Huu Mtazamo wa vyombo vya habari kuwa Vita uwaathiri zaidi wanawake na watoto ni Mtazamo usio na mantiki

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,042
10,463
Ukweli ni kuwa Vita vina madhara kwa jamii nzima bila kujali jinsia au umri. Kutambua kuwa Vita vina madhara kwa wanawake na watoto tu tafsiri yake ni kuwa mwanaume ni mtu asiyekuwa na thamani katika ulimwengu huu kiasi kwamba mabaya yanapomkuta inakuwa ni sawa kwake kulinganisha na wengine ambapo yanapo wakuta wanastahili kuonewa huruma.

Ikumbukwe Kuna wanaume wengi waliopoteza viungo vyao na hata maisha kwenye uwanja wa vita kwa lengo la kulinda jamii zao hususani wake na watoto wao dhidi ya adui Leo hii kuona kuwa wanaume sio waathirika wakubwa wa vita ni kutotambua mchango na juhudi za wanaume katika kupambania maslahi ya jamii.

Ifike wakati vyombo vya habari na mashirika ya kutetea haki za binadamu muache ubinafsi kwa kutoegemea katika jinsia ke pekee yake bali mfanye shughuli zenu kutokana na hali halisi ilivyo kwani kutetea haki za wanawake na watoto hakuwapi uhalali wa kutotambua juhudi za wanaume kumbukeni sisi ndo waume na baba zao.

Mwisho Kila mtu anastahili heshima yake bila kujali jinsia au umri kwani mwanamke atabaki kuwa mwanamke na mwanaume atabaki kuwa mwanaume.

From northern part of Tanzania.
 
Ni kweli Vita huwaarhiri saana wanawake na watoto Kwasababu wanaume wengi hufa na kupata ulemavu kwaiyo hukosa nguzo ya kuegamia na kupoteza viongozi
Mwanaume hujipambania na kupambania watu wake kwa Hali na mali. Mwanaume atakaa juu siku zoote iyo inajulikana ndo maana hata hakuna anaejisumbua kumuongelea Kwasababu ipo wazi inajulikana kijamii na kidini pia.
 
Back
Top Bottom