sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,029
Nakumbuka nikiw chuoni kuna jamaa alikuja kwangu baada ya kuzunguka kwa wengi akiwa na shida ya laki 3 , nilimuonea sana huruma ikabidi nimpe, tukakubaliana baada ya miezi miwili anilipe.
Miezi miwili imekatika nkavuta pumzi, baada wa wiki nikamfata geto kwake tulikutana njiani ila akawa anazuga kuongea na simu anawahi sehem flani nikasema ok its fine, kesho yake namkuta geto akapanga maneno atanipa baada ya wiki nikavumilia.
Baada ya hio wiki nmeenda kwake nagonga mlango kimya, najua aliwa ndani ila nkaona isiwe kesi tutakutana tu.
Baada ya siku 2 nikamuona kwa mbali, nae nahisi aliniona basi akakata kona flani ivi nikaenda kona hio simuoni jamaa.
Ikabidi niende kumsubiri geto kwake, anafika tu nae kanikuta, akaanza zile za laki 3 kitu gani, mara kafura hasira, n.k kapaniki flani ivi akaingia ndani akafunga mlango na funguo.
Kesho yake nakumbuka nlienda geto kwake nikamlia timing, anapotoka tu nikaingia ghetto lake, nilibeba laptop yake na simu smartphone kibabe, akaanza kunitishia sijui ataripoti polisi mi nikamwambia nishakukatia rb we nyau kwa utapeli.
Nikapanda bodaboda nikala nduki.
Kesho yake nafika chuo namkuta jamaa getini, akanipa laki 3 yangu cash, tukarudi geto nikampa vyake ikawa imeisha ivo.
Jamaa bado ni rafiki yangu tukikumbushana huo mtiti tunacheka, ila siwezi kuja kumkopesha na sidhani kama na yeye ana wazo la kuja nimkope