Hussein Bashe aionya serikali, ataka mgomo wa Madaktari Muhimbili lisishughulikiwe kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hussein Bashe aionya serikali, ataka mgomo wa Madaktari Muhimbili lisishughulikiwe kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Jan 9, 2012.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Source ya hii taarifa ni facebook ya Hussein Bashe

  Ndg zangu Leo nimefika Hospitali ya Taifa baada ya kupigiwa simu na Mgonjwa ambae ni Mkazi wa Wilaya Nzega ambae amekuwepo hapo kwa siku Nne bila Huduma imebidi nimtoe na kumpeleka Hospitali ya Aghakhan ambako nimemuacha anapata Huduma.

  Kilichonisukuma kuandika andiko hili ni kuiomba Serikali Tatizo la Madaktari lisichukuliwe kisiasa na si vyema kutumia Ubabe katika kutaka kulitatua tatizo hili wanao umia si Viongozi Bali ni watanzania wanyonge ambao walikipa dhamana Chama cha Mapinduzi, kwanza Madaktari wanachodai ni Haki Yao ya msingi kuwafukuza si suluhisho,kutowalipa pia sio suluhisho ni vizuri kutofanyia Siasa na Ubabe Swala hili niombe wakubwa walitazame jambo hili kwa haraka kuna wagonjwa Muhimbili hawajapata Huduma kwa siku nne nimeshuudia wagonjwa wanavolalamika.

  Madaktari ni Watanzania Kama kuna UKATA why not kukutana nao kuongea nao officially? We can only solve our problem through mazungumzo ktk hili nadhani serikali inawajibu wa kulitatua kuokoa Watanzania wanao umia bila hatia.

  Naamini Swala hili lisipofanyiwa siasa na Ubabe tutaokoa maisha na maumivu ya wananchi wasiokua na Hatia
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ilo lawezekana ila sio ktk serikali ya JK.
  Maana sio wehu wale wakagoma wana madai ya msingi badala ya kuwasikiliza serikali inaleta jazba
   
 3. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ni maamuzi ya kipumbavu na ubabe wa kizamani. Huwezi elewa kama hapo ktk Wizara ya Afya kuna wasomi. Hii Wizara ingekuwa enzi za Mwalimu Nyerere angeipangua kuanzia waziri.katibu mkuu mpaka wakurugenzi! Wanacheza na maisha ya Watanzania.
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Vitu vingine Mkuu vinahitaji kutumia hekima, ila kwa vile hawa wakubwa hawana wagonjwa Muhimbili maana wa kwao wakiumwa wanakimbilia Apolo India na kwingineko wanashindwa kuelewa madhara ya kuwanyanyasa madaktari!

  Kwanini madaktari wasilipwe vizuri, mbona wabunge wanadai posho wanaskilizwa kama si kelele za watu wangesha lipwa? Wasitwambie hakuna fedha je, nivikao vingapi Tanzania nzima vinafanyika na watu wanalipwa kuanzia Halimashauri, Wilayani, Manispaa, Mikoani, Wizarani fedha zinatoka wapi za vikao?

  Serikali ishughulikie swala la madaktari kwa hekima na busara bila jaziba, kukurupuka na kutojali madhara ya maamuzi yao wanaoteseka ni wanyonge wasio na namna ya kwenda private Hsp wala India na kwingineko!
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Bashe hajui au anafanya makusudi? Kweli hajui kama serikari ya mkw€re imefilisika? Mimi sidhan kama bashe haelewi kuwa suluhisho pekee kwa serikali mufilisi ni kutumia ubabe.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Umesema vyema sana .Wasi wasi kama kesho uraia wako hutahojiwa ila kwa kuwa wewe uko na RA hakuna mbungi.Watanzania ikateni CCM kwa njia ya kura .Ikataeni uchaguzi wa mitaa unao kuja .
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  anajua ila nae anasema!
   
 8. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  well said Bashe, you guy seem to be talking sense most of time.
   
 9. so who

  so who Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo waziri wa fedha yupowapi maana mara ya mwisho desemba nilisikia kapata oc kaenda jimboni kwake anasema kuna watu wanataka afukuzwe CCM iliakose uwaziri sasa tu na wazri anaota kufukuzwa CCM watumishi nyeti wanalalamika hawjalipwa nyie wizara ya afya mtukamatie huyu waziri tumuulize mara ya mwisho kapeleka lini fedha muhimbili madaktari warudi kazini halafu sisi tununue haya maandamano mpaka wizara ya fedha watuonyeshe mgao wa fedha za desemba ulikuwa vipi maana nae yule kwa mbwembwe za kusema hawajafilifilisika hajambo! dalili za kufilisika mbona zipo wazi tu ona siku ya mafuriko jangwani mkuu wa mkoa statement ya kwanza kabla hajaanza kuokoa watu anasema mafuriko yametokea jangwani tunategemea misaada kutoka kwa wasamaria wema hata hajafika eneo la tukio anapanga jinsi ya kuanza kupokea misaada njaa mbaya jamani mkulo sema usiogope sema kama fedha zimekushinda kugawa kutokana na vipaumbele halisi.
   
 10. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kutoka rohoni mwangu huwa naona kabisa mtu kama Bashe na Nape wako ant ccm na wana qualfy kabisa kuendesha harakati zao za kisiasa wakiwa chama cha upinzani kama cdm,ccm inazama jamani kulikoni hawa vijana??!!!Eeeh kina January eti ccm kisa nini?chama cha Baba?!!Ajabu hata Jf wanaikimbia wako facebook daily si waje jf wasidiwe kimawazo jamaniiiiiiiii
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa. kwenye mpira timu ikizidiwa huwa inaanza kutembeza viatu kwa timu pinzani kuikata makali! lol
   
 12. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Well ni kweli unalosema lakini si sawa kusema maamuzi yanafanywa kisiasa kwa kuwa siasa unataka itoe defnition ya kuwa mambo yanafanywa bila utaalamu....maauzi yote ya serkali duniani yanafanywa kisiasa na hata taratibu za kuamua wao wakae pale pia ni ya kisiasa.kweli walicheleweshewa posho zao kwa wiki moja lakini wiki moja inatosha kuanza kugoma na kuacha wagonjwa tena kwa daktaria alieapa kumsaidia mgonjwa?....madaktari tanzania nzima hawakulipwa na kwa nini wa nuhimbili peke yao ndio wagome tena baada ya kupewa malipo ya wiki moja kupunguza makali ya maisha na kuahidiwa kulipwa baada ya wiki moja....serkali ifanye kazi yake.chukua intern walioko kasulu na mbalizi waje muhimbili na peleka hao wa muhimbili uko kibondo.....hata akili ya kugoma inayeyuka.Serkali ifanye juhudi kwa kuwa hali ya uchumi duniani ni ngumu.Hivi kila ambaye mshahara wake ukichelewa wiki moja akigoma hapa Tanzania ni kampuni gani itafanya kazi?
   
 13. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa kaya (Baba Riz) wapigie magoti RA na EL wakusaidie kuwalipa hawa watumishi wako. Tumia ule usemi wetu ''If u can not fight them, join them''
   
 14. j

  jigoku JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  wewe Fisadi mtoto umenichefua roho yangu,waambie hao mafisadi baba zako watangaze rasmi nchi imefilisika,haina kitu wananchi watawaelewa sio kufukuza watu wakidai haki yao,kumcheleweshea mtu haki yake hata kwa nusu saa ni kosa kubwa,wewe mtoto na wazazi wako mafisadi tangazeni rasmi chi imefilisika hata wananchi watawaelewa na mtoe sababu,hat kama fedha zote mmezifanyia ufisadi semeni ukweli ili wananchi wawa hukumu,unanyamaza watu wanajiuliza kwanini hawalipwi,walimu nao wanadai kila mahali wanadai mtakoma kushabikia ufisadimwisho wa siku umma utadai na hapo ndio mwisho wenu.
   
 15. vimon

  vimon Senior Member

  #15
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  wewe ni pimbi hujui kitu funga domo lako.
   
 16. D

  Dan08 Member

  #16
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 23, 2009
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  unalijua unalo lisema kweli au umejazwa propaganda nawe unazisema bila kujua..collegues wenzetu kwanza wanadai haki yao ya msingi na walipaswa wapewe ushirikiano na wizara,kama ulivyosema kucheleweshewa mshahara sio jambo geni,na mara zingine unachelewa hata zaidi ya wiki lakini hakuna mgomo,tatizo hapa ni kukosa ushirikiano na wizara na majibu yakibabe yasiyoeleweka yanayotolewa na wizara
   
 17. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kama kweli sirikal imefilisika kwa nini vigogo wanatibiwa nje ya TZ kwa fedha nyingi huenda ni zaidi ya hizo Madaktari wanazozi dai? Sirikali haiwajali wananchi wake!!!
   
Loading...