asante kwa ufafanuzi mzuri mkuu.
Kuna wakati mke au mke wanatengana kwa muda hata miaka 2 au 3, then, ndo wanaamua kupeana talaka baada ya kipindi hicho. swali: mali wanayochuma wakati hawapo pamoja inakuwaje! Nayo wanagawana?. Kama nyumba ilikuwa haijapauliwa, mke akajitenga akamwacha mme akamalizia nyumba na kufanya finishing zote, inachukuliwaje kimahakama?
Mkiamua kutengana tu,bila kwenda mahakamani.Mtaendelea kutambulika kama wanandoa?Hata kama kila mmoja anaishi na mwenzi mwingine na labda alishazaa huko na mwenzi alienae.
Kisheria hakuna muda maalum wa kuachana, hata dakika tano baada ya kufunga ndoa mwaweza kuachana. Ila ni lazima kuwe na sababu za msingi zilizoainishwa kisheria kama kutelekeza, uzinzi na ukatili. Hayo yanaufafanuzi wake. Kuna sababu nyingine zinazoandamana na hizo kama hamjafanya tendo la ndoa baada ya ndoa, ugonjwa usiopona ambao unasababisha kutofanya unyumba na pia kama umegundua ni maharimu na mlikuwa hamfahamu.
Nimeuliza tu,mimi ndoa yangu ni mpaka kifo kitutenganishe,kama amri ya Mungu ilivyo.
Ndugu, ni kweli lakini kulingana na Sheria ya Ndoa ya Tanzania, mahakama ndio chombo chenye mamlaka ya kusema kuwa ndoa imevunjika, na kabla ya miaka miwili ya ndoa huwezi kufungua shauri la divorce mpaka upate ruhusa ya mahakama. Unaweza kuruhusiwa kufungua shauri la divorce kabla ya huo muda kama kuna exceptional hardship.

acha uvivu wa kufikirialiyewaunganisha MUNGU BINADAMU asiwatenganishe
Tuko pamoja ndugu Bondpost, lakini kuna jambo lingine linanitatiza. Vipi kuhusu talaka tatu? Kwani hizi nazo mpaka ziende mahakamani au nikimtwanga mwenzangu inatosha? Sijaziona kwenye Sheria ya Ndoa.