Humu ndani ukiondoka na mawazo, basi unahitaji mtaalamu wa saikolojia

roselyn2

Member
Jun 7, 2022
86
379
Nimeona si vyema kama sintowajulia hali members wenzangu, wanafamilia wangu, samahanini kama nitakuwa naandika upuuzi kabla hamjaanza kunishushia michambo

Tokea nimejiunga humu kwenye majukwaa ya jamii, naweza sema kwa asilimia 80 mawazo yamepungua, imekuwa ni sehemu ya kutulizia akili, kwa sababu utaingia humu ndani utakutana na visa vya hapa na pale, istoshe ni mahali ambapo watu hatufahamiani kwa ukaribu lakini tunaishi kindugu, tunakwazana kwenye uzi mmoja, tunaenda kupatana kwenye uzi mwingine

Tunaishi pasipo kufahamiana, lakini kupitia mchango na mawazo ya mtu, unakuwa tayari ushajenga taswira ya mhusika, mzabzab ni kama vile namuona mpaka tabia maake si kwa jinsi anavyoreply nyuzi za watu, ni kana kijana mwongeaji, mwembamba, mcharuko anaependa kumchangamkia kila dada, kila mke wa mtu

Kama namuona Sky Eclat kama mama ambaye hucheka na wanae wawili akitoka kazini huku kawabebea vijizawadi, ni mtu wa kuhasa na kutoa ushauri kwa watu hususan wanawake, namuona ni mnene wa size, mrefu kidogo

Namuona pia DeepPond kama baba ambaye ni mcheshi kwenye familia yake ila yuko makini na simu yake mfukoni akihofia mkewe kutofumania sms za mama J

Nafurahi pia kuwaona mashost zangu wakina to yeye cocastic Depal financial services binti kiziwi na wengine wengi jinsi wanavyoishi kama majirani waliopanga nyumba moja, mara chache kutomkuta cocastic kwenye uzi aliochangia to yeye, nawapenda sana

Ila kuna hawa man biznes na mpwayungu village ee mola wasaidie watoto wa watu, ni kama rika yangu hivi, si kwa utoto jamani walionao napenda sana kusoma nyuzi zao, wanatengeneza uzi nyingi, very funny, napenda sana chai zenu, mna vipaji, keep it up mje mtuuzie vitabu siku moja natamani tuonane siku moja

Ni wengi tu mnaolifanya jukwaa kuwa la moto, nitawaelezea zaidi wengine kwenye huu uzi

Najihisi furaha kuifahamu jamii forums, mahali ambapo moyo wangu husuuzika napoteza mawazo, nakuwa mpya

Asanteni sana, Mungu awabariki katika majukumu yenu ya hapa na pale, nawapenda nyote

rikiboy Extrovert Bujibuji Simba Nyamaume Smart AJ Smart911 Kunguru wa Manzese Mtoto halali na hela @
 
Humu ndani kuna watu wamefanyika baraka kwenye maisha yetu nje ya jf kwa namna moja ama nyingine, katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kimahusiano na kishostito…

Jf idumuuu,, na member wake…
You can say that again babygal😘

Aki bila jf ningepata wapi mie shost anayenipa kicheko muda wote😍

JF idumu
Idumuuuu
Idumu tena👏👏
 
Kitu kigumu katika maisha ni kuzoeana na kujuana na watu, Naimagine wewe unaweza kuzoea watu ambao hata hamjuani wala kuonana na even kukariri ID's. that's strange and new to me.

JF naona kama mtandao tu ambao naingia sometimes nacomment nonsense au vitu vya msingi alafu nalog out.
Kuna kitu kinaniambia lazima utakuwa mpweke wewe na JF ni escape door from reality.

Digital social life.
 
Nimeona si vyema kama sintowajulia hali members wenzangu, wanafamilia wangu, samahanini kama nitakuwa naandika upuuzi kabla hamjaanza kunishushia michambo

Tokea nimejiunga humu kwenye majukwaa ya jamii, naweza sema kwa asilimia 80 mawazo yamepungua, imekuwa ni sehemu ya kutulizia akili, kwa sababu utaingia humu ndani utakutana na visa vya hapa na pale, istoshe ni mahali ambapo watu hatufahamiani kwa ukaribu lakini tunaishi kindugu, tunakwazana kwenye uzi mmoja, tunaenda kupatana kwenye uzi mwingine

Tunaishi pasipo kufahamiana, lakini kupitia mchango na mawazo ya mtu, unakuwa tayari ushajenga taswira ya mhusika, mzabzab ni kama vile namuona mpaka tabia maake si kwa jinsi anavyoreply nyuzi za watu, ni kana kijana mwongeaji, mwembamba, mcharuko anaependa kumchangamkia kila dada, kila mke wa mtu

Kama namuona Sky Eclat kama mama ambaye hucheka na wanae wawili akitoka kazini huku kawabebea vijizawadi, ni mtu wa kuhasa na kutoa ushauri kwa watu hususan wanawake, namuona ni mnene wa size, mrefu kidogo

Namuona pia DeepPond kama baba ambaye ni mcheshi kwenye familia yake ila yuko makini na simu yake mfukoni akihofia mkewe kutofumania sms za mama J

Nafurahi pia kuwaona mashost zangu wakina to yeye cocastic Depal financial services binti kiziwi na wengine wengi jinsi wanavyoishi kama majirani waliopanga nyumba moja, mara chache kutomkuta cocastic kwenye uzi aliochangia to yeye, nawapenda sana

Ila kuna hawa man biznes na mpwayungu village ee mola wasaidie watoto wa watu, ni kama rika yangu hivi, si kwa utoto jamani walionao napenda sana kusoma nyuzi zao, wanatengeneza uzi nyingi, very funny, napenda sana chai zenu, mna vipaji, keep it up mje mtuuzie vitabu siku moja natamani tuonane siku moja

Ni wengi tu mnaolifanya jukwaa kuwa la moto, nitawaelezea zaidi wengine kwenye huu uzi

Najihisi furaha kuifahamu jamii forums, mahali ambapo moyo wangu husuuzika napoteza mawazo, nakuwa mpya

Asanteni sana, Mungu awabariki katika majukumu yenu ya hapa na pale, nawapenda nyote

rikiboy Extrovert Bujibuji Simba Nyamaume Smart AJ Smart911 Kunguru wa Manzese Mtoto halali na hela @
Financial service ana muda haonekani huku,.ebu niulizien..asije akawa analea ka babu kalikopokea mafao yake
 
Back
Top Bottom