Humphrey Polepole anafanya siasa katika nafasi yake. Ndiyo kazi aliyoteuliwa bila kujali madhara kwa pande mbili! Wapo wa kujitafakari

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Humphrey Polepole anafanya kile anachoamini kuwa ndiyo kazi anayotakiwa kuifanya ili aendelee kubaki mjini. Amepewa malengo, yeye anaangalia hilo! Hajali madhara kwani hayamhusu katika nafasi yake hiyo. Kazi ni kwa hizi pande mbili kung'amua chaka wanaloingizwa na Humphrey Polepole!

Niwahakikishie kuwa baada ya jana Polepole kufanikiwa kumvua mpinzani ubunge alienda nyumbani kwake akiwa ni mwenye furaha sana! Kama ni mlevi basi jana kazitandika kwelikweli! Ameweza kumvua mtu ubunge. Kwa maana nyingine ameweza kupunguza idadi ya wabunge wa upinzani kwa sasa! Yajayo kwake yeye hayamhusu maana siyo kazi yake. Lazima watu tuelewe ni nini hasa kazi ya Polepole.

Leo akifanikiwa hata kumvua Mbowe ubunge atafurahi sana ingawa kwa sasa anamuita kila jina baya kwa uongozi wake ndani ya Chadema. Utashangaa sana siku imetokea ndoto kisha Polepole akakaa na Mbowe kumpokea CCM atakavyompamba kwa kila jema na atasema CCM imelamba dume! Hiyo ndiyo kazi ya Polepole!

Sasa lipo tatizo ambalo lazima pande mbili za kulia na kushoto kwa Polepole zinatakiwa kuliangalia sana!

1. Upande wa kushoto
Huu ni upande wa yule anayehama mfano Mwita Mwikabe.
Unaposhawishiwa kuhama kwanza lazima utafakari sana tena sana. Je huyu anayenishawishi kuhama ana agenda gani? Ana nia gani kwangu? Sasa mtu unahama kisha unasema eti nimehama kwa sababu sina nafasi ya kugombea uenyekiti. Je huko unakoenda utapata hiyo nafasi? Ukishawaza hilo angalia sana yule aliyekushawishi kujidanganya hivyo, anafanya hivyo kwa sababu gani? Sasa unakuja kugundua kuwa yeye yule pale yupo kazini. Anajitahidi hata kutumia hila kuifanikisha kazi yake "Kazi ya ujanja ujanja" na kudanganya! Kwanini hujiulizi kuwa hakuna sababu ya kuacha ubunge kisha ukaenda tena kugombea ubunge huohuo? Kisa ni nini? Unagundua kuwa UMEDANGANYWA! Umedanganywa ukadanganyika. Na kudanganywa huko kisha ukaingia kingi tayari umemuongezea credit yule aliyekudanganya maana ndiyo kazi yake! Ukiingia kwenye vikao vya hicho chama ulichodanganywa kuhamia utaona yule aliyekudanganya anasifiwa kuwa aliweza kutumia uongo ulio wazi kumvua mtu ubunge! Atapata sifa kupitia upumbavu wako na wewe uko palepale ukijishuhudia namna ulivyo mpumbavu.

2. Upande wa kulia
Huu ni upande ambao utalazimika kuingia gharama za kipumbavu kwa kuwa umekubaliana na upumbavu wa mtu mjinga ambaye ndiyo kazi yake anayofanya bila hata kufikiri. Tutaitisha uchaguzi mdogo tutatumia fedha za walipa kodi huku watu hawa wakiwa hawana msaada wowote wa zaidi kwetu! Hawatoongeza chochote kwetu zaidi ya idadi tu. Tuanalazimika kuinamisha vichwa chini kutokana na haya! Haya ya kukwepa kuutazama ukweli halisi! Hivi waliohama kisha wakatuletea gharama kubwa za uchaguzi mdogo kama serikali mpaka sasa wametuletea jipya gani? Wametuongezea thamani gani? Mtulia na Godwin wameonyesha thamani gani ya sisi serikali ya CCM kulazimika kurudia uchaguzi kwa ajili yao! Bungeni? Serikalini? Kwenye chama? kwenye jamii? wana thamani gani ya kipekee?
Mwita Mwikabe hata tukirudia uchaguzi kisha Akashinda, sisi kama CCM atatuletea nini? sisi wana CCM tutafaidika nini na yeye kuja kwetu kwa dharura?

Ataleta thamani gani inayotufanya sisi serikali kuingia gharama za kumrudisha yeye bungeni baada ya mtu mmoja kumshawishi kuutupa huo huo ubunge?
Tukija kufikiria hayo tutaona ni swala la idadi tu ambayo kwetu wala haina maana wala thamani kwa sasa! Haina athari yoyote kwa sasa!

Niwashauri upinzani wasisusie uchaguzi! Waingie ili serikali hii iliyojaa watu wasiojielewa iendelee kugharamika kwa ujinga wao wa "kumuintateini" mjinga mmoja asiyejielewa! Tunafanya hivyo kwakuwa tunalea siasa za kijinga ndani ya awamu hii ya tano!
Bado narudia msemo wangu ule kwamba "Huenda kama taifa tumempata mtu asiyeendana na wenzake ndani ya dunia iliyostaarabika na ndiyo maana anawakwepa kwepa" Lazima tujitafakari sana kuhusu hilo.
 
Pole pole anafanya kazi ya mungu ya kuwatoa kwenye laana na kuwapeleka kwenye baraka.
 
Povu la nini mbn hujazungumzia akina lazaro??? Hujamtaja hapo mpumbavu ni nani??? Au tatzo mtu wenu akitoka kwenu kuja kwao inakuwa tatzo??? Ndo unatambua kwamba cdm akienda CCM hela za mlipa kodi zinapotea????
 
Maelezo marefu lakini mwisho wa siku kuondoka kwa Mwita Waitara kumeleta simanzi CDM.
 
Povu la nini mbn hujazungumzia akina lazaro??? Hujamtaja hapo mpumbavu ni nani??? Au tatzo mtu wenu akitoka kwenu kuja kwao inakuwa tatzo??? Ndo unatambua kwamba cdm akienda CCM hela za mlipa kodi zinapotea????
Nimekuelezea jinsi mnavyoendeshwa na kichwa kidogo cha Polepole!
 
ambao utalazimika kuingia gharama za kipumbavu kwa kuwa umekubaliana na upumbavu wa mtu mjinga ambaye ndiyo kazi yake anayofanya bila hata kufikiri.
Unaonekana kuumia ila jitahidi kujidhibiti. Usitukane.
Niwashauri upinzani wasisusie uchaguzi! Waingie ili serikali hii iliyojaa watu wasiojielewa iendelee kugharamika kwa ujinga wao wa "kumuintateini" mjinga mmoja asiyejielewa! Tunafanya hivyo kwakuwa tunalea siasa za kijinga ndani ya awamu hii ya tano!
Mjinga ni yule aliyenyang'nywa jimbo siyo aliyepata. Pesa za kuendesha uchaguzi ziko kwenye bajeti na ndio gharama ya kujenga demokrasia. Usilie pambana.
 
Unaonekana kuumia ila jitahidi kujidhibiti. Usitukane.

Mjinga ni yule aliyenyang'nywa jimbo siyo aliyepata. Pesa za kuendesha uchaguzi ziko kwenye bajeti na ndio gharama ya kujenga demokrasia. Usilie pambana.
Kwenye uzi wangu nimetaja wajinga wanne akiwemo huyo aliyejivua ubunge! Soma kwa makini.
 
Back
Top Bottom