Huu mwenge ni wa uhuru, au ni mwenge wa utumwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu mwenge ni wa uhuru, au ni mwenge wa utumwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwananchit, Oct 6, 2012.

 1. m

  mwananchit Senior Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Wiki iliyopita nikiwa ndani ya basi la kutoka Tabora kuja Dar basi lilisimama kama dakika 40 hivi kwenye mpaka wa Tabora na Singida ili kupisha makabidhiano ya mwenge wa uhuru hivyo kusababisha kero kubwa kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara. karibia magari yote ya halmashauri husika, magari mengine ya serikari ha hata ambulance ya kubeba wagonjwa yalikuwa yameziba barabara. Sikuzisikia vizuri hotuba zilizokuwa zikitolewa, lakini nadhani kulikuwa na kupongezana kwingi na kusifiana sana kwa jinsi walivyothubutu na kuweza na kwamba kwa sasa wanazidi kusonga mbele bila kujali kwamba huko kunakoitwa mbele ni wapi!

  1. Wilaya zinazofanya vizuri kwenye mapokezi ya wenge wa uhuru, basi mkurugenzi wake hawezi kuondolewa hata akifanya madudu. Mkuu wa wilaya hiyo aweza hata kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa

  2. Watendaji wa halmashauri wanaotegea au kutoroka mikesha ya mwenge huo wanapewa maonyo makali na wanaweza hata kupoteza ajira zao

  3. Maandalizi ya mapokezi ya mwenge yanakuwa na vikao vingi vyenye posho, yanachukua muda mrefu na yanawahusika karibia wataalam wote kwenye halmashauri husika hivyo kuwanyima muda wa kutimiza majukumu yao mengine. mathalan, mhandisi wa wilaya anatakiwa kusimamia kwa dhati ujenzi wa majukwaa na mapambo katika maeneo yote mwenge utakapopiga kambi hivyo kumnyima muda wa kusimamia wakandarasi wanaojenga barabara na majengo ya serikali na mwisho wake utekelezaji wa miradi unakuwa ni mbovu. Ikumbukwe pia kwamba shughuli hizi zisizo na tija za kujenga majukwaa, nk zinajirudia hata kwenye mapokezi ya viongozi wa kitaifa

  4. Pamoja na wananchi kuchangishwa kwa nguvu ili kugharimikia mafuta ya mwenge ambao unywaji wake wa mafuta ni zaidi ndege kubwa za boeing, bado fedha za za serikali kami vile OC na nyinginezo zinatumika hivyo kuathiri bajeti kwa kiasi kikubwa. Licha ya mwenge, fedha nyingi pia zinatumika kwenye mapokezi ya viongozi wa kitaifa.

  Zamani tulikuwa tumeaminishwa kwamba kazi ya mwenge ni kuwamulika na kuwafichua wanyonyaji na mafisadi wengine, lakini kwa hali ilivyo sasa, inaelekea kazi ya mwenge imebalika na sasa unawamulikia mafisadi ili waone vyema fursa mpya za ufisadi kama kwenye sekta ya gesi na mafuta. Haiingii akilini kwamba miaka 50 ya uhuru bado tu mwenge wa uhuru unazidi tu kuwafichua wahujumu uchumi bila hatua zozote dhidi yao kuchukuliwa kama tulivyoona wenyewe kwenye zoezi lililoshindwa la kuvuana magamba.

  Nadhani sasa ni muda muafaka wa mwenge kupumzishwa ili utoe nafasi kwa vyombo husika kuwachukulia hatua wezi, majambazi, mafisadi na wabakaji wote wa uchumi wetu ambao wamekwishafichuliwa siyo na mwenge, bali wanaoitwa wapinzani. TUMENYONYWA KIASI CHA KUTISHA, TUMEFISADIWA KIASI CHA KUTISHA, TUMEDANGANYWA KIASI CHA KUTISHA, NA TUMEFANYIWA USANII KIASI CHA KUTISHA. SASA TUNATAKA UHURU WETU!

  Tanzania juu, juu, juu zaidi!
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Mwenge wa uhuni
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Huu mwenge ...to be honest inafika mahali tuseme basi...Bora hizo pesa zipelekwe kuboresha hospital kuliko kuziteketza for nothing
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mtu kama unataka kuhalalisha maono yasiyokuwepo ya chama chenu ni heri ukanyamaza ili usionekane punguani katika medani ya kisiasa.

  Kama mtu ambaye amesoma na kuelewa anashindwa kuthamini rallying points za kuleta ushirikiano nchini, huteleweka mtakwa yako ni nini haswa.

  Tujiulize pale viongozi wa chama fulani wanapo kaza makoo yao na kuimba piiipooooz! Maana yo nini haswa, kama si kuwa kusanya kwa umoja wale walio wao?
  Au pengine ni kuwatia mapepo hao wanachama wao?

  Si vizuri mtu mwenye akili kuleta mada ambazo majibu yate unayafahamu lakini kwa chuki zako.
  Watu kama mwenye mada hii wanaona ni heri kuvunja kikombe ili wote tusinywe chai.

  Kama chama chenu hakina sera zinazoeleweka zaidi ya kuandamana ni heri mumuulize mzee Mtei kwa muelekeo.
   
Loading...