Huu mti unahusishwa na suala la ushirikina. Je, kweli?

rungemba

Member
Nov 23, 2013
76
6
Habri wana jamvi.. Kuna huu mti unatumika Sana Kama mapambo na
1475819660071.jpg
kivuli ktk nyumba zetu.. Kuna mgen alinitembelea akanambia Mti huu unahusishwa na ushirikina. Mikosi magonjwa na nuksi ktk nyumba. Kwa anaejua ukweli au tusaidiane kutafiti
 
Habari hii inaukweli nadhani.
Nimeshuhudia watu wengi sana waliokuwa wamepanda hii miti "uzazi wapango" waliokuwa wameipanda jirani na Nyumba zao, walishaifyeka kwa imani kama hizo. Mwenye ukweli wa kisayansi atuweke wazi.
 
Ni panga uzazi, maana yake hautoi matawi hovyox2, yanatoa kwa awamu na uzazi mmoja hutambaa pamoja.
Hiyo ya mikosi ni kuwa watu hudhani ukipanda nyumbani mizizi ikaingia ndani basi wewe na mkeo mlizaa hovyo basi watu wanakufa. Hasa wajaluo huamini hivyo.
Haina ukweli wowote, nyumbani kwangu nimepanda zaidi ya 15
 
Mkuu,niliipanda pia kwenye nyumba yangu,nikaambiwa tahadhari hiyo ila nikapuuza vikali.Leo hii ninavyoongea,familia yangu imesabaratika,maisha yalivurugika vibaya hadi niliuza nyumba,mikosi iliyotokea nusura maisha yangu na ya mwanangu yapotee.Ni kwa neema ya Mungu tu nipo hadi sasa.Nalazimika kuamini ingawa mimi ni mgumu sana kuamini vitu hivyo.
Na pia imenipa changamoto ya kuyatizama maisha kwa namna tofauti sana na nilivyoyatizama awali.Kweli dunia hii ina mambo magumu sana,nikipita kwenye nyumba yangu hiyo,huwa machozi yananilenga na macho hubadilika kuwa mekundu..maumivu huwa makali moyoni hasa nikikumbuka jinsi nilivyowapenda wanangu..niliuza kila kitu mf.gari na kugawa vingine.Nilipata mikosi kazini na kufikishwa mahakamani.Nashukuru Mungu nilishinda kesi na naendelea na maisha.
 
Duuùuu pole mkuu
 
Jamani hizi imani mkiziendekeza mtaharbikiwa kwa ujinga tu. Msiamini vitu visivyokubalika. Nina mti kama huo kwa miaka zaidi ya 10 na maisha yanendelea tu
 
nimeshasikia habari kama hizi kwa baadhi ya miti...

mti wa mbilimbi na mti wa hina ni miti yenye kuleta mikosi na bahati mbaya kwa wakazi wa hiyo nyumba..

maua ya jasmin ile harufu yake inaita majini...

mti wa mkungu ni makazi ya majini..

kwa upande wangu sijawahi kuthibitisha ukweli ni upi, ivyo naona ni iman potofu kwa jamii isiyo elimika...
 
Mkuu,niliipanda pia kwenye nyumba yangu,nikaambiwa tahadhari hiyo ila nikapuuza vikali.Leo hii ninavyoongea,familia yangu imesabaratika,maisha yalivurugika vibaya hadi niliuza nyumba,mikosi iliyotokea nusura maisha yangu na ya mwanangu yapotee.Ni kwa neema ya Mungu tu nipo hadi sasa.Nalazimika kuamini ingawa mimi ni mgumu sana kuamini vitu hivyo.
Na pia imenipa changamoto ya kuyatizama maisha kwa namna tofauti sana na nilivyoyatizama awali.Kweli dunia hii ina mambo magumu sana,nikipita kwenye nyumba yangu hiyo,huwa machozi yananilenga na macho hubadilika kuwa mekundu..maumivu huwa makali moyoni hasa nikikumbuka jinsi nilivyowapenda wanangu..niliuza kila kitu mf.gari na kugawa vingine.Nilipata mikosi kazini na kufikishwa mahakamani.Nashukuru Mungu nilishinda kesi na naendelea na maisha.
Pole sana mkuu usikate tamaa utafanikiwa zaidi ya mwanzo Usikate tamaa
 
Dah hii miti nyumbani kwa wazazi wangu ipo kama 12 ,kwangu nina minne na hayo unayo yasema hayapo

Ila pole kwa uliyo yapitia
 
Back
Top Bottom