Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,483
- 51,057
Ndugu Polepole
Ulishiriki mchakato wa kutafuta katiba mpya, Chini ya uongozi wa Genius Jaji Warioba ulizunguuka nchi nzima kutafuta maoni ya wananchi, kuyachakata na hatimaye kutuletea rasimu bora kabisa ya katiba al-maarufu rasimu ya Jaji Warioba.
Na baada ya kuiandaa rasimu hiyo, ulizunguuka kuielezea na kuifundisha kwa wananchi, na kwa kweli wananchi walikupokea vizuri, walikupenda sana kwa jinsi ulivyokuwa ukidadavua issues zao nyingi njema kabisa katika katiba hiyo.
Ulizungumza uwezeshaji wa wanawake katika vyombo vya maamuzi kwa mujibu wa rasimu hiyo - Wanawake walifurahishwa sana
Ulizungumza uwezeshaji wa wananchi katika kuwa na nguvu zaidi za kuwaweka viongozi wao madarakani, kwa mfano rasimu ilitaka teuzi za rais kama vile mawaziri zithibitishwe na bunge.
Ulizungumzia jinsi muundo wa sasa wa muungano unavyoibana Zanzibar na ukaelezea jinsi vyombo mbalimbali vya serikali wakiwemo makatibu wakuu kupitia kamati yao, ofisi ya waziri mkuu, ofisi ya makamu wa raisi jinsi wanavyotaka muundo wa serikali tatu au unaoshabihiana na serikali tatu.
Sasa Ndugu Polepole, Wananchi wa Tanzania wanataka katiba mpya, na kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa katiba mpya ni CCM, na kinara wa vikwazo vya katiba mpya ni rais Magufuli.
Kwa hiyo basi wewe ndugu Polepole, kitendo cha kuendelea kuwa ndani ya CCM isiyotaka katiba mpya yenye mzizi mkuu kwenye rasimu ya warioba na kitendo cha kuendelea kumsapoti rais Magufuli aliyegoma katakata kutupa katiba mpya japo ilikuwemo kwenye ilani ya uchsguzi ya CCM ya mwaka 2015 maana yake unashiriki dhambi ya kuwanyima wananchi katiba mpya wanayoitaka.
Ndugu Polepole ulizunguuka nchi nzima kuwaeleza wananchi hatari ya madaraka makubwa ya rais, ukafikia hatua ukasema rais ana madaraka ya kuwapoteza watu wote waliomo ukumbini, (wale waliokuwa wanakusikiliza) na asifanywe kitu!.
Sasa ndugu Polepole, kama hilo unalitambua kwa nini uko kwenye Chama na unamnadi mtu ambaye hataki katiba mpya ili aendelee kutawala kwa kutumia katiba mbaya ambayo ni hatari kwa ustawi na mustakbali wa Taifa hili?
Ndugu Polepole mbona ulishiriki kutungisha mimba ya katiba mpya na baada ya mimba kutunga unakuwa msitari wa mbele kumtaka Mama Tanzania aitoe hiyo mimba?
Ndugu Polepole kama unaamini watanzania wanataka mabadiriko na kama unaamini kuwa katiba mpya ni chachu kuu ya mabadiriko ya kweli basi toka huko CCM uje uungane na upinzani ili tuweze kurudisha rasimu ya katiba mpya ya Genius Jaji Warioba
Hapa chini ni video yako ukielezea hatari za madaraka makubwa ya rais kwa mujibu wa katiba hii ya sasa ya kidikteta iliyopitwa na wakati