Hussein Ramadhan'Sharo Milionea' aibiwa nguo zote alizokuwa amevaa kabla ya ajali.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
SERIKALI wilayani Muheza imetoa muda wa saa 24 vinginevyo italazimika kutumia nguvu ya dola kuwasaka na kuwafikisha mahakamani wananchi wote wa Kijiji cha Songa Kibao Maguzoni waliohusika na wizi
wa mali za Msanii Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea', aliyezikwa jana Lusanga Muheza.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu, wakati akitoa tamko la Serikali kutokana na aibu hiyo iliyojitokeza wakati wa tukio la ajali ambapo msanii huyo aliibiwa mali zote ikiwa ni pamoja na nguo alizovaa.

Alisema Serikali itatumia nguvu kuwasaka watu hao kwa sababu inajulikana waliohusika na wizi huo na kutahadharisha kuwa wajisalimishe wenyewe kabla hatua ya kuvamia kijiji hicho
na kutumia nguvu ya dola haijafanyika.

Mgalu alitoa saa 24 kuhakikisha vitu vyote vilivyoibwa vinasalimishwa na baada ya hapo nguvu itatumika kuwasaka
watu wote na watakamatwa na kufikishwa Mahakamani.

Mwandishi,
Benedict Kaguo
Kutoka gazeti la Majira

ANGALIZO:
Watanzania kama tumefikia kiwango hiki cha kutokuwa na hekima na huruma basi tunakuwa kama taifa mfu. Umaskini siyo sababu ambayo inatufanya tufikie kiwango hiki cha fikra na matendo yasiyo ya kibinadamu mwenye akili timamu.
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,960
2,000
Hili ni jambo la kawaida sana ajali inapotokea.Nakumbuka nilikuwa natoka Dar - Arusha tyre ya mbele ya gari tulilokuwa tukisafiria lilipancha maeneo ya Maili kumi [Korogwe] gari likaacha njia likaingia maporini bahati nzuri halikupinduka ndani ya dakika 5 tulikuwa tumezungukwa na vibaka kama hatukuwa na silaha tungekoma tukapiga risasi moja hewani wakatawanyika.Sasa pata picha Sharo alikuwa mwenyewe,keshakufa ana vitu vizuri nguo,fedha,simu na nk.
 

prince pepe

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
215
0
Hivi kamera ya mwandishi mwangosi ilishapatikana?

Hope vitu vya marehemu sharo vitapatikana pia
 

mtotowamjini

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
4,530
0
mpaka aibiwe mtu maarufu ndio serikali inafungua mdomo....mbona wananchi wanaibiwa kila siku kwenye ajali..mbona hao vibaka hatusikii wamekamatwa?
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Hata kama ni umaskini ila sio katika hali hiyo pya kumvua nguo mtu aliyepata ajali na kumuacha utupu
 

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,059
2,000
ukiwaona kama watu mioni hawana utu. Tabia hii iko vijijini vyote vilivyopo pembeni mwa barabara kuu. Serekali ikomeshe tabia hii, sijui wao ndio ndio wanaombea sana ajali zitokee ili waibe chupi za watu??.
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
kuna sehem za vijiji hata upite saa nane za usiku unawakuta watu wanatembea barabarani na wengine wamekaa vijiweni wanaongea sasa sijui hao watu wanasubiri ajali au wanasubiri nini usiku huo wa manane
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
13,328
2,000
ukiwaona kama watu mioni hawana utu. Tabia hii iko vijijini vyote vilivyopo pembeni mwa barabara kuu. Serekali ikomeshe tabia hii, sijui wao ndio ndio wanaombea sana ajali zitokee ili waibe chupi za watu??.

Ndio sababu pale Wami pembeni ya mto kuna kituo cha polisi. Kiliwekwa ili kuzuia aibu za namna hii mara ajali zinapotokea
 

Kifarutz

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
1,740
1,225
Umasikini unapimwa kwa vitu vingi vikiwepo vijimambo kama hivi. Poor Sharobaro sijui kama ile nguo tunayovuaaga ya mwisho ilibaki..!
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Umasikini unapimwa kwa vitu vingi vikiwepo vijimambo kama hivi. Poor Sharobaro sijui kama ile nguo tunayovuaaga ya mwisho ilibaki..![/QUOTE


ni balaa mkuu unaweza shangaa watu wanaenda kutafuta nguo ya kumsitiri marehem baada ya wajanja kuondoka na kila kiitu
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Inasikitisha sana. Binadamu wanakosa hata tone la maadili ya kibinadamu

Watu siku hizi wanakuambia bora ukutane na simba anaweza kukuogopa akakimbia akakuachia uhai wako kuliko ukutane na binadam ambaye ana haja na wewe kuna mawili atakuua au ataondoka na kila kitu na kilema akuachie
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Hili ni jambo la kawaida sana ajali inapotokea.Nakumbuka nilikuwa natoka Dar - Arusha tyre ya mbele ya gari tulilokuwa tukisafiria lilipancha maeneo ya Maili kumi [Korogwe] gari likaacha njia likaingia maporini bahati nzuri halikupinduka ndani ya dakika 5 tulikuwa tumezungukwa na vibaka kama hatukuwa na silaha tungekoma tukapiga risasi moja hewani wakatawanyika.Sasa pata picha Sharo alikuwa mwenyewe,keshakufa ana vitu vizuri nguo,fedha,simu na nk.

Mkuu,
Wow, mbona umenishitua unaposema jambo la kawaida kabisa. Yaani kwa Tanzania marehemu kuibiwa mpaka nguo alizovaa?
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,864
2,000
Double standard Government hizi ni mbinu za kutuondoa kwenye mijadala ya Kitaifa na kutulisha habari za kijinga, wakati haya ni matukio ya kila siku kwenye barabara zetu. Why Sharo is so special?
 

Kifarutz

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
1,740
1,225
Mkuu,
Wow, mbona umenishitua unaposema jambo la kawaida kabisa. Yaani kwa Tanzania marehemu kuibiwa mpaka nguo alizovaa?
Usisituke mkuu, kusema kweli ni jambo la kawaida marehemu kuibiwa kwenye ajali na ndo maana halisi ya ule msemo kufa kufaana. Na mbaya zaidi sometime hata majeruhi huwa wanamaliziwa ili kupoteza ushahidi. Kuna jamaa yangu ilibidi awambie vibaka, ''Jamani msiniibie mimi bado ni mzima''
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom