Humphrey Polepole ahubiri kuwa 2042 ndiyo mwisho wa Dunia na kurudi Yesu mara ya pili

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Katibu Mwenezi wa CCM, Hamfrey Polepole amesema mwisho wa dunia ni mwaka 2042. Akizungumza katika kipindi cha Sunday Worship cha WasafiTV amesema Yesu atarudi mwaka 2035 kulichukua kanisa (wateule wake) na kukaa nao mawinguni kwa miaka 7 hadi mwaka 2042 atakaposhuka kuihukumu dunia.

Lakini katika kipindi cha miaka 7 (2035-2042) kutakua na dhiki kuu duniani ambapo nzige wenye vichwa vya simba na mikia ya nge watawatesa waliobaki duniani. Ndicho kipindi ambacho Mpinga Kristo atajiinua na chapa yake ya 666 na kuiteka dunia.

Alipoulizwa mbona Yesu mwenyewe alisema hakuna ajuaye siku wala saa isipokua Mungu mwenyewe (Marko 13:32) amesema ninkweli siku na saa havijulikani lakini majira na mwaka wa Yesu kurudi vinajulikana.

FB_IMG_1612339454755.jpg


Nini maoni yako?
 
Hamjamwelewa huyu babu,

Ufafanuzi
Atakula bata mpaka 2035 alafu ataanza kuugua kwa muda wa miaka 7. Then ikifika 2042 anakata kamba.

Mwisho wake anataka kusema ndio mwisho wa wote
 
Tuachane na la polepole wasafi tv si imefungiwa sasa wasafi gani tena?
 
Tuliwaambieni wengine baada ya Oktoba 28 mngepatwa na recurring stress syndrome, haya sasa! JPM juu! Polepole juu! Sisiemu hoyeeee! #Miatano Tena!!!
 
Back
Top Bottom