Humphrey Polepole azungumzia hali ya kisiasa nchini; viongozi zaidi ya 20 kuhamia CCM Januari 18

Hahahaa........ nakuona tetty ulivyotetemeka laigwanan kutimba mjengoni!

Hahahhahahahahahah nani ni Lwaigwan rafiki??Huyu mlimuita Baba la Mafisadi au mwingine??Pole jamaa yangu siku Half Ray akisema Lissu anatinga Lumumba ndiyo itaniuma mpaka basi lakini huyo MwanaCCM kindakindaki,sijawahi kumuamini na sitokaa nimuamini mpaka naingia kaburini pole sana.
 
Miaka mitano mtamaliza bado mnanunua watu 2020 ikifika mliowanunua wanarudi walikotoka sasa hamuoni kama ni upumbavu.
Acha wazungu waendelee kututukana
Nchi zilizoendelea husikii upuuzi huu. Kama kuna mapungufu ndani ya chama wanakabiliana wao kwa wao huku shitholes countries watu wanahama chama kama si kupoteza pesa za walipa kodi
 
Karibu tufuatilie, kipindi ni Msema kweli na mtangazaji Albert Kilala! Up dates: Mwenezi anasema vyama vya Upinzani havina itikadi wala sera.

Pili anasisitiza CCM kwa sasa ina takribani wanachama milioni 12.

Tatu kuna wabunge na madiwani wslioomba kwa barua kujiunga na CCM lakini wamewakataa kwa sababu ni mizigo.

Nne viongozi maarufu zaidi ya 20 wa Chadema kutoka mikoani na taifani watahamia CCM tarehe 18/01/2018 na amesita kidogo kuthibitisha kwamba miongoni mwao mzee Lowassa yumo lakini mtazamo wa sura yake umeonyesha huenda akawemo!

Chanzo: Channel ten


Nape alishauri vizuri sama kuhusu hili suala
 
Lumumba hamnazo akili! Magu na Polepole akili zao zimefyatuka na ni waongo.Majuzi ndo wakatuaminisha kuwa watampokea kiongozi mkubwa kutoka Ukawa.
 
Achukue wabunge ns madiwani tume ya uchaguzi wapate mkwanja na tuache kulipa madeni kwanza
 
Wapinzani nawashauri waende wengi huko ccm,wakifika huko waungane watengeneze upinzani imara wakiwa hukohuko ccm
 
Mbona tunaongelea viongozi tu na sio wanachama.viongozi hao wanachama mbona hatuoni impact yao kwenye society.Nafikiri niwakati wa kukaa na kutafakari vizuri kwa nini tunafanya promo kubwa kwa hao viongozi.kwa nini tunawapa uzito mkubwa bila sababu.kuna siku hao hao watarudi huko wanakotoka hivi tutafanya promo.naomba wajiunge kama wanachama wengine tu tusiwape umuhimu mkubwa
 
wakijiunga so what??? uchumi unakuwa na umaskini miongoni mwa watanzania unapungua? Je kila mtanzania ana uhakika na mlo walau mmoja kwa siku?
 
Back
Top Bottom