MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wakati akizungumza na waandishi wa habari aliowaita mjini Dodoma katika viwanja vya Bunge, Bashe alisema katika sheria ya mawasiliano, Serikali inalazimisha kampuni za simu kujisajili katika Soko la Hisa ndani ya miezi sita, jambo ambalo linaweza kuporomosha mtaji wa kampuni hizo kwa pamoja.
“Sikubaliani na kuwalazimisha kujisajili kwa pamoja ndani ya kipindi cha miezi sita, kufanya hivyo tutashusha thamani ya hizi kampuni… nashauri kila Mtanzania aruhusiwe kuwa na hisa katika kampuni hizi tofauti na ilivyo sasa ambapo Mtanzania mmoja mmoja ndiye ana hisa katika kampuni ya simu,”alisema Bashe.
Bashe anataka sheria ambazo hazibani makampuni ya simu kujiorozesha DSE ziendelee.
Ikumbukwe kuwa Machi, 2010, serikali ilipitisha muswada wa kuzitaka kampuni za simu nchini kuuza hisa zake kwa umma. Juni 2010 muswada ukawa sheria kwamba baada ya miaka mitatu, zinatakiwa ziwe zimeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Lakini cha kushangaza huku kukiwa na harufu ya rushwa na ufisadi, Julai 2010 kifungu cha sheria kilifanyiwa marekebisho na kusomeka kwamba, kampuni za simu zinaweza kuorodhesha hisa sokoni baada ya kushauriana au kufanya mazungumzo na waziri mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kwa maana nyingine, serikali iliufyata ili makampuni ya simu yaendelee kukwepa kodi.
Ieleweke kuwa, sehemu ambayo serikali imekosa mabilioni kwa njia ya kodi ni kwenye makampuni ya simu na haya makampuni yalifanya kila linalowezekana ili yasilazimishwe kisheria kuuza hisa zake kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa sababu kama yatauza hisa zake DSE itayalazimu kisheria kuweka wazi vitabu vyake vya taarifa za fedha na Hesabu za kampuni zitaandaliwa kwa umakini zaidi.
Suala la kupika taarifa za fedha inakuwa ni ngumu kwa sababu Wakaguzi wa hesabu za kampuni wanatakiwa wawe na sifa za ziada ambao wamesajiliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu, pia inabidi The Capital Markets and Securities Authority (CMSA) iwe imewapitisha.
Pamoja na serikali kutoa punguzo la kodi kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 25 kwa Kampuni zinapoorodhesha hisa zake sokoni lakini haya makampuni ya simu hayakutaka kuorodhesha hisa zake DSE kwa sababu faida yaliyokuwa yanapata kwa kutolipa kodi ni kubwa zaidi ya kupata asilimia 5 kama nafuu ya kodi.
Bashe hakutaka kuona umuhimu wa hatua ya serikali na badala yake aliitisha press conference kupinga hii hatua ya serikali ya Rais Magufuli ambayo kwa sasa inayalazimisha kisheria makampuni ya simu kuorodhesha hisa zake katika soko la hisa(DSE) na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 01, 2016 ili kutoa fursa kwa Watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo na pia kuisaidia serikali kukusanya kodi stahiki.
Are we dealing with fierce personal interest or cash for questions affair?
Kwa maelezo zaidi unaweza kupitia hizi thread;