Huu Mkasa umenishtua na kunistaajabisha. Sikuwahi dhani inaweza tokea hivi

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Kuna sehemu toka jumatatu kuna kampeni ya uchangiaji damu. Huwa kunakuwa na mashamsham yake,nderemo ,hoi hoi na vifijo kem kem.

Basi nikawa nmepark gari yangu pembeni nataka kufanya huduma ya muamala wa simu.ndo kuona zogo jamaa pale wanapochangia damu kashika kifuko cha damu anasema atamwaga.

Nlishtuka na kutaka kujua kulikoni....maana alisikika akisema "ntamwaga damu" nikajua anamaanisha atampasua au mchana mtu hadi damu imwagike .maskini kumbe kaka wa watu hakuwa na nia hiyo mbovu.ndo kusimulia.

Anasema toka alivyopiga msosi jana usiku mahindi ya kuchoma vipande viwili na mihogo akashushia na maji ili angalau mfumo wa choo usije ziba basi hajatia kitu ndani mpaka mida hiyo..

Akiwa ametoka kucheck mitkasi ambayo haikwenda safi akaona ajongee mitaa flani kucheck washkaji kama wanaweza mwonesha siku.

Ndo akasikia kuwa pale ukichangia damu unapewa biscuit na black current. Akili ikacheza kuwa hapo angalau ataiona siku.so akaenda pima wakamwambia anaweza changia nusu lita.

Wamemtoa damu umefika wakati wa kumpatia kifuta jasho wanasema juice na biscuit vimeisha.wakati alimwona mshkaji anampa demu chupa nne za juice na demu hata hajachangia akapewa na vibox vya biscuit.

Yeye kachangia wanamletea longo longo eti aende kwa amani tu ... Jamaa aliamka akakinyofoa kile kifuko cha damu akashika kwa hasira kuwa sasa anamwaga damu.na pale patachimbika kinyama kama hawatompa vitu vilivyotamkwa.

Hapo mzee mmoja ilibidi aaingilie kati kwa kumshawishi jamaa ajiwe na huruma.akampa tsh 5000. Jamaa akakubali kuweka kifuko mezani na kusema kama kuna mtu anataka damu nyingine anaweza toa apewe tu pesa.

Akadai yeye hata wakitka kutoa damu yote yupo tayari la msingi wampe pesa.akasisitiza hata haitumii sana hiyo damu so wanaweza tu inyonya yote la msingi apate pesa ya msosi.

Nikastaajabu sana kwa maisha haya sijui kama watu watafika.
 
Kuna sehemu toka jumatatu kuna kampeni ya uchangiaji damu. Huwa kunakuwa na mashamsham yake,nderemo ,hoi hoi na vifijo kem kem.

Basi nikawa nmepark gari yangu pembeni nataka kufanya huduma ya muamala wa simu.ndo kuona zogo jamaa pale wanapochangia damu kashika kifuko cha damu anasema atamwaga.

Nlishtuka na kutaka kujua kulikoni....maana alisikika akisema "ntamwaga damu" nikajua anamaanisha atampasua au mchana mtu hadi damu imwagike .maskini kumbe kaka wa watu hakuwa na nia hiyo mbovu.ndo kusimulia.

Anasema toka alivyopiga msosi jana usiku mahindi ya kuchoma vipande viwili na mihogo akashushia na maji ili angalau mfumo wa choo usije ziba basi hajatia kitu ndani mpaka mida hiyo..

Akiwa ametoka kucheck mitkasi ambayo haikwenda safi akaona ajongee mitaa flani kucheck washkaji kama wanaweza mwonesha siku.

Ndo akasikia kuwa pale ukichangia damu unapewa biscuit na black current. Akili ikacheza kuwa hapo angalau ataiona siku.so akaenda pima wakamwambia anaweza changia nusu lita.

Wamemtoa damu umefika wakati wa kumpatia kifuta jasho wanasema juice na biscuit vimeisha.wakati alimwona mshkaji anampa demu chupa nne za juice na demu hata hajachangia akapewa na vibox vya biscuit.

Yeye kachangia wanamletea longo longo eti aende kwa amani tu ... Jamaa aliamka akakinyofoa kile kifuko cha damu akashika kwa hasira kuwa sasa anamwaga damu.na pale patachimbika kinyama kama hawatompa vitu vilivyotamkwa.

Hapo mzee mmoja ilibidi aaingilie kati kwa kumshawishi jamaa ajiwe na huruma.akampa tsh 5000. Jamaa akakubali kuweka kifuko mezani na kusema kama kuna mtu anataka damu nyingine anaweza toa apewe tu pesa.

Akadai yeye hata wakitka kutoa damu yote yupo tayari la msingi wampe pesa.akadai hata haitumii sana hiyo damu so wanaweza tu inyonya yote.

Nikastaajabu sana kwa maisha haya sijui kama watu watafika.
Hii ni fictional event. Ume exaggerate sana. Na NDIO sifa moja ya fictional event.
 
Back
Top Bottom