Huu muswada utazaa vyama imara huku vyama vya uongo uongo vikifa- isipokuwa hiki kifungu cha 6

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,318
HUU MUSWADA UTAZAA VYAMA IMARA HUKU VYAMA VYA UONGO UONGO VIKIFA- ISIPOKUWA HIKI KIFUNGU CHA 6

Leo nimemaliza kusoma muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa 2018, naweza kusema kwa uhakika na uhuru kamili kuwa 98% ya muswada huu ni mzuri sana iwapo tunataka vyama vya siasa viwe taasisi imara za umma zinazosimamia uwazi na uwajibikaji kuanzia ndani. Lakini wahenga waliwahi kunena kuwa, hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro.

Muswada huu wa sheria umemfanya Msajili wa vyama vya siasa kuwa mamlaka na madaraka kamili kama ambavyo mamlaka mbalimbali huanzishwa ili kusimamia nyanja mbalimbali kuleta ufanisi, Ofisi ya msajili imekuwa mamlaka inayosimamia, kuratibu na kudhibiti shughuli za vyama vya siasa kwa kuzingatia maadili ya taifa, miiko ya taifa na misingi ambayo taifa letu limeanzishwa kwayo. Kiufupi, muswada huu umempa meno zaidi msajili ktk kuhakikisha kuwa taasisi hizi zinayaishi mahubiri yao ya uwazi, uwajibikaji, uhuru wa mawazo, demokrasia ya ndani na nidhamu ktk fedha za umma.

Pamoja na uzuri wake, binafsi nimebaini udhaifu ktk baadhi ya vipengele, kitu kingine ni kuwa muswada huu umeacha baadhi ya mambo mengine ambayo hayakupaswa kukosekana. Kipengele ambacho nimeona kinahitaji kutazamwa kwa uangalifu ni kifungu cha 6.

Kipengele hiki kinahusu "Ulinzi wa Maafisa" na kinasomeka kuwa, sheria kuu inafanyiwa marekebisho kwa kufuta kifungu cha 6 na kuingiza kifungu kipya kama ifuatavyo: -

" 6. Hakuna shitaka lolote litakalofunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi au Maafisa wengine chini ya Msajili kwa kitu chochote kilichofanywa au kilichoachwa kufanywa kwa nia njema katika kutekeleza kazi yoyote chini ya sheria hii. "

Hiki ni kipengele kizito sana kinachoweza kuleta faida ndogo na hasara kubwa ktk demokrasia iwapo kitaachwa kama kilivyo. Kiuhalisia ni kuwa msajili, wakurugenzi na wasaidizi wake ni binadamu, hakuna binadamu asiyekosea ktk maamuzi, ni busara sana kuwa na sheria ambayo iwapo utekelezaji wake unategemea nia njema ya msajili au wasaidizi wake basi maamuzi yao yaweze kuhojiwa mahakamani ktk kuhakikisha kuwa aliyetoa maamuzi amefuata taratibu zote kwa haki mpaka kufikia maamuzi husika.

Hivyo, iwapo msajili anajua anaenda kusimamia sheria na katiba, tusimzuie kushtakiwa ktk maamuzi yake atakayoyafanya wakati wa kuitekeleza hii sheria, cha msingi kifungu hiki kiongezewe vifungu vinavyoweza kuelezea mazingira ambayo msajili kama ofisi hawezi kushtakiwa kwa maamuzi yake na mazingira ambayo msajili au wasaidizi wake wanaweza kushtakiwa nk.

Ikiwezekana kifungu hiki kiboreshwe kwa kutaja mpaka ukomo wa muda ambao shauri dhidi ya msajili au ofisi yake linapaswa kuwa limesikilizwa na mahakama ili kurahisisha maamuzi iwapo kuna 'deadline' ambayo vyama au wanachama wanapaswa kuifikia ktk michakato mbalimbali ya kidemokrasia. Kanuni za sheria ya vyama vya siasa inapaswa kuwa wazi sana kuhusiana na hili, ili kuweka mazingira ya haki kwa vyama/wanasiasa na uwajibikaji kwa ofisi ya msajili.

Sasa msajili wa vyama vya siasa ukimpa kinga ya aina hiyo ya kutoshtakiwa ipo siku atafanya maamuzi ya ajabu mpaka tutabaki midomo wazi kwakuwa hatutakuwa na pa kumpeleka kisheria. Kwa mamlaka na madaraka makubwa ambayo sheria hii imempa msajili kama msajili, mdhibiti na msimamizi wa hivi vyama, siyo busara kumpa kinga ya kutoshtakiwa.

Mwaka 2015 tulishuhudia uchaguzi wa urais Zanzibar ukivurugika na hata kufutwa kwa uchaguzi huo, moja ya sababu kuu iliyopelekea uamuzi huo ni kwamba makamishna wa tume ya uchaguzi waligeuka na kuwa mawakala wanaowakilisha maslahi ya vyama vyao ndani ya tume kinyume na sheria ya iliyoanzisha tume ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi. Kwa mujibu wa sheria tulitarajia makamishna wa tume wawe 'neutral' lakini tuliona kilichotokea, je tuna uhakika gani kwamba msajili wa vyama vya siasa, wakurugenzi wa Ofisi yake na wasaidizi wake waya kuwa 'neutral' ktk maamuzi yao?

Huenda aliyependekeza hiki kipengele alijua kuwa siku zote msajili au wasaidizi wake hawakosei, au ni watu wa upande wake kwamba maamuzi ya msajili yasiyohojiwa popote hayatakuja kumuumiza siku za baadae. Lakini binafsi nimeona hiki kipengele ni udhaifu mkubwa sana wa hii sheria, maana hata msajili akiteleza au akikosea kwa makusudi ktk maamuzi yake yanayoweza kuwa yameshikilia hatma ya chama au wanachama wa chama cha siasa ktk mchakato wa kidemokrasia hakuna sehemu ya kwenda kujiridhisha iwapo msajili au wasaidizi wake walitenda haki kwa mujibu wa katiba na sheria hii.

Uzuri wa huu muswada na madhaifu mengine ya huu muswada nitayaeleza kesho

Magoiga SN
 
mkuu huu muswada umeelezwa na kuchambuliwa kua una madhara makubwa kuliko hayo mazuri unayosema utayaleta, hivi mpaka watu waende mahakamani unadhani ni wajinga? acha utumwa wa akili!
 
Mswada huu inaisababishia machafuko ndani ya nchi, bunge lisipitishe Muswada huu.wabunge wa ccm wajitafakari upya maana unawahusu hata wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom