Humphrey Polepole: Vyama vya Upinzani vimekosa uhalali wa kutaka maridhiano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
1581057987113.png

Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi wa CCM Taifa, Ndg. Humphrey Polepole katika mkutano wa Kuadhimisha miaka 43 ya CCM wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, ameeleza kuwa Wamefuatilia mijadala na mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya Upinzani kuhusu kufanya maridhiano, Ndg Polepole anaeleza maridhiano ni hatua na vyama vya upinzani nchini vimeshindwa tangu mwanzo na hata sasa kuzingatia hatua za msingi na za awali kabla ya kufikia hatua ya maridhiano

na hivyo kukosa uhalali wa kutaka maridhiano, kwani maridhiano huanza kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo ya msingi, pili kujenga muafaka na tatu kuwa na maridhiano yenyewe.

Akifafanua kuhusu dhana na nadharia ya maridhiano, Ndg. Polepole amesema, kwanza kuwepo na uelewa wa pamoja juu nini watanzania wanataka, kazi kubwa ya maendeleo ambayo imekwisha kufanyika nchini na kubadilisha kabisa hali na ustawi wa watu, pili ni kuwa muafaka wa kitaifa kwa maana ya kukubaliana katika kazi nzuri ambayo imefanyika na katika yale ambayo hakuna muafaka ndio tunakwenda katika maridhiano.

Awali akihutubia mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 43 ya CCM, Ndg Polepole ameeleza ni kwa namna gani Chama cha Mapinduzi kimejipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, huku akiangazia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 43 ya CCM na kwa umahsusi mafanikio ya serikali ya awamu tano chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.

Kauli mbiu ya Miaka 43 ya CCM ni Tuliahidi, Tumetekeleza na Tunaahidi Tena kuchapa kazi kwa juhudi, Ubunifu na Maarifa Zaidi

Credit: Emmanuel Mbatilo
 
Huyu alishasema kwenye uchaguzi huru na wa haki, sisiemu ijiandae kukabidhi madaraka.. Sasa leo amegeuka kukitetea hicho hicho alichokuwa anakipinga.. Mwanaume kukosa msimamo ni sawa na Simba dume kukosa manyoya ya shingoni.. Bwege tu anakuwa..
 
Huyu alishasema kwenye uchaguzi huru na wa haki, sisiemu ijiandae kukabidhi madaraka.. Sasa leo amegeuka kukitetea hicho hicho alichokuwa anakipinga.. Mwanaume kukosa msimamo ni sawa na Simba dume kukosa manyoya ya shingoni.. Bwege tu anakuwa..
alipokuwa anajiita mwanaharakati alikuwa anaiponda sana ccm ila baada ya kuteuliwa ccm kapata ugali hivyo anaupigania ugali asiukose
namfananisha na mwanamke asiye na msimamo(mchepukaji)
 
Ana uelewa wa polepole, muda utafika ataelewa akiwa anakimbia.
Nashindwa kujadili contents zake sababu ya ufinyu wa kiakili alioutumia kujenga hoja yake


Kwa hiyo wewe ndo una uwingi wa akili na una uwezo wa kujenga hoja?
 
Huyu aliyezunguka nchi nzima na kujenga jina kwa kusisitiza umuhimu wa katiba mpya na baada ya cheo akaikanyagia mbali na kusifia uongozi unaopuuza umuhimu was katiba hiyo. Kumwamini polepole no upuuzi mkubwa kama kuamini mitume/manabii feki kina nabii Tito
 
”kazi kubwa ya maendeleo ambayo imekwisha kufanyika nchini na kubadilisha kabisa hali na ustawi wa watu” 🤔🤔🤔
Maisha ni magumu sana mtaani.
Tumenyooka (tunalimia meno) ustawi uko wapi?! Mungu anakuona polepole..!
 
Back
Top Bottom