Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Kuna mjadala unaendelea space pale twitter aisee kama haya maazimio ya kususia bidhaa na huduma yatafanikiwa hakika itakuwa hatari kwa uchumi.

Ushauri, Serikali wakutane na wapinzani haraka maana hata mishahara ya mapolisi inaweza kukosa huko mbeleni.

Ni ushauri tu mnaweza kuufanyia kazi au kuupuza ila kama hatua hizi zitafanikiwa hata kwa 25% makusanyo yataporomoka sana.

View attachment 1877729
CHADEMA imefilisika kweli kimawazo. Muanze kwa kususia kula na kwenda hospitalini. Kuacha kwenda shule na kunywa maji pia itapendeza
 
Mkuu are you serious kususia bidhaa hakuwezi kuleta athari za kiuchumi?
Sijasema hivyo, usinilishe maneno. Nimesema wanachama wa Chadema kususia bidhaa hakutaleta athari za kiuchumi.

Kwa Tanzania ina wanachama wa Chadema wangapi wenye purchasing power ya kutosha kuathiri uchumi wakisusia bidhaa?
 
Huo mgomo ni wa KIPUMBAVU kabisa na wala hauwezi kuleta impact kwa uchumi hata kwa 0.00000001%.

Kwa mfano kugomea mitandao ya simu unaanzanje? Hata kwenye hiyo Space wanatumia simu. Una mzazi wako inabidi umpelekee fedha ya chakula au dawa, utafikisha vipi ukigoma ?

Vijana wengi hayo makampuni ya huduma ndiyo ajira zao indirectly, wanasoma halafu wanakosa kipato.

Hiyo mijadala yao ni ya KIPUMBAVU
Kususia huduma maana yake Nini?

Kama Vodacom (mfano) walishiriki kuhujumu Haki za kirai kwa kushirikiana na hao manyan'gau Basi tupa laini chooni (sajili?) register mtandao mwengine,simple tu yaani.

Mtandao wa simu kupoteza watu 100 kwao ni hasara kubwa Sana.
 
Sijasema hivyo, usinilishe maneno. Nimesema wanachama wa Chadema kususia bidhaa hakutaleta athari za kiuchumi.

Kwa Tanzania ina wanachama wa Chadema wangapi wenye purchasing power ya kutosha kuathiri uchumi wakisusia bidhaa?
Kama waliompigia kura Lowassa akiwa mgombea wa CHADEMA walifika zaidi ya 6 milioni na maguful 8 milioni huoni hiyo idadi ni kubwa?

Hapo kuna wengine hawakupiga kura na wengine wangefata mkumbo wa ndugu zao, waume zao au marafiki zao kususia.
 
Kususia huduma maana yake Nini?

Kama Vodacom (mfano) walishiriki kuhujumu Haki za kirai kwa kushirikiana na hao manyan'gau Basi tupa laini chooni (sajili?) register mtandao mwengine,simple tu yaani.

Mtandao wa simu kupoteza watu 100 kwao ni hasara kubwa Sana.
Katupe line yako wala VODACOM hawakutegemei wewe nyang'au. Wataendelea na corporate customers wao ambao wanawapa 80% the business
 
Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato.

Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki.

Wanasema kuwa, jamii ya Watanzania wakipunguza matumizi ya bidhaa na huduma kama vile unywaji wa Bia, kupunguza matumizi ya sukari, maji ya kunywa, kupunguza miamala isiyo ya lazima na vyakula katika hoteli zilizosajiliwa.

Wanaamini kuwa kupunguza huko matumizi ya huduma na bidhaa itasababisha serikali kukosa kiasi kikubwa cha mapato.

Na kukosa huko mapato itasababisha serikali ishindwe kujiendesha kwa sababu mapato yamepungua. Na bila shaka, kutafuta namna ya kukaa na wadau na kuzungumza nao ili kuweza kutatua yaliyomo.

Wanaamini kuwa, njia hii ya kususia bidhaa na huduma 'Boycotting' itakuwa na ufanisi kwa sababu hakuna polisi watakaokuja kuwalazimisha watu watumie.

Wanaona kuwa njia hii ni ya amani na hivyo itawalazimisha serikali kurudi katika Misingi ya Utawala bora na kuleta uchocheo wa Katiba mpya.

Je, CHADEMA watafanikiwa kwa njia hii?
serikali ina njia nyingi za kutafuta hela, huwezi kuikomoa serikali, utakachofanya utazidi kumuumiza mtu wa chini, we unajuaje, je kama wana print note, kwani we noti zinapotokea na process yake unaifahamu. we kausha tu, serikali haikomoleki, ukijaribu kufanya hivo, bibi yako kijijini ndo atalia na umasikini
 
Ikitokea hivyo hapo ndiyo safi maana itapiga pentagoni kiuchumi na italazimisha watawala watie akili

Maana wakishakosa hela za kuwalipa mishahara hao wabeba bunduki ndiyo akili zitawaingia vizuri zaidi
CHADEMA waanze kwanza kwa kurejesha mishahara na marupurupu yote na ruzuku zote walizowahi kupewa na serikali dhalimu ya CCM.

Vinginevyo huu ni upumbavu kwq watu wazima
 
Kama Mbowe akili imestaafu muacheni huru, mnamuogopa nini sasa?
CCM ni hovyo ila ninyi Chadema ni hovyo kabisa! Mmekuwa kama wendawazimu! Yeyote atakayetoa mawazo huru ambayo yakiwa tofauti na yenu kwenu ni adui ni CCM na mnambambikizia uchama u-CCM. Huu ndiyo uhuru wa Demokrasia mnaoupigania? Hamshauriki! Tena hamfai hata kupewa nchi ikiwa ninyi na wafuasi wenu mna akili za namna hii! Kwa ufupi ninyi ni Madikteta.

Mwenye akili anadhibitiwa kwa kufungwa ila wewe usie na akili wanakuacha huru maana hauna madhara yoyote.
Yupi ambaye asiye na akili? Yule ambaye atakachoambiwa na Mbowe atachanganya na akili yake kwa kuyameng'enya zaidi au yule ambaye kila atakachoambiwa na Mbowe anafuata tu?

Mimi sipangiwi ila nashaurika, natafakari na nachukua maamuzi na ndiyo maana sina chama. Chama changu ni mafundisho ya Mungu tu.
 
Chadema haishindwi kupambana na CCM. CCM haipambani yenyewe inatumia jeshi,mahakama, na tume ya uchaguzi
Ikiwa unapigana na wa namna hii ni vyema kutumia akili zaidi na mipango madhubuti kuliko mihemuko na ununda usio na maana. Tena si mipango ya miaka 5 bali ulenge miaka kuanzia 15 mbele huko!

Wakati mwengine ni kuwafanya kwa macho ya karibu uonekane umefeli ila ya mbali mnoo umefaulu.
 
Back
Top Bottom