Hussein Mwinyi alikuwaje Mbunge wa Mkuranga wakati yeye ni Mzanzibar?

Nyerere aliuza utu na utaifa wetu kwa Wazanzibari. Leo mwanafunzi wa kizanzibari anapata mkopo wa elimu ya juu kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa kodi za Wabara.

Yote tisa kumi ni kivipi Mzanzibari anakuwa Mbunge sehemu ya Bara?

HUSSEIN MWINYI aliweza vipi kuwa MP na jimbo lake la uwakilishi kuwa Mkuranga sehemu ya Bara?
Katiba haijatamka kwamba ili uwe mbunge lazima uzaliwe eneo husika! Mkuranga ni sehemu ya JMT kama zanzibar. Think globally
 
Unaweza kuwa mbunge sehemu yoyote ndani ya Tanzania, Mana ubunge ni suala la JMT. kwa mana mbara anaruhusika kuwa mbunge Zanzibar na Mzanzibar anaruhusika kuwa mbunge Bara.
Ila suala la uraisi wa Zanzibar na wajumbe wa baraza la uwakilshi ni suala la Zanzibar tu, kwahiyo hayo wabara hayawahusu.

Ila huyu Alhaj Dr. Jr si mzanzibar, mkuranga ndipo kwao.
 
Nyerere aliuza utu na utaifa wetu kwa Wazanzibari. Leo mwanafunzi wa kizanzibari anapata mkopo wa elimu ya juu kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa kodi za Wabara.

Yote tisa kumi ni kivipi Mzanzibari anakuwa Mbunge sehemu ya Bara?

HUSSEIN MWINYI aliweza vipi kuwa MP na jimbo lake la uwakilishi kuwa Mkuranga sehemu ya Bara?
Muulize baba yake mzee Mwinyi vipi alikuwa Raisi wa Zanzibar wakati yeye sio Mzanzibari?
Vile vile mzee Jumbe aliwezaje kuwa Rausi wa Zanzibar?
 
Mbona ni jambo la kawaida sana...! Leo hii bara Raisi ni Mzanzibar, na Zanzibar Raisi ni Mbara wa Mkuranga. Kwa hiyo ni bila bila.! Fanya yako bwashee kazi Iendelee....
Hakuna rais wa bara, ni rais wa Tanzania
 
Ukitaka uwajue Wazanzibari walivyo nenda wewe ukagombee Mwanakwerekwe, au katafute tu Kiwanja Zanzibar au Pemba. Wanatuona sisi Machogo sana, wao wamejazana Mbagala na Kigamboni.
Halafu eti wanataka Zanzibar yao na wa bara wabaki na Tanganyika yao! Sikiliza hiyo

 
Mkuu THE LOST ni mapenzi ya Mungu kwa visiwa hivi kuwa karibu kabisa na fukwe za bara. Siku zote visiwa havina mwenyeji.

Ni mahali panapowakutanisha watu wa rangi na mataifa mbalimbali wanaotokea nchi kavu, ndio maana visiwa vingi vimejaa machotara, yaani damu mchanganyiko.

Wale wanaoitwa wazanzibari wengi wao asili yao ni makabila ya pwani na wachache ndio kutoka mikoa kama Kigoma na Tabora.

Watu wengi hufanya kosa la kuwaongelea wazanzibari kama vile hawana kabisa DNA za huku bara.
 
Halafu eti wanataka Zanzibar yao na wa bara wabaki na Tanganyika yao! Sikiliza hiyo


Huyu muungwana ukimfuatilia asili yake kwa maana ya vizazi vitatu nyuma utakutana na asili ya Kilwa, Tanga kwa upande wa babu na kule kwa bibi utakutana na asili ya Mombasa au Yemen.

Ule uarabu unaokuwa ndani ya damu yao huwa unawaongopea kiasi cha kuwafanya wajione watu fulani wa tabaka la juu.
 
Kwani Nchi yetu inaitwa Zanzibar au Pwani Mkuranga au ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Zanzibar ikiwa imemezwa ) ndani kama ni Kiashirio tosha Sisi ni Wamoja na Mtu ana Uhuru wa Kuishi popote na hata Kugombea Uongozi wowote pale akiamua?
Asubutu🥺
 
Familia yao ni asili ya Uzaramoni, zamani ikiwa wilaya ya Kisarawe kabla kugawanywa kuwa wilaya Y Mkuranga na walihamia Zanzibar baadhi wengine bado wapo Mkuranga. Baba yake alikuwa ana nyumba Yombo dovya kipindi akiwa raisi mama yake aliishi huko.
Na yule mpemba aliyegombea Kinondoni kupitia Chadema mbona hajaulizwa kwanini aligombea Kinondoni wakati yeye ni mpemba
 
Nyerere aliuza utu na utaifa wetu kwa Wazanzibari. Leo mwanafunzi wa kizanzibari anapata mkopo wa elimu ya juu kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa kodi za Wabara.

Yote tisa kumi ni kivipi Mzanzibari anakuwa Mbunge sehemu ya Bara?

HUSSEIN MWINYI aliweza vipi kuwa MP na jimbo lake la uwakilishi kuwa Mkuranga sehemu ya Bara?
Nadhani kuna jambo inapasa watu wali fahamu kwenye huu Mungano ukiwa wa kweli au vurugu tupu.
Zimekubalika serikali mbili.
Serikali ya Zanzibar na Serikali ya muungano.
Wa zanzibari tuu peke yao wanahaki na serikali ya Zanzibar.
Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Tanzania kwa hivyo wa Zanzibari wote ni watanzania.
Kwa hivyo watanzania ni watu wote kutoka bara na Zanzibar, na wanahaki ya kuchaguwa au kuchaguliwa popote pale Tanzania.

Kumbuka wanao kuwa na haki ya kuchaguwa au kuchaguliwa kwa zanzibar ni wazanzibari. sio wa tanzania wote.

Kwa ufupi kwa nini Zanzibar wanaupinga muungano.
Nikuwa Zanzibar imemezwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania.

Katiba ya mwanzo Ya Tanzania ni ilele ya Tanganyika isipokuwa kila penye neno Tanganyika pame futwa na kuwekwa tanzani.
Tarehe 9 december 1961 ni siku ya uhuru wa Tanganyika lakini sasa tuna sherehekea uhuru wa Tanzania.

kesho kutwa dec. 9 2021 utasikia tuna sherehekea Uhuru wa Tanzania kutimiza Miaka 60.
ukweli Tanzania haikupata Uhuru kwani haikutawaliwa ila imeundwa .
Tangu kuzaliwa kwa Tanzania ni miaka ni miaka 57 .kuanzia 26 April 1964.
 
Kwani Mwinyi si ni Mdengereko? Mkuranga na Rufiji ni kwa Wadengereko.
Kwa hiyo alikuwa sahihi kugombea ubunge Mkuranga.
Swali la kujiuliza inakuwaje Zanzibar inaongozwa na Mbara kwa nini?
 
Kuna wazanzibar wengi wanaajiriwa bara kwenye ajira ambazo si za muungano ilihali Kijana mwenye asili ya Bara hawezi kupata ajira kwenye serikali ya Mapinduzi. Kiufupi, Chao ni Chao, Chetu ni chawote.
 
Japo ni kweli Mzee Ali Hassan Mwinyi hakuwa Mzanzibari kwa kuzaliwa, kwani alihamia Zanzibar, akawa ni Mkaazi wa Zanzibar, akasoma Zanzibar, akao Zanzibar tena wakeze wote wawili, Bi Khadija na Bi. Sitti wote ni Wazanzibari, hivyo Dr. Hussein Mwinyi ni Mzanzibari kamili.
P

Nadhani asilimia kubwa ya Wazanzibari ni descendants wa walowezi kutoka Tanzania Bara. Kwahiyo, kimsingi, hawana sababu ya kuwaona recent immigrants kutoka Tanzania Bara kuwa foreigners fulani hivi, wasiokuwa na haki za kisiasa sawa na Wazanzibari wengine!
 
Back
Top Bottom