Humphrey Polepole unaamaanisha nini kusema hivi?

Nawasalimu kwa jina la Tanzania

Polepole amenukuliwa akisema kuwa katika awamu ya Tano aloondoka ni mtu mmoja tu MAGUFULI , lkn serikali ni ileile ,chama ni kilekile

hivyo hakuna awamu ya sita ,Tusiwe tunachanganya.

SWALI?
Wataalam humu ndani naombeni nielemishwe "kwa hiyo anachosema POLEPOLE ni sahihi " kwamba hii serikali anayoongoza mama ni ya Awamu ya Tano na si ya Sita na tumhesabie awamu ya sita 2025?

Na je?

Ikitokea Mama asigombee awamu ya 2025 awamu ya tano itahesabika imetawala kwa miaka 10 ( vipindi vyote viwili)

Kwa unyenyekevu naomba kuelimishwa maana kipindi hiki Tunachanganywa sana jmn!!! kila mtu ana lake jambo tunashindwa kujua which is which.

karibuni !
View attachment 2033387
Tunahangaika sana na mambo anayoyasema na mengi ni ya kufikirika/kudhania maana hana ushahidi wowote na naona kama tunapoteza muda bure.
 
Ni awamu ya sita kwa sababu kipindi cha pili awamu ya tano hakikufikia nusu ya muda wake kwa hiyo hakina sifa ya kuitwa awamu kwa maana hiyo Rais aliyepo kaanza awamu ingine ya sita
Amechaguliwa na nani kuongoza hiyo awamu unayoita ya sita?.
 
... naona wanajaribu kumrudisha Samia "kwenye mstari" ili aweze kurithi mauchafu ya mtangulizi wake maana hata yeye (Samia) alikuwepo halafu jana akadai eti yeye "anaangushiwa jumba bovu" utadhani hakuwa sehemu ya serikali iliyopita! Sasa Polepole na genge lao wameamua kuchukua hatua; na hatua ya kwanza ni "kumrudisha kwenye mstari" kwamba hii bado ni Awamu ya Tano. Then mengine yatafuata.

Wameshtuka Mama anataka "kuchomoa kiaina" kuharibu legacy ya "kipenzi chao" and therefore hatma ya genge pia itakuwa shakani endapo Samia "atasimama na wananchi" kama alivyodai kwenye hotuba yake jana. Kauli ya Polepole si yake; bali yeye ni kipaza sauti tu; mtambo uko nyuma huko!
Acha umbea wewe Nani anamrudisha kwenye mstari!!? Yeye mwenyewe Alishasema kuwa Yeye na maghufuli nikitu kimoja na kwakuwa Yeye alikuwa nimakamo haipaswi ajitenge na awamu 5 jambo muhimu hapa Yeye apambane kwa akili ili ayamalize makundi yariyo ndani ya serikali yake
 
Mliomuona utotoni hebu tuambieni hakuwahi kuugua kwashiakor kweli huyu? Mbona akili yake imechoka haraka tena ghafla hivi?
1636118554444.jpg
mimi ninayo hii x-ray yake!
 
Ukweli mchungu, kaondoka Magufuli, makamu wake kachukua nafasi yake chama kilekile, sera zilezile. Polepole kasema ukweli
 
Ukweli mchungu, kaondoka Magufuli, makamu wake kachukua nafasi yake chama kilekile, sera zilezile. Polepole kasema ukweli
Ulikuwa una umri gani wakati Mzee Mwinyi anatolewa Zanzibar kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania?
 
Nilisoma Katiba sehemu inasema... Makamu wa Rais ataapishwa kumalizia muhula ulio Baki sidhani kama walisema kuanza Awamu Nyingine
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kwandikwa alitoa siri za nchi!yaani ule unyeti wa nchi ukawa nje!Jiwe alitaka abadili mihula ya utawala kuwa miaka saba hapo 2023 angeanza upya kutawala kwa katiba mpya kwa miaka 14 zaidi!!!!!Sina info hasa za ndani Bali naunganisha codes!!Inawezekana Kwandikwa alitoa siri kuhusu kifo cha jiwe au Alikosea kukubaliana na jiwe kuingiza Imbonerakure wa kirundi walioua sana kule Zanzibar!!!RAISI AJAYE KWANGU NI MWINYI JUNIOR BAADA YA MUHULA MOJA KULE ZENJIBAR!!NAUNGANISHA CODES TU MKUU!WASIJE KUNIDAKA KISA CODES ZANGU TU!MI BADO MDOGO!!
Codes zatosha mkuu.
 
Nilisoma Katiba sehemu inasema... Makamu wa Rais ataapishwa kumalizia muhula ulio Baki sidhani kama walisema kuanza Awamu Nyingine
Mimi nadhani hii awamu ni ya 5 na makamu akawa raisi ili amalizie muhula wake

ila kwasababu za kujipamba na kusifia ndo ikawa hvyo

kwaharakaharaka polepole anaonekana ana point.
 
Nawasalimu kwa jina la Tanzania

Polepole amenukuliwa akisema kuwa katika awamu ya Tano aloondoka ni mtu mmoja tu MAGUFULI , lkn serikali ni ileile ,chama ni kilekile

hivyo hakuna awamu ya sita ,Tusiwe tunachanganya.

SWALI?
Wataalam humu ndani naombeni nielemishwe "kwa hiyo anachosema POLEPOLE ni sahihi " kwamba hii serikali anayoongoza mama ni ya Awamu ya Tano na si ya Sita na tumhesabie awamu ya sita 2025?

Na je?

Ikitokea Mama asigombee awamu ya 2025 awamu ya tano itahesabika imetawala kwa miaka 10 ( vipindi vyote viwili)

Kwa unyenyekevu naomba kuelimishwa maana kipindi hiki Tunachanganywa sana jmn!!! kila mtu ana lake jambo tunashindwa kujua which is which.

karibuni !
View attachment 2033387
Polepole Yuko sahihi, hapa hakuna Cha Awamu ya SITA Wala Shangazi yake! hii ni Awamu ya 5B l, na uhakika angalia Baraza la mawaziri ni Lile Lile la awamu ya 5A, IGP ni Siro yule yule, CDF ni Mabeyo yuleyule, nk watendaji ni walewale, na majuzi kawarudisha hata walowahi kutemwa na JPM kwa mfano Januari Makamba, Makame Mbarawa, Ashatu Kijaji, Sofia Mjema, Ombeni Sefue nk! hii ni awamu ya 5B msidanganyike na hawa ndio wanamuangushia gari bovu Rais!
 
Nawasalimu kwa jina la Tanzania

Polepole amenukuliwa akisema kuwa katika awamu ya Tano aloondoka ni mtu mmoja tu MAGUFULI , lkn serikali ni ileile ,chama ni kilekile

hivyo hakuna awamu ya sita ,Tusiwe tunachanganya.

SWALI?
Wataalam humu ndani naombeni nielemishwe "kwa hiyo anachosema POLEPOLE ni sahihi " kwamba hii serikali anayoongoza mama ni ya Awamu ya Tano na si ya Sita na tumhesabie awamu ya sita 2025?

Na je?

Ikitokea Mama asigombee awamu ya 2025 awamu ya tano itahesabika imetawala kwa miaka 10 ( vipindi vyote viwili)

Kwa unyenyekevu naomba kuelimishwa maana kipindi hiki Tunachanganywa sana jmn!!! kila mtu ana lake jambo tunashindwa kujua which is which.

karibuni !
View attachment 2033387
Naona wanasiasi wanaanza kuziogopa namba witiri kwenye awamu. Hawataki ajaye aitwe awamu ya saba bali ndo awe awamu ya sita. Lakini wakumbuke hakuna awamu yenye marais wawili. Kama Polepole anataka iwe awamu ya tano asubiri mama akimaliza mhula wake amshawishi atakayekuja ajiite awamu ya sita.
 
Tuendelea kuomba uzima , tuone Tanzania itafikia wapi.
 
Polepole ana ng'ata na kupuliza ....Huyu anataka kuongea ukweli ila anasita ,(ataonekanaje na ccm)

ndo maana mnatumia nguvu kubwa kumwelewa

leo yuko mweupe ,kesho mweusi keshokutwa njano mkimfuatilia mtauumia vichwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom