john agrey
JF-Expert Member
- Jan 24, 2015
- 1,280
- 2,079
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), ameeleza kukunwa na nyaraka na maandiko ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, yanayohusu madini ya Tanzania. Akichangia bungeni Bashe alisema baada ya kusoma maandiko hayo hadi usiku mnene, alibaini Tanzania imeibiwa vya kutosha kwenye sekta hiyo.
“Jana (juzi) nilienda kumuomba Lissu anipe yale maandiko yake na alinipe nimeyasoma sana na hadi saa tisa usiku nilikuwa nayasoma maandiko yale ukisoma maandiko ya Jaji Bomani na kesi ambayo yeye Lissu aliisimamia mwaka 2006, nchi hii imeibiwa kwa muda mrefu sana.
Bunge limefanya makosa na huko nyuma tumefanya makosa, sasa tumepata mtu (Rais Magufuli) wa kupambana na rasilimali za nchi hii tumuunge mkono Watanzania," alisema.