Huu nao ni ufisadi, japo ni ufisadi dagaa nao unapaswa kukomeshwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu nao ni ufisadi, japo ni ufisadi dagaa nao unapaswa kukomeshwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Jan 10, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yupo mtu, raia wa Kenya aliwahi kuniambia kuwa, watanzania wote ni wezi. Nikamkatilia kata kata. Tukabishana sana, mwisho tukaachana bila kufikia muafaka. Lakini baadaye nikagundua kuwa, madai ya yule Mkenya yalikuwa na ukweli kwa asilimia kubwa. Ufisadi huu wa vidagaa unafanyika sana kwa wafanyakazi wa Serikali hasa hii ipo zaidi katika wizara ya elimu.

  Wakati wa kuajiriwa. Unakuta mtu Kwao ni Kigoma, kapangiwa kufanya kazi Kigoma. Lakini ukiingia katika faili lake utashangaa kukuta maelezo yanayoonyesha kuwa kwao ni Mtwara. Mtu wa Dodoma, anafanya kazi Dodoma. Lakini utashangaa mgogo naye kageuka kuwa Mhaya wa Bukoba.

  Mnyaru naye anadai kwao ni Tanga huku Mbondei anageuka na kuwa Mnyakyusa. Ilimradi kila mtu anafukuzia nyongeza ya vijisenti vya nauli wakati wa likizo. Sijui kwa yale makabila ambayo ndimi zao haziachi rafudhi ya asili kuongea kama wachaga, wakurya na wasukuma. Sijui inakuaje pale mchaga anapodai kwao ni Iringa! Hakika huu nao ni ufisadi pia.
   
 2. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  sasa kama serikali haitaki kuwaongeza mishahara wafanyeje?
   
 3. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Mambo ya serikali lege lege hayo bana.
   
 4. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Acha tu wafanye hivyo coz hawafanyi manunuzi yoyote ya kupata 10% japo wanafunzi wao wakishafika maofisini hawataki tena 10% ila wanakula 90%
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni system.. Ndiyo maana watu wanaona chama mbadala ni bora kuliko hiki kilichopo. Kila awamu kinapoendesha serikali,ni uozo unaoanzia juu.. Huko chini unakoongelea ni kwa waganga njaa tu! Nikupe mfano mmoja utashangaa. Kwamba,kuna fedha zinazotumwa kwenye H'shauri za nchi hii kwa ajili ya Ukimwi[chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii]. Mnapoandika mchanganuo, ndipo mnapopewa fedha. Cha ajabu,yule mhusika wa mfuko huo wizarani,hatumi fedha kabisa ama atatuma kidogo kwa zile H'shauri ambazo hazikuandaa mazingira ya kumpa % huyo bwana! Matatizo yanaanzia juu kwa kifupi.
   
Loading...