Huu ndio mkataba wa Karl Peters na Chifu Mangungo ulitufanya tunawekwa chini ya Mjerumani

Kwenye Bible kuna mtu anaitwa Jezebel. Alikuwa mke wa mfalme Ahab. Alisababisha matatizo makubwa kwenye utawala wa Ahab. Ni story ndefu kidogo. Baadae alikufa. Cha ajabu baada ya miaka mingi. Kanisa linakemewa ktk kitabu cha Ufunuo kwamba yafaa wamkatae Yezebeli maana bado yupo kwa namna nyingine. Nataka kusema nini. Akina Carl Peter, Ramazan na akina Mangungo huweza kurudi ktk roho ileile ila miili tofauti.
 
Ni dhahiri kwamba Mangungo hakujua kusoma wala kuandika Kijerumani. Inaonekana pia kupitia kwenye maelezo ya mkataba kwamba mkalimani mwenyewe hakujua kusoma wala kuandika kabisa. Kwa gharama yoyote ile, ikumbukwe kwamba Ramazan alikuwa ameajiriwa na Karl Peters na alitakiwa kufuata maelekezo yake.
Karl Peters aliwasili Ujerumani Februari 7, 1885 akiwa na lundo la mikataba. Peters alitumia mikataba hiyo kupata kibali maalum - Schutzbrief – ili kutambuliwa kwa madai yake Februari 27, 1885.
Kwa maneno mengine, Otto von Bismarck, Chancellor mkuu wa Ujerumani wakati huo, alikuwa amebadili sera yake ya awali dhidi ya Ujerumani katika kutafuta makoloni.

BRIGHT KAROLI
brightkaroli424@gmail.comView attachment 969193View attachment 969194
Mangungo naye alikuwa kilaza, hakushanga Karl Peters amekuja lini na mkalimani wake sijui Mluguru, Mkaguru nk. amejua Kijerumani lini!
 
Mkataba haukuwa kwa Faida ya Waafrika wala Waafrika walikuwa hawana Say Mkataba huo ulikuwa ni kwa ajili ya wao Waliosign mkataba kama kinga ya wengine wataokuja baada yao kuonyesha kwamba ni mali yao...

Kwa Mu-afrika hata angekataa mwisho wa siku wangechukua kwa nguvu...; Scramble and Partition of Africa, Mu-afrika alikuwa hana Say... (Just a Pawn to be Sacrificed)

Tofauti na sasa wachache wanaamua kugawa mali-asili ya vizazi vijavyo kwa faida ya muda mchache
 
Mkataba haukuwa kwa Faida ya Waafrika wala Waafrika walikuwa hawana Say Mkataba huo ulikuwa ni kwa ajili ya wao Waliosign mkataba kama kinga ya wengine wataokuja baada yao kuonyesha kwamba ni mali yao...

Kwa Mu-afrika hata angekataa mwisho wa siku wangechukua kwa nguvu...; Scramble and Partition of Africa, Mu-afrika alikuwa hana Say... (Just a Pawn to be Sacrificed)
Hii mikataba kama kesi za ardhi tu za kipindi hiki
 
Msovero Usagara Novemba 29, 1884.
Kwa kweli. huu mkataba haukuwaacha salama Wasagara hadi leo. Uchumi wao ni duni sana, ni kama wametengwa na dunia vile. Pamoja na udongo wenye rutuba na mito mingi Kilosa ya Wasagara bado imebaki nyuma na wao wameamua kuwa kama Waswahili halisi. Nashukuru Mungu Wasagara wamenipa ekari 40 ktk kijiji kilichokuwa na Ikulu ya Chief wao (Msovero a.k.a Msowero wanavyoitamka leo). Huku Usagara tuna hadi kijiji cha Ulaya.
 
Back
Top Bottom