Humu JF kuna watu waongo, ukifukua makaburi utastaajabu

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,024
24,374
Kati ya mambo yanayoniacha hoi humu jf, ni baadhi ya watu kuja na nyuzi zao ambazo baadae zinageuka na kuwa pindua pindua hasa kwenye jukwa la MMU.

Unakuta mtu analeta uzi ambao unaonyesha yeye ni mwanaume lakini anakuja na mwingine unaoonyesha yeye ni mwanamke na unakuta watu ambao labda pengine ni wageni au kutokana na kufuatilia sana nyuzi humu wanakuwa wanachangia pasipo kushtukia hilo! Hiki ni kituko aisee.

Mwingine analeta uzi kuwa yupo nyumbani hana kazi tokea mwezi may, anatafuta, then baadae analeta uzi unaoonyesha anakazi ambayo aliipata tokea mwaka jana na anaendelea nayo na imempa mafanikio makubwa!

Mwingine analeta uzi unaonyesha ana elimu ya chuo kikuu, ngazi ya degree halafu baada ya muda unakutana na uzi mwingine ambao anasema elimu yake ya kiwango cha juu ni cheti au kidato cha nne.

Hili jambo kuna wadau humu wanaliona na wanachimba kweli makaburi, na mtu ukikomaliwa utaona jf ilivyo na ladha yake halisi!!
 
Usipate nao shida! Hao ni wana JF wenye ndimi mbili, ndumila kuwili wakubwa hao!

tongue-splitting.jpg
 
Watu kama hao ndio wanaofanya JF inoge

Humu utasikia,nina gari,nina masters,....yani ni full kupeana stress tu ,wengine utasikia nafanya kazi kwenye shirika moja kubwa hapa mjini....baada ya week anakuja tena na uzi mwengine...."natafuta kazi yoyote iliyo halali elimu yangu darasa la saba"
 

Similar Discussions

19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom