Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Kagame alisema hata ongeza muda na alipo ulizwa mara kadhaa alisisitiza hataongeza muda, kuna yule babu Museveni mwaka 2006 alisema hatogombea tena lakini bado anang'ang'ania...
Wakati hao ndio role models wake. Why awe against nao?
Lazima nyayo zifuatwe. Hakna namna.
 
Hiyo clip ni ya zamani wala sio ya sasa. Hivyo sio mtu wa kumuamini bado.
 
Hiyo yote michezo imepangwa...muda si mrefu utaona wananchi waliopangwa wanaingia barabarani kuandamana wakitaka Magufuli aongezewe muda.
 
Magufuli hataongeza muda, na kasema hili mara nyingi.

Ameshagundua kwamba urais si kitu rahisi kama alivyofikiria awali. Anaombea miaka yake ipite astaafu...
Many times anavunja ahadi, many times anavunja katiba

Usiangalie kauli angalia matendo!
Ni sawa na demu, kwa kauli anakwambia sitaki lakini kwa vitendo anakupa signal kuwa go ahead.

Yeye atasema mimi binafsi sikutaka kuongeza muda, lakini nyie wabunge ndo mmeamua na mimi siwezi kuingilia mjadala wa bunge na maamuzi yake, case closed!
 
Magufuli hataongeza muda, na kasema hili mara nyingi.

Ameshagundua kwamba urais si kitu rahisi kama alivyofikiria awali. Anaombea miaka yake ipite astaafu...

Kabla ya uchaguzi wa Nov 2020 tulisema Magufuli sio mtu anayeheshimu box la kura, na huo uchaguzi utakuwa ni kupoteza muda kwani ameshapanga matokeo yaweje. Kuna watu kama ww walisema rais ameahidi kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki.

Mpaka akina Mbatia walikubali maneno yake na wakawa wanasema rais ameahidi uchaguzi utakuwa huru na haki, je maneno yake yalikuwa kweli kweli kilichofanyika kwenye uchaguzi huo mkuu? Tuna uzoefu na huyo jamaa sio mtu mkweli.

Kama wewe unamuamini hiyo ni haki yako, lakini ni mtu muongo.
 
Wapinzani kama wapo.....waache kuogopa hisia bali waanze maandalizi ya 2025....! Muda hauchelewi. Itafika muda chama tawala kimejiandaa kwa kuwa na candidate mwingine sahihi, upinzani hawaelewi waungane au wasiungane, hawajui nani awe mgombea, hawajui kauli mbinu ni ipi...? Ndio unafka wakati huyu anaimba ubwabwa,Huyu anasema Bata na huyu ananadi Bata Demokrasia....!!!

Hakuna mtu mwenye akili timamu atashiriki uchaguzi wowote Magufuli akiwa bado rais kwa katiba hii. Na kwa taarifa yako ccm haitegemei mgombea yoyote bora ili kutangazwa washindi, balo wanategemea vyombo vya dola tu. Njia pekee ya kuwatoa ccm madarakani ni machafuko, kwani box la kura ni kupoteza muda.
 
Juma Nkamia ni mstaafu

Ally Kessy ni mstaafu

Jah people ameishia darasa la pili

Musukuma ameishia darasa la saba

Babu Tale ameishia madrassa.

Hawa hawawezi kumshawishi Dr Magufuli aongeze mihula.

Maendeleo hayana vyama!
Tukienzi kiswahili
 
Ushauri wangu ni Kama humpendi JPM, jiandae kisaikolojia kuendelea kuwa naye kwa miaka mingine mingi. You will lose nothing if you are wrong.
 
Hivi vitu vinasukwa kitaalamu na mapropagandist mwanzo mhusika anasetiwa lazima akatae kijanja ili ionekane umejizuia ikashindikana watu wameng'ang'ana. Inaonesha watu hawajui utamu wa madaraka... kuachia huwa ningumu ushazoea kufaidi huku ukinyenyekewa nawatu wazima leo urudi kijijini umwachie raha mwenzio??!! Weeeh!! Subiri utajua hujui
 
Magufuli hataongeza muda, na kasema hili mara nyingi.

Ameshagundua kwamba urais si kitu rahisi kama alivyofikiria awali. Anaombea miaka yake ipite astaafu...
Wewe msaulifu sana kwanza alisema kazi ya urais ni ngumu miaka mitano inatosha, baadaye akachukua fomu peke yake akamwekea mizengwe Membe asigombee, kwenye kampeni akadai kwa nini tunamnyima miaka mitano tena, akasahau alishasema kazi ya urais ni ngumu na miaka mitan inatosha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom