Huu Muziki wa Kijeshi wa China siyo mchezo: China sasa hivi siyo ya kuchezewa wako fiti

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
6,476
2,000
Wa kawaida sana, ukilinganisha na wababe wenzake kama USA na RUSIA... ila kwetu huku huo ni mziki haswaaa ... ambao hatuwezi kuucheza
Naona unavichukulia poa hivyo vyombo

Hapo kuna Dongfeng-17 hizo ni hypersonic missiles, inaweza kupiga Aircrfat carrier yoyote ya Marekani hata zilizoko huko Guam, Kwa sasa Marekani hana bado hiyo kitu

Pia hapo kuna Dengfeng 41- Hiyo inaweza kwenda umbali wa km 12000 hadi 15000 na inabeba warheads 10 na kila moja inaweza kupiga target tofauti. Hiyo ni strategic missile ya kubeba vichwa vya nyukilia na inaweza kupiga target yoyote ndani ya Marekani.

Vita vya ardhini kwa sasa Mmarekani hatii mguu, sasa hivi China ana 5 generation Stealth aircraft zinazoitwa J-20 na yupo anatengeneza Aircraft carrier zake mdogomdogo.

Mpe miaka 10 tu mtamulewa!
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
6,476
2,000
China as a nation under the root of all evils CCP makes me sick!

Nchi isiyojali haki za wanadamu sio nchi,ni mavi kama mavi mengine!
In the last 50 years Marekani kaua watu wengi zaidi duniani kuliko mchina
Kaua watu milion Iraki
Kaua watu zaidi ya Milioni Vietnam kwa vita bogus
Kaua watu kibao wasio na hatia Afghanistan
Huko Marekani Black people bado wanabaguliwa kimya kimya, rejea mashambulizi ya mapolisi dhidi yao!

Hiyo USA unayoihusudu ni biggest violator wa haki za kuishi za watu duniani
 
Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
10,744

Bro bora USA kuliko China ..bora akubague mzungu wa USA kuliko mchina wa uchina, hayo mawatu sio mabaguzi tu ni makatili kabisa, muzungu anaeza kukubagua lakini akakupa haki yako furesh ..sasa miwatu ya mimacho midogo ni mashetani hadi mwisho..

NB: Marekani atabaki kuwa baba wa dunia kwa miaka mingi ijayo ..hizi Russia, China cjui Iran wanarukaruka tu...
 
login-logout

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
278
500
Naona unavichukulia poa hivyo vyombo

Hapo kuna Dongfeng-17 hizo ni hypersonic missiles, inaweza kupiga Aircrfat carrier yoyote ya Marekani hata zilizoko huko Guam, Kwa sasa Marekani hana bado hiyo kitu

Pia hapo kuna Dengfeng 41- Hiyo inaweza kwenda umbali wa km 12000 hadi 15000 na inabeba warheads 10 na kila moja inaweza kupiga target tofauti. Hiyo ni strategic missile ya kubeba vichwa vya nyukilia na inaweza kupiga target yoyote ndani ya Marekani.

Vita vya ardhini kwa sasa Mmarekani hatii mguu, sasa hivi China ana 5 generation Stealth aircraft zinazoitwa J-20 na yupo anatengeneza Aircraft carrier zake mdogomdogo.

Mpe miaka 10 tu mtamulewa!
Kwaiyo kipindi mchina anapiga Marekani atakuwa amelala ? China bado hajafikia uwezo wa Marekani bado.. isipokuwa USA na CHINA vita ikitokea hao watapigana, ila mchina atapigwa, nae Marekani atashinda ila hali yake kiuchumi itakuwa mbaya..... hizo 5 generation kwani anazo peke yake ? Even USA anayo madude ya kupiga bara to bara
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
6,476
2,000
Bro bora USA kuliko China ..bora akubague mzungu wa USA kuliko mchina wa uchina, hayo mawatu sio mabaguzi tu ni makatili kabisa, muzungu anaeza kukubagua lakini akakupa haki yako furesh ..sasa miwatu ya mimacho midogo ni mashetani hadi mwisho..

NB: Marekani atabaki kuwa baba wa dunia kwa miaka mingi ijayo ..hizi Russia, China cjui Iran wanarukaruka tu...
Ilichukua marekani miaka 300 kuwa hivi ilivyo tena kwa kufanya udhalimu mkubwa kama vile biashara ya utumwa, kuua wahindi wwkundu mamilioni, kupiga nchi nyingine kuiba resources, lakini China haijafanya udhalimu kama huo,

imewachukua wachina miaka 70 tu (japo ni taifa kongwe duniani, hata misri nao ni taifa kongwe pia lakini hawana kitu)
Wape wachina miaka mingine 20 uone shughuli yake

Hao unaowaita wavimba macho wamekujengea reli ya TAZARA na walikusaidia mno kwenye vita ya Kagera
 
ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
2,174

Sema chief una mahaba kweli yani alafu pia una chuki na kwa mantiki hiu ni ngumu wewe kujadili hoja rationally sababu mara zote maneno yako yanaakisi chuki uliyonayo dhidi ya USA na mahaba uliyonayo kwa wachina, mfano umesema wachina wapewe miaka mingine 20 watakuwa wamempita USA swali ni je USA yeye atakuwa amesimama au yeye ataacha harakati zake za kuendelea kujijenga? Jibu ni hapana kama china anavyojijenga uku akiota na kutamabi kuwa kama USA, basi na USA mwenyewe halali wala hapumzik,i anapambana ili siku zote aendelee kuwa wa kwanza, ivyo izo unazosema wewe ni ndoto ambazo haziakisi uhalisia wa mambo ulivyo.
 
rate ya development ya wachina ni ya kasi ya kutisha zaidi kuliko Marekani
Hebu angalia China ya mwaka 1960 na China ya leo, ni tofauti sana.

Hawa wachina wa leo nao wana mission za mwezini kama ilivyokuwa wamarekani.

Wachina wanaongoza kwa Patents za kitafiti nyingi kuliko Wamarekani.

Wachina wanawadai Wamarekani mapesa mengi, wakati wachina wao hawana deni bali wana surplass wakati Wamarekani wana deni kutoka vyanzo mbalimbali duniani zinazofikia dola Trilion 20.

Sasa hivi anachokifanya mchina ni kujenga navy na airforce ya ukweli, baada ya hapo kijeshi Marekani atakalishwa!.

Wakati huko Marekani wanajihusisha na Ndoa za mashoga na mambo ya. kipuuzipuuzi kama kuvamia nchi mbalimbali duniano kuleta machafuko, kupiganisha vita ili waibe resources, China yenyewe inakuletea dili la WIN-WIN. hawaingilii siasa yako ya ndani bali utajiju mwenyewe!
Marekani iko tayari kuua viongozi wa nchi mbalimbali wazalendo ili wasimike vibaraka, China hana mambo ya hivyo
 
bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,128
2,000
Daah
Kwanza kabisa, naona hapa kuna mtu anatishwa, anaambiwa aangalie upya sehemu ya maamuzi yake.
Pili, kiukweli jamaa wameweka pesa jeshini. Kumbuka hii ni ya maonesho tu, je stock halisi iliyopo? na ukiangalia kuna ndude inaonekana ni nzito balaa, maana idadi ya tairi tu zinazobeba inatisha
Mwisho, binadamu ni mtu wa ajabu sana. Imagine anakaa anawaza jinsi ya kuuwa watu wote ikiwezekana ili kubance power tu
Iasee, Mwenye nguvu mpishe lakini. Tunamshukuru mchina kwa hatua hii mujarabu kabisa. Sisi bado tunapambana kujenga vyumba vya madarasa
 
ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
6,754
2,000
Naona unavichukulia poa hivyo vyombo

Hapo kuna Dongfeng-17 hizo ni hypersonic missiles, inaweza kupiga Aircrfat carrier yoyote ya Marekani hata zilizoko huko Guam, Kwa sasa Marekani hana bado hiyo kitu

Pia hapo kuna Dengfeng 41- Hiyo inaweza kwenda umbali wa km 12000 hadi 15000 na inabeba warheads 10 na kila moja inaweza kupiga target tofauti. Hiyo ni strategic missile ya kubeba vichwa vya nyukilia na inaweza kupiga target yoyote ndani ya Marekani.

Vita vya ardhini kwa sasa Mmarekani hatii mguu, sasa hivi China ana 5 generation Stealth aircraft zinazoitwa J-20 na yupo anatengeneza Aircraft carrier zake mdogomdogo.

Mpe miaka 10 tu mtamulewa!
ICBM zote zina hypersonic speed!

Ili kuweza kuipiga carrier lazima upenye ulinzi wa meli vita nyingine zinazoisindikiza hyo carrier ambazo zina ulinzi dhidi ya makombora pia zina makombora ya kushambulia pia bila kusahau submarine ambazo pia hua zinaisindikiza hyo carrier.
Kumbuka mpaka sasa nchi zenye high tech missile warning systems ni USA & Russia mchina hana Teknolojia hiyo hvyo kombora linavyotoka China tu Marekani wana kua wanauezo wa kujibu haraka kuliko kombora litoke Marekani kwenda China,China watakuja kugundua likishatua ardhini.

Marekani ana makombora ya Trident ambayo ni SLBM yanabeba vichwa 8 vya nuclear,na ni vigumu kuyazuia sababu unakua hujui mahali ambapo nyambizi ilipo ukilinganisha na ballistic missiles za ardhini hao kina Dongfeng

Ndege za stealth mchina kacopy na kupaste toka F-22 na F-35 hata ukizitizama kwa macho tu ni ngumu sana kuona tofauti. Sio Ndege tu hata Reaper drone mchina kacopy katoa yake.
Hizo J-20 za mchina mpaka leo hazijaanza kazi pia hazina engine za fifth generation fighter zinatumia engine za warusi, ni target ya heat seeking missiles.

Mpaka sasa hakuna nchi ya kuishinda Marekani kwenye convectional warfare na kwenye nuclear hakuna nchi zinazifikia Russia & Marekani, labda tungoje miaka hiyo ijayo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom