Hussen Mwinyi: Watakaokaidi wito wa Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kukomeshwa kwenye ajira

jotozs

Member
Jul 17, 2017
12
10
Screenshot from 2017-07-18 14-03-08.png

Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi amesema vijana ambao watakaidi wito wa kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria, watakuwa wamekaidi amri halali na majina yao yatapelekwa mamlaka za ajira kwa ajili ya hatua dhidi yao.

Kauli hiyo ameitoa wakati JKT ikiendelea na mchakato wa kufufua kambi tano nchini ili kufanikisha uwezeshaji wa vijana wanaomaliza elimu ya juu ya sekondari kujiunga na jeshi hilo kwa kujitolea na kwa mujibu wa sheria.

Awali, ilikuwa lazima kwa wahitimu wa elimu ya juu ya sekondari na vyuo kujiunga na mafunzo ya mwaka mmoja JKT kabla ya kuendelea na masomo au kuanza ajira, na baadaye muda ukapunguzwa.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, Waziri Mwinyi amesema uchaguzi wa vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo unafanyika bila kutumia kigezo chochote zaidi ya kuwa mhitimu wa kidato cha sita.

“Yeyote ambaye jina lake linakuwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuhudhuria mafunzo, ni lazima akahudhurie na asipoenda anakuwa amekiuka amri halali. Majina ya walioteuliwa, yalionyesha waliohudhuria na waliokaidi tunayapeleka katika mamlaka za ajira,” amesema Dk Mwinyi.

Hivi karibuni wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya JKT kwa vijana wa kujitolea katika kambi ya 838 KJ Maramba wilayani Mkinga, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema jeshi hilo linakusudia kufufua kambi tano.

Amezitaja kambi hizo kuwa ni 826 Mpwapwa mkoani Dodoma, 845 Itaka (Songwe), 846 na 847 zilizoko Rukwa na 839 Makuyuni (Arusha) ambayo imeshaanza kupokea vijana ambao wanaendelea na mafunzo.

Chanzo: Mwananchi
 
Halafu mujibu gani unachagua. Kwa nini wasiende wote . Yaani wengine wapate muda wa kuapply vyuo wengine wakose. Halafu kuna wazazi wengine wameshindwa kuwapeleka sababu hawana hela, yaani unampa mzazi wiki moja tu awe amepata nauli pamoja na mahitaji mengine. Kuna wengine wamepangiwa kigoma ili hali wanishi Mbeya. Unajua nauli ya kwenda na kurudi pamoja na malazi ni shilingi ngapi. Hapo bado mashuka, mashuka, raba etc.
 
Inabidi serikali iliangalie hili,maana familia nyingine kipato duni,hivyo unavyolazimisha kumpa mzazi majukumu mengine yasiyo na ulazima wala tija sio sawa.
 
Yaani n

Yaani alieshiba hamjui mwenye njaa, kuna wazazi wengine hata hiyoelfu 70 ya ada kwa mwaka inakuwa shida kuipata hadi mwanafunzi anachelewa shule zaidi ya mwezi. Watu wanapofanya maamuzi wanngalie hali halisi za Watanzania. Kama JKT wameamua kufanya hayo mafunzo yake lazima kwa wote sio kuchangua baadhi ili kutenda haki. Pia wanafunzi wasafirishwe bure na kulipiwa kila kitu. Hii itakuwa fursa na haki sawa kwa wote.
 
Wengine wameitwa JKT wakati wako chuo tayari-na kwenye tangazo lao walifikiri hao walikosa chuo. Sasa ukimuadhibu huyo mtu utakuwa sawa?

Waziri huyu hivi yeye alikenda JKT? Kuna kastori kuwa zamu yake ilipofika yeye ndo alikwenda huko uturiki akawaachia wengine zigo hilo. Nikastori tu labda wajuvi watatufahamisha.
 
Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi amesema vijana ambao watakaidi wito wa kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria, watakuwa wamekaidi amri halali na majina yao yatapelekwa mamlaka za ajira kwa ajili ya hatua dhidi yao.

Kauli hiyo ameitoa wakati JKT ikiendelea na mchakato wa kufufua kambi tano nchini ili kufanikisha uwezeshaji wa vijana wanaomaliza elimu ya juu ya sekondari kujiunga na jeshi hilo kwa kujitolea na kwa mujibu wa sheria.

Awali, ilikuwa lazima kwa wahitimu wa elimu ya juu ya sekondari na vyuo kujiunga na mafunzo ya mwaka mmoja JKT kabla ya kuendelea na masomo au kuanza ajira, na baadaye muda ukapunguzwa.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, Waziri Mwinyi amesema uchaguzi wa vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo unafanyika bila kutumia kigezo chochote zaidi ya kuwa mhitimu wa kidato cha sita.

“Yeyote ambaye jina lake linakuwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuhudhuria mafunzo, ni lazima akahudhurie na asipoenda anakuwa amekiuka amri halali. Majina ya walioteuliwa, yalionyesha waliohudhuria na waliokaidi tunayapeleka katika mamlaka za ajira,” amesema Dk Mwinyi.

Hivi karibuni wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya JKT kwa vijana wa kujitolea katika kambi ya 838 KJ Maramba wilayani Mkinga, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema jeshi hilo linakusudia kufufua kambi tano.

Amezitaja kambi hizo kuwa ni 826 Mpwapwa mkoani Dodoma, 845 Itaka (Songwe), 846 na 847 zilizoko Rukwa na 839 Makuyuni (Arusha) ambayo imeshaanza kupokea vijana ambao wanaendelea na mafunzo.

Chanzo: Mwananchi

Ajira zenyewe ziko wapi?Hizo wanazopewa wa kanda ya ziwa tu au kuna nyingine?
 
Yaani n

Yaani alieshiba hamjui mwenye njaa, kuna wazazi wengine hata hiyoelfu 70 ya ada kwa mwaka inakuwa shida kuipata hadi mwanafunzi anachelewa shule zaidi ya mwezi. Watu wanapofanya maamuzi wanngalie hali halisi za Watanzania. Kama JKT wameamua kufanya hayo mafunzo yake lazima kwa wote sio kuchangua baadhi ili kutenda haki. Pia wanafunzi wasafirishwe bure na kulipiwa kila kitu. Hii itakuwa fursa na haki sawa kwa wote.
Yaani wameishupalia kama kodi-nauli na vitu kadha ujinunulie mwenyewe kama huna kakope. Haya bana ndo uzalendo huo.
 
Hawa jamaa bhana, wanapeleka wanafunzi JKT wakati hawajajiandaa. Mdogo wangu alichaguliwa Makutupora lakini hakwenda kwasababu muda wa kuanza chuo ulikuwa umefika, So na huyo atakuwa amekaidi?

hii ndiyo serikali ya CCM mnayoishereheka hapa kila kukicha.

unorganized state.
 
Yaani n

Yaani alieshiba hamjui mwenye njaa, kuna wazazi wengine hata hiyoelfu 70 ya ada kwa mwaka inakuwa shida kuipata hadi mwanafunzi anachelewa shule zaidi ya mwezi. Watu wanapofanya maamuzi wanngalie hali halisi za Watanzania. Kama JKT wameamua kufanya hayo mafunzo yake lazima kwa wote sio kuchangua baadhi ili kutenda haki. Pia wanafunzi wasafirishwe bure na kulipiwa kila kitu. Hii itakuwa fursa na haki sawa kwa wote.
Nakumbuka na Mimi ni miongoni mwa tuliopitia hayo mafunzo Miaka kazaa nyuma enzi za jk,tulipofika vikosini kila kitu tulipewa bure,tukapewa na posho kila mwezi ya kujikimu,kwa miezi yote mitatu tuliyokuwa kule,na nauli tulirudishiwa kikubwa ni kukusanya tiketi yako,kama ulikuja na ndege utalipwa nauli ya ndege,kama basi utalipwa na nauli ya basi,na kurudi pia hivyo hivyo nauli tulipewa.sasa sijui sasa hivi kaingia mdudu gani kiasi kwamba,hayo majukumu anapewa mzazi ilihali,si mzazi anayetaka mtoto wake aende jkt,Bali serikali imelazimisha hilo swala,hivyo basi isikwepe majukumu ya kuwagharamia hao vijana ikiwa wanaona kuna faida kwa taifa itaipata ikiwa watapita huko jkt,lakini wakiona hakuna faida waache kulazimisha watu,wajiongezee majukumu yasiyo na tija wala faida.
 
Wengine wameitwa JKT wakati wako chuo tayari-na kwenye tangazo lao walifikiri hao walikosa chuo. Sasa ukimuadhibu huyo mtu utakuwa sawa?

Waziri huyu hivi yeye alikenda JKT? Kuna kastori kuwa zamu yake ilipofika yeye ndo alikwenda huko uturiki akawaachia wengine zigo hilo. Nikastori tu labda wajuvi watatufahamisha.
wanatakiwa kwenda baada ya kumaliza masomo kwani huandika barua ya kuhairisha mafunzo na kuhaidi kwenda baada ya kumaliza chuo
 
Hawa jamaa bhana, wanapeleka wanafunzi JKT wakati hawajajiandaa. Mdogo wangu alichaguliwa Makutupora lakini hakwenda kwasababu muda wa kuanza chuo ulikuwa umefika, So na huyo atakuwa amekaidi?
Mie nilipangiwa Orjoro wakati huohuo napaswa niende chuo na boom nimepata, mie nikaenda chuoni
 
Back
Top Bottom