kimipango.
Kimekuwa silaha ya kisiasa. Kilipoanza kutolewa serikali ilihimiza mtu akipate, hawakukipata. Serikali ikajitia hamnazo kusema "hakuna tatizo utaratibu utarahisishwa."
Tume ya Uchaguzi ilikataa kuhusisha kitambulisho hiki na uandikishaji wapiga kura. Ilipata upinzani kwa serikali, lakini ZEC walikamata barabaraba. Serikali ikaachia.
Lakini baada ya kushindikana kukifuta, Chama cha Wananchi (CUF) ilihimiza kila mtu ahakikishe anapata kitambulisho. Watu walikihangaikia kukipata kwa utaratibu wa kawaida uliowekwa.
Walioshindwa kukipata, wakatumia fedha; uchawi wa kizungu. Ni hongo au mlungula. Wengi walikipata. Masheha, viongozi wa ngazi ya chini kabisa kiserikali, walitajirika sana kwa njia hii ya "penye uzia penyeza rupia."
Serikali ikapiga mbizi. Ilipoibuka juu, ikaingiza kipengele kwenye Sheria ya Uchaguzi Na. 11 ya mwaka 1984 kinachoshurutisha kila mwananchi kuwa na kitambulisho ndipo aandikishwe kupiga kura.
Yaleyale waliyosema wachambuzi mwaka 2005 serikali ilipoleta mradi wa kitambulisho. Tayari mamia ya watu wanakwama kukipata, hata wenye sifa stahili.
Ilivyo sasa, huwezi kuandikishwa ili kuingia kwenye daftari la kudumu la wapiga kura (DKWK). Waliobahatika kuwa nacho wameula. Wasiokuwa nacho, na wale vijana waliotimiza umri wa kupiga kura – kuanzia miaka 18 baada ya mwaka 2005, ndio walio katika mtihani.
Tangu awali, kitambulisho ilikuwa kazi kukipata kama huna sura ya kupigia kura mgombea wa CCM. Wanaohusika katika utaratibu wa kukipata wana ujuzi wa kutambua sura ya mtu na yule ambaye wanaona si mwenzao, hapati.
Kwa hivyo wanaohitaji kitambulisho sasa ni kama wanatafuta pepo ya Mwenyezi Mungu. Lazima wamuabudu Sheha. Kumuabudu sheha ambako ni dhambi kubwa kidini, kunategemea mengi. Hujui uende wakati gani. Usiku au mchana; au awapo na mkewe. Ni suala la kubahatisha.
Tume ingekuwa adilifu, ingechukua hatua kuhakikisha kila mwenye sifa ya kupiga kura anaingia kwenye daftari. Si adilifu na haitambui wajibu wake kwa jamii bali zaidi inaangalia watawala wanataka na kupanga nini?
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Salum Kassim Ali, anasema Tume haina ubavu wa kusaidia wanaokwama kupata kitambulisho. Ndo basi imetoka.
Haijali kwamba ina wajibu wa kumuingiza kila mtu mwenye sifa na inapaswa kumsaidia aingie. Tunalo tatizo Tanzania: hakuna mazoea ya kusaidia kurahisisha utaratibu haki ikapatikana. Mbaya zaidi pale wahusika wanapolea vikwazo.
Mkurugenzi wa uchaguzi anachojua ni "asiyenacho haandikishwi." Kama mtangulizi wake, Khamis Ali Ame, ndivyo anavyojiweka. Kwake si tatizo daftari likipungua watu hata wenye sifa. Hana cha kukosa. Moyoni mwake haumii hata chembe.
Anafuata nyayo za wanasiasa viongozi wa CCM. Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga wanasema "hakuna anayenyimwa kitambulisho." Nyanga anaongeza, "Ofisini kuna rufaa moja tu (ya mtu aliyenyimwa kitambulisho)."
Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Vitambulisho, Juma Ame, anasema hakuna aliyenyimwa kitambulisho na vipo yapata 8,000 ofisini kwao wenyewe hawajachukua.
Kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi ni kitanzi kwa wananchi. Ila naamini itafika siku kitaja kuwa kitanzi kwa viongozi waovu. Siku ni moja tu.
SOURCE: MWANAHALISI
 
Kila la kheir. Dhulma haidumu milele. Woooooote waliofanya dhulma Znz wapo wapi sasa? wama maisha gani?
 
Kila la kheir. Dhulma haidumu milele. Woooooote waliofanya dhulma Znz wapo wapi sasa? wama maisha gani?
Wengine ni wagonjwa taabani ,mkapa ana ukimwi na wengine wamewahi kuonekana sokoni wakiomba omba wagaiwe japo shilingi kumi .
 
Back
Top Bottom