Huu mziki wa Makamanda tuliu-miss hata CCM wenyewe wanaukubali

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mara zote Chadema huwa ni watu wastàarabu watu wa furaha na hamasa tu that's all, tatizo CCM hawapendi kuona wenzao wakifurahi watafanya kila mbinu kuwachokoza wakizidiwa wanakimbilia polisi.

Tupingane kwa hoja sio kwa risasi, tukutane Feb, 17.




Hii ni amsha amsha tu ya makamanda kuonyesha wanaume wamerudi, CCM wasije kukimbia.
 
Kuzuia mikutano ya upinzani ni kati ya makosa makubwa sana ki mkakati.
Mara baada ya uchaguzi mkuu ilipaswa ile mikutano na maandamano viendelee CHADEMA na Lowasa wangechuja na kukinaiwa mapema sana na kuifanya CCM kutokuwa na kazi wala hoja ngumu dhidi yao.
Sasa hivi wananchi wanawa miss sana wapinzani, wana miss mikutano ya wapinzani na changamoto walizokua wanaziibua kupitia majukwaa ya mikutano ya kisiasa. Wananchi wameizoea sana CCM maana ndiyo wenye kibali cha kufanya mikutano wakati wote na popote, CCM siyo habari tena, inaishi kwa vituko na matukio wanavyo vitengeneza wenyewe. Kampeni za Kinondoni na Siha zitaongea zaidi na kuthibitisha haya niyasemayo.
Miaka fulani (nadhani mwaka 2001 au 2002) katika utawala wa rais Benjamin Mkapa aliwahi kusikika akisema "wana CCM wanalalamika kwa nini sisi hatufanyi mikutano wakati wapinzani wanafanya mikutano mingi kwa bidii, mimi nasema waacheni wapinzani wafanye mikutano mingi iwezekanavyo, kwa sasa hivi CCM tumeweka gear yetu kwenye Neutral, na muda utakapofika wa sisi kuanza mikutano wapinzani watakuwa washajichokea.
Hali ilivyo kwa sasa ni dhahiri tukifika mwaka 2009 ao 2010 CCM itakua imejichokea sana, wataishiwa vyote kitu ambacho kita warahisishia sana wapinzani. Uchaguzi wa Kinondoni na Siha unatarajiwa ndiyo utatumika kama kipimo kwa CCM kujipima taswira yake ilivyo kwa wananchi. Huenda mikutano ya kisiasa ikaruhusiwa baada ya uchaguzi huo. Maana ni dhahiri CCM itashindwa kwa aibu kuliko ilivyo shindwa wakati ule na hiyo ndiyo itakuwa sababu ya mikutano kuruhusiwa.
 
Back
Top Bottom