Hussein Bashe: Nilimwambia Rais, mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee


K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,691
Likes
2,207
Points
280
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,691 2,207 280
bashe-jpg.622015

Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema 'Ndiyo' mzee.

Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.

"Mimi nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko' huo ndio msimamo wangu na siku naona kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali" alisema Bashe

Aidha Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamshauri vinginevyo ili na yeye akiingia akae kimya avute pesa na kutulia kimya.

"Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM huwezi kumuachia mtoto wa jirani kutatua matatizo ya ndani ya nyumba yenu na huo ndiyo msimamo wangu lakini wazee mkisema baba eeh wewe nenda kawa mzee wa ndiyo mzee, zikija vuta saini nenda zako mtaani basi nitafanya hivyo kwa sababu nitakula good time kama wabunge wengine" alisisitiza Bashe

Mbali na hilo Bashe amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa wanapoelekea mwaka wa 2020 kuwa changamoto ya maji, umeme itakuwa historia jimboni hapo na kusema katika suala la elimu watahakikisha wanafika kiwango ambacho watajivunia.

EATV
 
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
19,305
Likes
11,610
Points
280
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
19,305 11,610 280
Mbona hajaeleza alichofanya toka hiyo 2015,au aliwaita watu kuwaambia hatakua "ndio mzee"
 
B

betty marandu

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2011
Messages
830
Likes
358
Points
80
B

betty marandu

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2011
830 358 80
kiapo chetu nitasema kweli daima,kipo nyuma ya kadi,mafisadi na mawakala wao watachomoka mmoja baada ya mwingine
Kama kweli mnasema kweli daima watajeni hao mafisadi na mawakala wao na muwatoe ndani ya ccm muache kulalama pindi wanachama wanapoondoka.Hivi kwani MTU akishatoka ccm ndo hujulikana fisadi wakati akiwamo huwa hamuwajui?Acheni unafiki
 
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
14,523
Likes
4,343
Points
280
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2012
14,523 4,343 280
......
.....kwa heri giza
 
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
3,601
Likes
3,540
Points
280
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
3,601 3,540 280
Daahh... Huyu hana tuhuma lakini siku akitoka ccm tutaskia mengi!
 

Forum statistics

Threads 1,238,030
Members 475,830
Posts 29,310,139