Huu mwaka ni kama uliopita na Ujao. Salam kwa Watanzania daraja la kwanza

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Ndugu Watanzania!

Kwanza kabisa ningependa kuwasalimu kwa niaba ya Familia yangu. Na Pili nichukue nafasi hii kuwatakia Maandalizi mema Ya Krismas na Mwaka Mpya. Naukaribisha mwaka 2017 nikiwa katika matumaini yale yale ya miaka yote toka Taifa hili liundwe. Wakati huu naandika nasikiliza ule wimbo unaosema “ipo siku yangu”

Kwa miaka mingi Watanzania maskini wanaishi kwa matumaini. Kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Kila siku ikifika ni afadhali na jana. Usiku Mbu mchana Nzi. Lakini tunashukuru wale tunaowachagua watuwakilishe wao wanatuwakilisha kwenye mambo mengi sana. Ndiyo wanatuwakilisha kupata Matibabu mazuri, wanatuwakilisha kupata ELimu nzuri kwa familia zao. Wanatuwakilisha kupata Mishahara na marupurupu Mazuri. Si tuliwachagua wakatuwakilishe? Wanatuwakilisha huku sisi tuliendelea kuona Vumbi tu. Kwa mazingira yanavyozidi kwenda hata namba hatutaweza kuzisoma tutakuwa tunaona Vumbi tu.

Nyumbani kwangu hali ni ile ile ya maumivu masika tope kiangazi vumbi. Hakuna jema. Watoto wanasoma shule za kata tamaa ambazo zina walimu walokata tamaa. Wanangu kila siku akirudi nikiwauliza mmesoma nini wanasema hata hawakuelewa labda wakienda tena kesho maana mwalimu kasema wataonana kesho. Nlishukuru kuwa Elimu sasa ni Bure. Na kiukweli Imekuwa ELimu Bue Kabisa. Hili nalo tunapaswa sijui tushukuru au tusije tukakufuru. Ukipewa Shukuru. Tunapokea hivyo hivyo.

Watoto wa Wabunge wetu wao wanatuwakilisha kusoma zile shule nzuri nzuri. Si tuliwachagua wakatuwakilishe ? acha watuwakilishe. Wana siasa wao wanaendelea kupanda ngazi kwenda juu kwa kukanyaga mabega yetu.mungu awape nini?gunia la chawa?

Mwaka 2017 unakuja mwenzangu ananiuliza nimejipangaje mbona nalia lia tu. Namjibu tu inshallah maana hata sioni kama kuna ishara yoyote ya kuboreshewa maisha. Wanasema tujitume… unawezaje kujituma kwenda sehemu ikiwa huna hata nauli? Na bado huwezi kumtuma mtu pia.

Wanasema tuchape kazi. Tujishughulishe. Lakini mbona wao hawatuoneshi kujishughulisha huku ni kupi?wanatumia kodi zetu kwa maendeleo yao. Sisi wengine mnatuchanganya mnapozungumzia kuendelea kufungua mviwanda vya kutengeneza keki wakati maandazi na vitumbua vinatushinda. Hizo keki si mtakuwa mnauziana wenyewe?

Naumia sana naposikia kuwa mpaka mwaka huu tunaondoka kuna matukio ya watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Bado wanakufa watu wanazikwa pasipo uchunguzi mkubwa sana kufanyika. Lakini alipokufa faru yohana hilo suala limevaliwa njuga na kutaka maiti yake ifukuliwe kwa uchunguzi. Nawaza sana nagundua ni kudra t undo zinatuweka hai.

Kila mwaka tunasema hili nalo litapita. Lakini mbona hayeshi? Yapo kila siku? Wakuu muwe na huruma. Nasi pia tunapenda kuishi kama ninyi. Kwa nini mnatuanzishia Jehanamu hapa hapa duniani? Kwa nini mmeanza kutuhukumu tuishi kama mashetani nanyi mnaishi kama malaika? Ni vyema wote tuishi kama malaika maana hatutaki kaa na mashetani huku mitaani.

Mwaka unakatika.mshahara wangu nalipia kodi ya nyumba, nauli na kidogo chakula. Ila mkiwa kwenye raido na tv mnasema tujifunze ku sevu pesa. Nina watoto 3 napokea tsh 400,000 kwa mwezi. Nlilipie maji,maji,mkaa,kodi ya nyumba,chakula,nauli ya mimi kazini. Matibabu ikitokea ugonjwa. Bado unanambia nisevu ? nasevu nini hapo na wakati najikuta nadaiwa? Kwa nini huwa mnapenda kututukana kwa lugha za reja reja hivyo? Ni rahisi sana kusema nenden mkajiajiri.

Ni kweli kuwa tunajiajiri bila mitaji nab ado katika mishahara hiyo makato lukuki? Kwa nini mnapoteza nguvu nyingi katika mambo yasiyo na faida na kutotumia nguvu kabisa katika mambo ya faida?lile mnalopaswa kulitenda hamlitendi na lile msilopaswa ndo mwatenda kila siku?

Naona kama sina ndugu wa kuweza kunisaidia. Nikifa leo au kesho hata maiti yangu ni bure itazikwa tu kama mbwa na watu wanisahau palepale. Sijajua nitaitwa mhaiaji haramu,mkimbizi au jambazi. Wakuu muwe na huruma na sisi pia ni binadamu.

Mwaka 2017 unakuja, tofauti yake itakuwa kwenye kuandika tarehe tu lakini kiuhalisia hakutakuwa na jingine jipya. Kila ziku zinavyoenda afadhari na jana. Nawasalimu watanzania wenzangu.

Salamu hizi ni kutoka huku ninakoishi ambako nako ni Ikuru yangu Mimi na Familia yangu au Black House kwa jina la kiingereza.
 
Back
Top Bottom