mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Nimesoma na kuvutiwa na habari ya gazeti la Mwananchi la leo Jumatano, Januari 18, 2017 yenye kichwa "Bashe: Nimekusudia kuleta mabadiliko Nzega Mjini".
Kama kilichoandikwa kwenye hilo gazeti (nimerejea baadhi hapa chini) ni ukweli, basi Wabunge wenzake wanapaswa kuiga huo mfano badala ya kulilia kuoneshwa "live" bungeni, au mikutano ya hadhara na maandamano.
Wabunge walilie kuandikwa kwenye magazeti, au kuoneshwa "live" shughuli wanazofanya, kama wabunge, kuleta mabadiliko kwenye majimbo yao ya uchaguzi.
Habari kuhusu baadhi ya shughuli za Mh Bashe jimboni kwake, akisimamia utekelezaji wa ilani ya chama chake (kwenye sekta ya elimu, afya, miundo mbinu na huduma za jamii), kama zilivyoandikwa gazetini, ni kama zifuatazo:
1) Elimu: ujenzi wa vyumba 13 vya madarasa, na bado ujenzi unaendelea. Kwa kidato cha 5&6, ujenzi wa madarasa 2 na bweni umekamilika katika Shule ya Sekondari Bulunde.
2) Afya: kukamilika kwa ujenzi wa zahanati Kata ya Nhobola. Ujenzi wa nyumba ya mganga unakaribia kukamilika. Kupitia Wizara ya Afya, jimbo limepata gari la kutumia kutoa huduma za afya.
3) Maji: visima virefu 6 vya maji vimechimbwa. Wakati Rais alipotembelea jimbo, walimwomba Sh 200m ambazo wamepatiwa na zaidi, kwa ajili ya mradi wa maji katika mji wa Nzega.
4) Ujasiriamali: vikundi 40 vya wananchi katika jimbo, baada ya kuhamishwa kuanzishwa kwake, vimekopeshwa fedha (Sh 20m kutoka ofisi ya Mbunge na Airtel nao wakatoa Sh 20m) kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Ni imani yangu, na Watanzania wenye kutaka mabadiliko ya kweli, kuwaunga mkono Wabunge kama Mh Bashe.
Naamini pia Waheshimiwa Wabunge wengine watatupa mrejesho wa shughuli zao, tangu wachaguliwe. Waache siasa za majukwaani na maandamano, au kupiga vijembe Serikali kwa maneno matupu.
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA.