Humphrey Polepole njoo umalize huu mchezo wa kitoto (Hoja za CAG, Zitto na Mbowe)

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,025
2,000
Humphrey Polepole mimi nakuambia ukweli kabisa kwamba unahitajika uwanjani kuja kumalizana na hoja za CAG, Zitto Kabwe na Freeman Mbowe.

Mbona mchezo huu kwako ni wakitoto tu na kwako unahitaji press conference moja tu ya dakika 45 kumzima CAG, Zitto na Mbowe.

Mbona kupindi cha Magufuli kulikuwa hakuna CAG yeyote aliyekuwa anakusumbua. Kipindi hicho ilikuwa CAG akiweka ugoko wewe unaweka jiwe. Lazima CAG avimbe.

Huyu Zitto na Mbowe kipindi cha Magufuli uliwamudu sana ilifikia hatua mpaka 'uliwanunua' madiwani wao na wabunge wao kwa bei chee sana. Sasa wameanza tena kufurukuta.

Mimi najua kwako hili ni suala dogo sana hebu piga press conference moja matata sana ambayo itatoa vumbivumbi hili lililotanda angani.

Au ni kweli haya ninayoyasikia kwamba wewe mwenyewe mguu nje mguu ndani?
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,926
2,000
Humphrey Polepole mimi nakuambia ukweli kabisa kwamba unahitajika uwanjani kuja kumalizana na hoja za CAG, Zitto Kabwe na Freeman Mbowe.

Mbona mchezo huu kwako ni wakitoto tu na kwako unahitaji press conference moja tu ya dakika 45 kumzima CAG,Zitto na Mbowe.

Mbona kupindi cha mwendazake kulikuwa hakuna CAG yeyote aliyekuwa anakusumbua. Kipindi hicho ilikuwa CAG akiweka ugoko wewe unaweka jiwe. Lazima CAG avimbe.

Huyu Zitto na Mbowe kipindi cha Mwendazake uliwamudu sana ilifikia hatua mpaka uliwanunua madiwani wao na wabunge wao kwa bei chee sana. Sasa wameanza tena kufurukuta.

Mimi najua kwako hili ni suala dogo sana ebu piga press conference moja matata sana ambayo itatoa vumbivumbi hili lililotanda angani.

Au ni kweli haya ninayoyasikia kwamba wewe mwenyewe mguu nje mguu ndani?

Uzi ndiyo huo.
Hivi Polepole bado anatembelea V80 ...... !!
 

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
1,946
2,000
mimi nimemiss zile mbwembwe zake za kupiga hesabu za kujumlisha na kutoa kuhusu matumizi ya trilioni 1.5.

giphy.gif
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,809
2,000
Mzee Polepole atakuja kutuambia nini??? Kwa elimu gani ya "Economics/Mathematics/Auditing/Tax Administration" aliokua nayo ya kumzidi CAG???

Unafikiri, hayo mahesabu na uchambuzi wa matumizi ya serikali aliotoa CAG ni sawa sawa na kuhesabu vitumbua au visheti??? Au kuhesabu buku mbili mbili za wajumbe wa CCM walioingia kwenye vikao huko chamwino???

● Mzee Polepole atawadanganya nyinyi maboya wa lumumba, kwasababu mmeshazoea kudanganywa na kuishi kwa posho za buku mbili.

● Mzee Polepole ameshakufa kisiasa kama alivyokufa baba yake Mzee Bashiru Ally Kakurwa na Mzee Kigwangalla. Ila MATAGA bado hamjalijua hilo. Subirini mtaona kama 2025 watarudi bungeni au serikalini hao wadudu.

● Mzee Polepole muda si mrefu, nyaraka zinawekwa wazi mbele ya "raia wenye hasira kali" za hela alizopiga kwenye uchaguzi, kushawishi na kusababisha matumizi ya hela za uchaguzi kwenda juu zaidi ya budget ya uchaguzi 2020 iliowekwa.

● Mzee Polepole ajipange 2025, harudi bungeni si kwa kupitia mlango wa kina mama (Viti Maalum) wala kuchaguliwa na wananchi. Hapo wakati Ukatibu Mwenezi utakuwa umeshachukuliwa na mtu mwingine CCM.

● Mzee Polepole & SUKUMA GANG (Wasio na Experience yoyote ya Siasa Chafu = Waliotembelea koti la Marehemu Kichaa) wanauliwa wote kisiasa hata kabla ya 2025, watauliwa na (#Team JK, #Team KINANA, #Team NAPE/JANUARY = CCM YA ZAMANI ILIORUDI MADARAKANI NDANI YA CHAMA).
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,024
2,000
Unajua wengi wa hawa wanasiasa wa Magufuli wanashindwa kumtetea na moja ya sababu kubwa ni kuwa ni Kikwete hasa ndiye aliyewaibua huko vichochoroni walipokuwa.

Kwa hiyo hata kama Magufuli aliwapa nyadhfa mbalimbali na kwa kweli wana mengi ya kumshukuru ila bado watamtii sana Kikwete na watafuata lolote atakalowaambia.
 

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,025
2,000
Unajua wengi wa hawa wanasiasa wa Magufuli wanashindwa kumtetea na moja ya sababu kubwa ni kuwa ni Kikwete hasa ndiye aliyewaibua huko vichochoroni walipokuwa.

Kwa hiyo hata kama Magufuli aliwapa nyadhfa mbalimbali na kwa kweli wana mengi ya kumshukuru ila bado watamtii sana Kikwete na watafuata lolote atakalowaambia.
Kama kuna hoja ya msingi vile.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,047
2,000
Pole pole alikuwa na akili nzuri sana kabla hajahamia huko alipo, yule Polepole aliekuwa anaichambua ile rasimu ya Warioba sijui alienda wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom