Humphrey Polepole nenda polepole, CCM ni kubwa haizoeleki na haijawahi kumwacha mtu salama

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
pic%2Bccm.jpg


Kwanza kabisa mm sipo kwenye chama chochote cha siasa ila ni mkereketwa wa siasa za Tanzania.

CCM ina wanachama wengi sana ndani na nje ya nchi na n chama kikongwe sana.CCM kilikuwa na watu lakini leo hii wako wapi? Walikuwepo watu bhana..sasa je?

Ndugu yangu Polepole nenda polepole. Watakuacha njiani.Watakukana wenzio. Siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.CCM siyo mama yako wala baba yako.Haieleweki.


Ona hizi kauli zako:-

“Ukienda kwenye kanuni za uchaguzi za 2017 fungu la 25: Nafasi ya uongozi ni kazi ya muda wote (inazitaja hapo), Mkutano Mkuu wa Taifa haujatajwa, lakini mkuu wa wilaya ni kiongozi wetu wa Serikali pia ni kiongozi wetu wa chama,” alisema Polepole na kuongeza:

Mkuu wa wilaya ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ni mjumbe wa halmashauri kuu ya wilaya na ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya. Huyu pia ni kamisaa wa Serikali, ‘public officer’ anayefanya kazi zote za chama. Sasa nikasema hekima pale ituongoze, yaani mtu ujiongeze mwenyewe.”

Aliendelea kusema: “Kama wewe una dhamana zote hizi, kwa nini mkutano mkuu tusimwachie mwanachama mwingine asiye na dhama nyingine yeye ashiriki kwenye mkutano wa chama?”

Polepole aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara na baadaye Ubungo jijini Dar es Salaam alisema kwa sasa kuna wakuu wa wilaya wapatao 166 na kama wote wataomba nafasi hizo, watafurika kwenye nafasi za chama hicho.

“Kama wakuu wa wilaya wote watachukua kwa pamoja wako 166, zamani mkutano mkuu tulikuwa 2400 sasa hivi tumepunguza idadi tumekuwa 1,700, hao ni wanachama walioomba dhamana halafu kati ya hao 166 ni wakuu wa wilaya,” alisema Polepole na kuongeza:

“Upande wa pili ni hekima ya kuwa na kiasi. Wewe una nafasi kadhaa, hizi nafasi nyingine tumwachie mtu mwingine. Hiyo inakuja kutokana na maelekezo yetu kwenye fungu la 22 kwamba; mtu mmoja kofia moja. Ukiwa kiongozi una dhamana tayari basi hii nyingine waachie wengine nao waweke mawazo yao katika kupeleka mbele chama chetu.


Utapotea ndugu.
 
Sasa kwa nini anakataa hekima isitumike Mkuu wa wilaya kuwa mtu asiye na chama kabisa? Haoni kuwa kuwa na vyeo vingi husababisha mgongano wa maslahi kwa kiwango kikubwa?
 
Polepole analeta mapinduzi ndani ya chama,lakini mjadala haujafungwa ni mapendekezo sijui yake mwenyewe au mwenyekiti wake?
 
Mwenyekiti anasafisha wanamtandao wote (team Kikwete, team Membe, team Lowasa, team Mwigulu, team Makamba, n.k). Anataka kujaza team Chatou.
 
Pengine mtoa mada ni gwiji la fasihi maana sijaelewa tatizo ni nini hadi polepole aachwe, kwa jinsi nilivyosoma naona polepole ameongea point za maana sana, au ndio tuseme wakuu wa wilaya ni "vijana" wa "mwenyekiti" hivyo ndugu polepole akianza kuwawekea vikwazo basi na yeye hatakua salama kutoka kwa "mwenyekiti"??
 
Huyo ni mchumia tumbo aliyepoteza thamani alivyoachana na katiba ya wananchi !!

Mungu amlipizie
 
Bwana polepole tambua kuwa kuwa ule msemo usemao kuwa 'hata shetani akizeeka huwa malaika' ni gilba tu haiwezekani mkuu. shetani ni shetani tu na kamwe hawezi kuacha itikadi zake!
 
Back
Top Bottom