Uongoz wa soko umewazuia watu kujenga mpaka watakapoleta greda ili kusawazisha,wafanyabiashara wamepinga na kupelekea kuamua kulala hapohapo sokon ili kuzuia utekelezaj wa maamuz ya uongoz wa soko.
 
Kumbeee! Kwahiyo ripoti ya kuchunguza jambo lilitokea sio "research"? Your research lecturer was very brilliant!!!
Tofautisha kati ya utafiti na uchunguzi!Uchunguzi hufanywa kubaini chanzo Cha jambo lililokwisha tokea!
Huwezi Kuta eti Polisi anasema anafanya utafiti kwenye kesi kumbaini mtuhumiwa,hiyo ni blunder!
 
IMG_0570.jpg
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amesema uchunguzi umebaini kuwa mshumaa uliowashwa na mateja ndio sababu ya kuungua kwa soko la Karume na kusema anaamini jeshi la polisi litakuchua hatua stahiki kwa wahusika kwa kuwa wanajulikana.

“Sasa zile hisia za nani kachoma nini, mmeona wenyewe, tumeelezwa na mmemsikia Jose amejitoa mhanga ameeleza kwamba tusipoteze muda aliyechoma soko ninamjua, ninaamini jeshi la polisi litachukua hatua stahiki kwa sababu watu hao wanajulikana,” amesema RC Makalla.

Mshumaa Ndio Umeteketeza Soko la Karume

My take...

Mimi najaribu kuwaza, huyu aliyemuona huyo teja akiangusha mshumaa alichukua jitihada gani kuzuia hili janga lisitokee? Lakini kwa nini isiundwe tume maalum kabisa kufanya tafiti na kuja na majibu kuhusu hii choma choma ya masoko maana imekithiri sasa. Zilianza shule kuchomwa moto karibu mwaka mzima, wananchi wakiwa hawajui chanzo, leo yameanza masoko kuteketea. Kuna haja ya kulitazama hili kwa jicho la kipekee.
 
SERIKALI YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUREJEA KARUME KWA MPANGO MZURI.

- Umati walipuka kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.

- RC Makalla apokea taarifa ya ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza Chanzo Cha Moto.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameruhusu Wafanyabiashara wa Soko la Karume kurejea na kuendelea na Biashara kwa kuwekewa Mpango mzuri ambapo Wafanyabiashara wa Soko hilo wamepongeza uamuzi huo na kuishukuru Serikali.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na Wafanyabiashara hao Mara Baada ya kupokea Taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo Cha Moto, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Rais Samia ameelekeza pia uwepo utaratibu mzuri wa kuzuia Moto, kuhakikisha hakuna atakaedhulumiwa eneo lake na kutoa ruhusa kwa Wafanyabiashara kujenga Vibanda kwa gharama zao.

Kuhusu Ripoti ya chanzo Cha Moto, RC Makalla amesema Kamati imebaini Moto huo ulitokana na Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya "Mateja".

Aidha RC Makalla amesema Baada ya kupokea ripoti hiyo ataikabidhi kwenye Mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji wa maoni na Mapendekezo yote ya Kamati.

Miongoni mwa Maoni na Mapendekezo ya Kamati hiyo Ni pamoja Ujenzi wa Soko jipya linaloendana na Hali ya Sasa na vizimba kutolewa kwa kipaombele kwa wazawa, uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia Moto, Barabara za kuingia na kutoka, Ujenzi wa Majengo ya Muda mfupi, Kila mfanyabiashara kuwa na bima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na Kuungua Hilo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 7.2 ambapo idadi ya Wafanyabiashara waliokumbwa na janga Hilo Ni 3,090.

Pia soma:

- Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati (18/01/2022)
View attachment 2094094
Kwaiyo ni mshumaa..
sawa kazi endelee
 
Kwa hiyo mateja walijenga mpaka kibanda cha kuvutia unga hapo sokoni na hakuna aliyechukua hatua!
Sasa mkuu wa mkoa, wilaya na kamanda wa polisi wanasubiri nini kuachia ngazi?
 
RC na Rais wanajidai mateja hawawezi kutajwa kwa ajili uchunguzi unaendelea kumbe wanawasitiri vigogo wa madawa ya kulevya.
Halafu mtazame yule Kamanda wa polisi. Anaonekana kama vile hapendi mambo yanavyokwenda. Anaonekana kama vile watu wanamburuta.
 
Uzuri wake haya malalamiko yote Leo yamemalizwa wamewekwa kundi maalum wanasubiri bilioni 5 wapewe maana wameahidiwa wamesahau kabisa kwamba mitaji yao imeungua pale.

Leo hawajakaa kutafakari kauli za Rais wameishia kushangilia ujinga.

Rais ameshasema ametoa pesa ya kujenga soko la Kariakoo, ametoa pesa ya kujenga soko la Jamgwani na baada ya hapo hao wa Karume itabidi wapishe pajengwe soko kubwa la kisasa lenye uwezo wa kutoa huduma kwa masaa 24.

Kauli hii inashabihiana sana na wale waliokuwa wanadai kwamba soko limechomwa ili kuwaondoa hapo kidizaini wasirudi na apewe mwekezaji.

Nilisikia hizi tuhuma kutoka kwa haohao machinga ambao leo wameyaziba masikio yao kwa pamba au kwa makusudi ili mradi wachache wameshapata Chao kidogo kitu.

Nawakumbusha ndugu zangu wamachinga kwamba hapo Karume hamtakaa muda si mrefu mtahamishiwa Jamgwani na hapo anapewa mwekezaji maana hata Rais Leo ametamka hilo pamoja mmeamua kunyamaza au kunyamazishwa au kujifanya hamjasikia alichosema leo.
 
Pale Karume litajengwa soko la kimataifa lenye hadhi na litafanya kazi 24/7.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amesema uchunguzi umebaini kuwa mshumaa uliowashwa na mateja ndio sababu ya kuungua kwa soko la Karume na kusema anaamini jeshi la polisi litakuchua hatua stahiki kwa wahusika kwa kuwa wanajulikana.

“Sasa zile hisia za nani kachoma nini, mmeona wenyewe, tumeelezwa na mmemsikia Jose amejitoa mhanga ameeleza kwamba tusipoteze muda aliyechoma soko ninamjua, ninaamini jeshi la polisi litachukua hatua stahiki kwa sababu watu hao wanajulikana,” amesema RC Makalla.

Mshumaa Ndio Umeteketeza Soko la Karume

My take...

Mimi najaribu kuwaza, huyu aliyemuona huyo teja akiangusha mshumaa alichukua jitihada gani kuzuia hili janga lisitokee? Lakini kwa nini isiundwe tume maalum kabisa kufanya tafiti na kuja na majibu kuhusu hii choma choma ya masoko maana imekithiri sasa. Zilianza shule kuchomwa moto karibu mwaka mzima, wananchi wakiwa hawajui chanzo, leo yameanza masoko kuteketea. Kuna haja ya kulitazama hili kwa jicho la kipekee.
hawa wanasiasa muda wote wanafikiria watanzania bado ni wale wale wa 1977 february tarehe 5, na kuna baaadhi yao huenda wana kazi maalum , huyu makala alipokuwa mbeya soko la chimala kila mara likiungua, kaja dsm ni yaleyale ...................!!!!
 
Back
Top Bottom