VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Hili ni ombi-amri. Ni kwa maslahi mapana ya chama chetu na hata Serikali iliyoundwa na chama chetu cha Mapinduzi. Katika kuonesha kuwa CCM na Serikali ya awamu hii ya tano zimemiliki kila idara ya 'mechi' hii ya kisiasa Tanzania, ni vyema jambo hili likafanyika.
Nakuomba na kukuagiza kufikisha ujumbe huu kwa wahusika wa kiserikali na kichama. Umefika wakati wa kuwa na BUNGE LIVE. Kuanzia tarehe 31 mwezi huu, Bunge litaanza vikao vyake Dodoma. Ni wakati wa kuruhusu BUNGE LIVE.
Tunataka kuwaona Mawaziri wetu wakijibu majibu mujarabu bila tabu. Tunataka kuwaona Wabunge wetu wakijenga hoja za haja na za kuleta faraja. BUNGE LIVE litarudisha ari ya Wabunge wetu ambayo imeporomoka vya kutosha na kutisha.
BUNGE LIVE litatupa 'ujiko' CCM na kusahaulisha katazo la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini. BUNGE LIVE litatuonesha wanaCCM jinsi tunavyojua mambo na siasa. Bunge ni uwanja mkubwa zaidi wa kisiasa. Tuutumie kwa kuonesha BUNGE LIVE.
Mwafaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)