Huu mkwara wa Waziri Seleman Jafo kwa Wakuu wa Mikoa unamuhusu pia na RC Makonda?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Akiwa anaongea ' mubashara ' kabisa sasa hivi kupitia Kipindi cha 360 cha Clouds tv Waziri mpya wa TAMISEMI, Mchezaji mpira / kandanda mzuri tu wa zamani na mtoto wa mjini hasa Seleman Jaffo amesikika akisema ' Kauli ' ambayo ni ya ' Kimkwara ' kabisa kwa Viongozi walio chini yake hasa Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

Waziri huyo wa TAMISEMI Jaffo amesema namnukuu..." Nawaomba Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote nchi nzima kuhakikisha kuwa katika maeneo yao kunakuwa na Maendeleo makubwa, wasimamie vizuri Sera za Serikali na wawe Wabunifu na zaidi ya hapo hatutaelewana kabisa kwani sitaki ugoigoi chini ya huu Uongozi wangu "...mwisho wa Kumnukuu.

Namalizia kwa swali ' dogo ' tu je haya maneno ya Jaffo yanamuhusu pia / moja kwa moja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul C. Makonda ambaye ana ushawishi mkubwa Serikalini na kwa ' Taita ' mwenyewe wa Magogoni au inawahusu tu Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya wa Mikoa mingineyo?

Na swali pia la ' nyongeza ' hivi ' Kiitifaki ' kati ya RC Makonda na Waziri Jaffo ni nani ana ' Cheo ' kikubwa kuliko mwenzake? Na je ni nani anatakiwa kuaminika haraka / upesi mbele ya ' Taita ' wa Magogoni kama pakiwa na tatizo?

Naamini leo nitapata majibu ' Kuntu ' kabisa hasa kutoka kwa Members wa JF ambao huwa nawaamini siku zote ni Watu Werevu / Vipanga sana na hakuna hata siku moja wamewahi kuniangusha katika kunipa ' ufafanuzi ' wa jambo ambalo huwa nina ' utata ' nalo.

Nawasilisha.
 
Nadhani Bashite alisha wahi kutolea ufafanuzi suala la nani yupo juu. Ilikua ni kipindi kile cha Sakata la Nape na clouds. Alisema yeye hawezi kuhojiwa na tume iliyoundwa na waziri, akaenda mbele zaidi na kudai kuna watu wamejisahau sana kwenye hivi vyeo sababu hakuna tofauti kati ya waziri na RC, sababu hata mishahara yao alisema wana lingana.
 
Huyu aliyeleta tangazo la chapati maker apewe ban hajui taratibu za humu Jf, hapa sio instagram mtu anahoji unaweka picha ya chapati maker

Kuna anachokitafuta Kwangu Mkuu na soon atakipata kwani nadhani hata Yeye ananijua kabisa kwamba huwa ' simcheleweshi ' Mtu pale nikigundua kwamba ' anawashwawashwa ' na GENTAMYCINE.
 
View attachment 612440 laki 6 pia inatumia gas ........................ see me inbox

Hebu jiheshimu basi tafadhali sawa? GENTAMYCINE nina muda wa utani na umakini na hapa nipo katika umakini wangu tena uliotukuka kabisa hivyo usitafute makubwa nami baadae ukaanza kunilamu. Principle yangu humu haijabadilika ambapo ni ile ile tu kwamba Wewe ukijamba tu Mimi nakunya kabisa.
 
Amguse aone..... Amulize Nape yaliyomkuta nini.... Ukitaka kuujua ukali wa mwanamume, mguse mkewe!!!

ZIRO ALISIMIKWA HAPO ALIPO KWA "JEURI" YA HUYO BASHITE KUWANYANYASA AKINA WEMA SEPETU NA MANJI...ILIKUWA UKIAMBIWA UKARIPOTI SENTIRO ZIRO ANAACHA KAZI ZOTE ZA MKOA KUMRIDHISHA"MAMA YETU"...NA SASA KAULA .
 
Makonda amefungiwa huu mtambo mkimgusa tu unaenda na maji.....Theater High Altitude Area Defense [THAAD].....

thaaad.jpg
 
Back
Top Bottom