Huu mgao wa umeme isiwe ni mbinu ya kutafuta kiki kwa wananchi

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,508
2,000
Serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli ni aina ya serikali inayoendeshwa kwa matukio na kiki

Matatizo mengi yanaibuliwa na kutatuliwa na rais ili apate kiki na kuonekana anaipenda sana nchi na kuwapenda wananchi wake ili azidi kuwaaminisha kachaguliwa kwa lengo la kuwahudumia wananchi

Serikali ya Magufuli ni kama familia ya kambare ,Baba masharubu,mama masharubu na watoto masharubu kila mmoja anataka aonekane mkubwa na mchapa kazi mbele ya Watz

Tatizo la umeme lilianza kulalamikiwa Mtwara na Lindi ambako kuna vyanzo vikuu na madhubuti vya umeme ambavyo ni Gesi,cha ajabu akaenda waziri wa nishati akaonesha masharubu yake ,mikwara kibao na kusema tatizo la umeme liishe,ile anageuza kisogo tu tatizo limeendelea kama kawa

Now tatizo limekua la nchi nzima umeme ni shida ,sasa hii isije kuwa mbinu ya Magufuli na serikali yake ya kutafuta kiki,mwisho ataibuka na kusema tatizo la umeme liishe Mara moja ili wananchi wamsifu kwa kutatua matatizo

Mlikuja na porojo kibao eti mgao wa umeme utakua historia baada ya kukamilika mitambo ya umeme wa gesi ya kinyerezi ,hiyo mitambo imekamilika sasa huu mgao unatoka wapi

Kwa style hii Magufuli usitegemee Sera yako ya Tz ya viwanda itatimia labda viwanda ya kupika gongo,vyerehani vinne na vile vya kuchakata bangi ambavyo havihitaji nishati ya umeme

Na hiyo treni ya umeme inayotaka kuletwa itaendeshwa kwa umeme gani ?

Aibu sana nchi ina zaidi ya miaka 50 chini ya serikali ya CCM lakini bado matatizo kila kukicha aibu sana

N.B Ni wajinga pekee wanaoamini Magufuli na CCM yake italeta maendeleo ya kweli Tanzania
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,759
2,000
bashite kajaza mapicha yake kwenye maduka ya watu pale mlimani city mall bila ridhaa yao
unategemea kiongozi anayewaamini watu dizaini ya bashite ni wa kumuamini!!!
 

Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,554
2,000
Mkuu hakuna Kiki ngoma ngumu Mgao unapigwa hadi Magogoni ndo ujue kuwa Tanesco wamevurugwa..,
 

maalon

JF-Expert Member
Feb 14, 2015
475
500
Inawezekana ikawa hivyo au siku mitambo ya umeme ikiwa sawa jamaa akipelekewa taarifa anaweza kufanya ziara ya kushitukiza na kaagiza kuwa kuanzia kesho asisikie mgao wa umeme na kweli umeme kesho yake ikawa hakuna mgao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom