HUPI MUDA WA KUACHAMA NA MKE au MME WAKO KISHERIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HUPI MUDA WA KUACHAMA NA MKE au MME WAKO KISHERIA

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by WILSON MWIJAGE, Feb 6, 2012.

 1. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Katika kipindi cha miaka miwili mfululizo mahakama inaridhika kwamba X na Y ni mme na mke ilimradi tu walikuwa wanaishi wote chini ya paa moja. Je ni kwa kipindi cha muda gani mahakama itaridhika kisheria kwamba mme ametendana na mke wake au mke ametengana na mme wake?
  :lol:
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  miaka 2 kama hawajawai kuwapamoja kama mke na mume ndoa inafutika nilivyockia mm
   
 3. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Nashukru kwa majibu yako, nadhani ni mwanzo nzuri kwangu
   
 4. c

  christer Senior Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  u

  una maanisha kuwa na uhusiano wa kinyumba?sijakupata vyema
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Only and when the marriage broken down beyond repair and hence issue of Court Decree for Divorce nad custody of the child if any. Na kama kuna mali mgawane pia sio ujue kuacha tu.
   
 6. k

  kakolo Senior Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Jamani hiyo mali inayogawanwa ni ipi? Yote au mliyochuma pamoja?
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  aliyewaunganisha MUNGU BINADAMU asiwatenganishe
   
 8. m

  muleba Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ni mwanasheria nataka nitolee ufafanuzi suala hili, hakuna muda maalum wakuachana kusheria ila kuaa mbali kwa muda wa miaka 3 bila kuwa under the same roof then a party to the marriage can use that as one among the grounds for divorce na ni lazima iwe kwa miaka 3 mfululizo.

  Pia kuna other grounds like adulterly ambayo ni uzinzi kwa kiswahili nadhan, kubadili imani na kuwa na imani ambayo mwenzako wa ndoa haielewi na inampa mashaka.

  Kuugua magonjwa ya kumfanya mwanaume asiweze kuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa na mkewe ambacho ni kitu muhimu na sababu zingine nitasema cku ingine.
   
 9. B

  Bandio Senior Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Vipi kama wanandoa wamekubaliana kwa hiari yao kuwa mbali under certain circumstances inaweza kuchukuliwa pia kama ground ya divorce?
   
 10. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Asante sana kwa ufafanuzi wa kina, lakini kama alivyosema Muleba; Chukulia kwamba tumekubaliana mimi na mke wangu kwamba aende kwao kufuatana na hali ngumu ya kimaisha inayotukabili mpaka hapo itakapo tengamana. Je nao ni muda wa miaka mitatu ndipo ninaweza au anaweza kudai taraka mahakamani na mahakama ikaridhika?
   
 11. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sorry, niliposema "....... alivyosema Muleba ........" nilikuwa namaanisha Bandio!
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Jamani tusije wote tukaoneka hatujui lugha yetu ya kiswahili....
  Jamaa nasema ....HUPI!! ......badala ya Upi!!!!!!!!
  Edit bwana ni Upi, upi, siyo Hupi!
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Haya makabila haya...'sa zingine' inabidi tuchukuliane tu hivyo hivyo! Mwanzoni nilidhani tatizo hili lipo kwenye matamshi tu kumbe hata kwenye kuandika lipo!
   
 14. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  DUH! Hata kwenye kuandika!....basi tutawakoma Wajuluo humu.
   
 15. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kisheria hakuna muda maalum wa kuachana, hata dakika tano baada ya kufunga ndoa mwaweza kuachana. Ila ni lazima kuwe na sababu za msingi zilizoainishwa kisheria kama kutelekeza, uzinzi na ukatili. Hayo yanaufafanuzi wake. Kuna sababu nyingine zinazoandamana na hizo kama hamjafanya tendo la ndoa baada ya ndoa, ugonjwa usiopona ambao unasababisha kutofanya unyumba na pia kama umegundua ni maharimu na mlikuwa hamfahamu.
   
 16. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kumbuka suala la mwenza kuwa mbali kwa muda sio kigezo tosha kwa maana mwaweza kuwa bado mnamawasiliano ya kawaida na mnakutana baada ya muda fulani hauwezi kuvunja ndoa. Kama yupo mbali na amekutelekeza kwa maana ya kwamba hata mwanamke anaweza kumtelekeza mume mahakama ikiridhika pamoja na mengineyo yaweza kutoa amri ya kutengua ndoa.

  Ila mahakama haiangalii suala moja kwa hiyo ni lazima uwe na ushahidi mzito wa kuishawishi mahakama kwamba ndoa hiyo haiwezekana kuwepo kisheria tunasema 'the marriage is broken irreperably or irretrievably' to the extent kwamba no way the two will live in hostility.
   
 17. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Suala ya mgawanyo wa mali na custody of children huja baada ya kutatua ishu ya whether the marriage is broken irreperably, mali hugawanywa ile tu iliyopatikana baada ya ndoa kwa maana tunapresume wote wawili mmechangia nguvu kwa namna moja au nyingine na hapa haswa wanawake lazima mfahamu mume pia yupo entitled kupewa ulichochuma wakati wa ndoa.

  Kama nyumba haikujengwa wakati wa ndoa lakini mlihamia baada ya harusi na mkaishi maisha yenu hapo, pia huchukuliwa kuwa 'matrimonial home' so inaweza kuingizwa kwenye mgawanyo wa mali. Ila zawadi na mali zilipatikana kabla ya ndoa hazitaguswa.
   
 18. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Ishu ya custody of children huangaliwa zaidi katika the best interest of the child. Ataangaliwa ni wapi atafaidika na malezi pia yeye mtoto mapenzi yake yako kukaa wapi although kuna umri mtoto husikilizwa lakini kama yupo chini ya miaka saba atakaa kwa mama yake ni lazima ila akiwa zaidi anaweza kusikilizwa kwa kuangalia wapi atapata malezi bora. Kwa ufupi nadhani nimeeleweka wadau. Nimejaribu kufupisha sana hapo. Suala la msingi ni lazima ifahamike, ndoa kuitengua huwa ni kazi kubwa sana mpaka mahakama iridhike na kuna vigezo vingi sana mpaka mahakama ifikie uamuzi wa kutengua ndoa. Marriage is an institution where citizens come from, therefore the state has a big interest in marriages.
   
 19. n

  ngilenengo1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 933
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  asante kwa ufafanuzi mzuri mkuu.

  Kuna wakati mke au mke wanatengana kwa muda hata miaka 2 au 3, then, ndo wanaamua kupeana talaka baada ya kipindi hicho. swali: mali wanayochuma wakati hawapo pamoja inakuwaje! Nayo wanagawana?. Kama nyumba ilikuwa haijapauliwa, mke akajitenga akamwacha mme akamalizia nyumba na kufanya finishing zote, inachukuliwaje kimahakama?
   
 20. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sio kila kitu kaunganisha Mungu.Ndoa za kisheria kaunganisha mwanadamu,kwa hiyo zinaweza zikavunjwa!
   
Loading...