Hutakuja kusahau tukio gani ulilofanya kukomboa pesa yako kwa mdaiwa msumbufu/mdhulumaji

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Nakumbuka nikiw chuoni kuna jamaa alikuja kwangu baada ya kuzunguka kwa wengi akiwa na shida ya laki 3 , nilimuonea sana huruma ikabidi nimpe, tukakubaliana baada ya miezi miwili anilipe.

Miezi miwili imekatika nkavuta pumzi, baada wa wiki nikamfata geto kwake tulikutana njiani ila akawa anazuga kuongea na simu anawahi sehem flani nikasema ok its fine, kesho yake namkuta geto akapanga maneno atanipa baada ya wiki nikavumilia.

Baada ya hio wiki nmeenda kwake nagonga mlango kimya, najua aliwa ndani ila nkaona isiwe kesi tutakutana tu.

Baada ya siku 2 nikamuona kwa mbali, nae nahisi aliniona basi akakata kona flani ivi nikaenda kona hio simuoni jamaa.

Ikabidi niende kumsubiri geto kwake, anafika tu nae kanikuta, akaanza zile za laki 3 kitu gani, mara kafura hasira, n.k kapaniki flani ivi akaingia ndani akafunga mlango na funguo.

Kesho yake nakumbuka nlienda geto kwake nikamlia timing, anapotoka tu nikaingia ghetto lake, nilibeba laptop yake na simu smartphone kibabe, akaanza kunitishia sijui ataripoti polisi mi nikamwambia nishakukatia rb we nyau kwa utapeli.

Nikapanda bodaboda nikala nduki.

Kesho yake nafika chuo namkuta jamaa getini, akanipa laki 3 yangu cash, tukarudi geto nikampa vyake ikawa imeisha ivo.

Jamaa bado ni rafiki yangu tukikumbushana huo mtiti tunacheka, ila siwezi kuja kumkopesha na sidhani kama na yeye ana wazo la kuja nimkope
 
Yaaani huu uzi umekuja juu kwenge notification panel nikiwa namuandikia msg mdeni wangu....

Nimeamini kumkopesha rafiki ni kununua uadui,
Mimi huyu hata anilipe sitaki tena urafiki nae,
Kanivuruga sanaaaaa, nikikumbuka alivyoomba na alivyo sasa hata siamini....
 
mkuu we nenda kwake somba vitu kama huna ujasiri huo uza deni kwa mtu mtata hapo mtaani umwambie unaemdai kwamba hio pesa ilikuwa yako na ya huyo mtata ila wewe umechoka kidai sasa ni zamu ya mtata
 
Kipindi hicho nimetoka veta nikapata ya kuendesha watoto wa shule kwa mshahara laki moja per month, boss akawa hanilipi ananipa hela ya nauli tu baada ya miezi sita dada aliyenilipia veta akaumwa na anatakiwa kufanyiwa oparation bugando, mi ndo wakuhudumia, kumwambia boss ananitisha kuwa hana hata mia niende polisi, mara akachukua dereva mwingine, kilichofata nilienda kwake saa moja muda anatoka job akanikuta sebuleni nimekaa na familia yake, Dah shida uleta maarifa nilipiga mayowe ndani kama mweu kelele nyingi majirani wakajaa, kuona vile akaona aibu mabosi wenzie wako nje nikawasimulia kila kitu wakamuona hafai, jamaa alienda bank muda huo akaja na laki sita yangu kesho yake nikamlipia sister hela hospitali .
 
😀😀Mmebaki marafiki,
Wengi hubaki maadui. Sasa anakwambia kipi kilimfanya asitake kukurudishia?
 
yani usipojiamini hii dunia utadhulumiwa sana, big up sana mzee, nmeipenda hii kweli ilikuwa ya kibabe
 
😀😀Mmebaki marafiki,
Wengi hubaki maadui. Sasa anakwambia kipi kilimfanya asitake kukurudishia?
mkuu marafiki huwa wanagombana mbona 😀😀, jamaa naona alisahau kwamba namdai kama vile wengi tulivyo wagumu kulipa madeni tunapopata pesa, nakumbuka urafiki uliisha kwa siku kama mbili ivi ila akaja kuniomba msamaha na kukiri kosa lake, basi ndo yakaisha.

ila sio besti, ni rafiki wa kawaida tu wa kukumbushana enzi za chuo, utani wa timu, n.k
 
mkuu marafiki huwa wanagombana mbona 😀😀, jamaa naona alisahau kwamba namdai kama vile wengi tulivyo wagumu kulipa madeni tunapopata pesa, nakumbuka urafiki uliisha kwa siku kama mbili ivi ila akaja kuniomba msamaha yaishe
Me kwa kweli kudai huwa siwezi na huto ona nakukumbushia deni. Ila ukijisahaulisha kunilipa huwa sisahau na hutokuja tena kuona nakukopesha pesa yangu. Labda niamue tu kukupa.
 
Hii mbinu mkuu ntaitumia kwa mdeni wangu mshahara ukitoka haiwezekani mtu awe anazurula na laki 5 zangu usawa huu.
Kipindi hicho nimetoka veta nikapata ya kuendesha watoto wa shule kwa mshahara laki moja per month, boss akawa hanilipi ananipa hela ya nauli tu baada ya miezi sita dada aliyenilipia veta akaumwa na anatakiwa kufanyiwa oparation bugando, mi ndo wakuhudumia, kumwambia boss ananitisha kuwa hana hata mia niende polisi, mara akachukua dereva mwingine, kilichofata nilienda kwake saa moja muda anatoka job akanikuta sebuleni nimekaa na familia yake, Dah shida uleta maarifa nilipiga mayowe ndani kama mweu kelele nyingi majirani wakajaa, kuona vile akaona aibu mabosi wenzie wako nje nikawasimulia kila kitu wakamuona hafai, jamaa alienda bank muda huo akaja na laki sita yangu kesho yake nikamlipia sister hela hospitali .
 
Kipindi hicho nimetoka veta nikapata ya kuendesha watoto wa shule kwa mshahara laki moja per month, boss akawa hanilipi ananipa hela ya nauli tu baada ya miezi sita dada aliyenilipia veta akaumwa na anatakiwa kufanyiwa oparation bugando, mi ndo wakuhudumia, kumwambia boss ananitisha kuwa hana hata mia niende polisi, mara akachukua dereva mwingine, kilichofata nilienda kwake saa moja muda anatoka job akanikuta sebuleni nimekaa na familia yake, Dah shida uleta maarifa nilipiga mayowe ndani kama mweu kelele nyingi majirani wakajaa, kuona vile akaona aibu mabosi wenzie wako nje nikawasimulia kila kitu wakamuona hafai, jamaa alienda bank muda huo akaja na laki sita yangu kesho yake nikamlipia sister hela hospitali .
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Huu uzi umekuja kipindi hiki nina mawazo tani 100.Kweli nimeamini kukopeshana ni kununua uadui tu...Kuna tajiri mmoja hataki kunilipa ela yangu tangu February mpk leo na nina uhakika ela anayo mana napata taarifa jinsi hasivyokwama kutoka kwa wadau wa ofisi yake.

Hiyo pesa nimefanya mbinu zote ila naona jamaa kaamua kunizima kiaina.Roho inauma mtu kukomalia 3M usawa huu.

Mpaka sasa sina cha kumfanya mana hatukuandikishana popote ila baadhi ya wafanyakaz wake wanajua namdai mana kazi zilizozaa deni nilifanya mimi peke yangu

Huyu mwamba nina miaka kibao nae tunafanya kazi pamoja na uwezo wake naujua hivyo haikuwa ngumu kumuamini kiwango hicho...Kukosekana kwa hiyo pesa kumeleta balaa kubwa ukizingatia sina kibarua chochote sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nenda kaongee naye upya ukiwa umeiweka simu mfuko wa shati iwe inarekodi, we mtege tu na maswali ionekane kweli unamdai milioni 3. pia itakua poa zaidi simu ikirekodi video.

ukimaliza hapo nenda kwa mwanasheria, watakupa barua umpelekee akubali mashtaka myamalize mapema au muende polisi alafu mahakamani.

nakwambia ukimpelekea hio barua akiona tu nembo ya jamhuri ya muungano lazima utakuwa umemtikisa,

fanya ivo muhimu uwe na ushahidi wa video, hakuna mtu anaependa kwenda polisi au mahakamani. mkomalie haswaaa
 
Back
Top Bottom