Huu Mchezo Ni Wa Kawaida Hapa Nchini

Hiyo nchi imekuwa kama jalala/ji-dampo, maana naona kila kilicho kibaya kinapatikana!!!
 
Halafu bongo kinachonishangaza ni wakati unapouliza jambo,basi watarushiana mpira hadi utachoka,mara mimi sihusiki muulize fulani,ukimuuliza naye,anakuambia,sisi tunahusika na hili,hilo ungewauliza fulani,hao fulani nao ukiwauliza,watakuambia,nasi hatuhisiki na hilo,kwa hiyo waulize fulani.Itafika muda utajikuta unaambiwa urudi kule ulikotoka,na jibu hujapewa.Hakuna uajibikaji hapa,foko jembe nyie.
 
Tanzania nchi yangu,
Kweli nchi yangu,
Haki ya Mungu,
Ninaapa Tanzania nitakulinda.

Huu ubeti huwa unanikumbusha mbali sana nikiwa nasoma shule ya upili.

Kuitwa Mtanzania si kuwa Tanzania tu ukivuta hewa ya Tanzania. Ni pamoja na kumiliki na kufaidika na Rasilimali zilizopo TZ. Kama haunufaiki nazo ni sawa na kwamba wewe ni mkimbizi na Wa TZ ni wale wanaofaidi.

Tusilete masihara hapa, Watanzania wanufaike na rasilimali zao ndio watajiona wazawa kweli sio kuwahamasisha kubeba mibendera ili wajione watazania, lazima wajivunie na kunufaika na maliasili zinazopatikana nchi mwao, ndipo watasema, TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
 
Back
Top Bottom