Humphrey Polepole aeleza mikakati yake baada ya kukabidhiwa ofisi na Nape Nnauye

DOFFA

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
425
233
1.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.



Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na Katibu anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.



Polepole alisema kwa misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tetea wanyonge hivyo katika muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama katika misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.



“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.



Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.



Polepole alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye; anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine.



Wakati huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.
HONGERENI VIJANA KWA KAZI NZURI.NAMKUMBUKA SANA POLEPOLE WAKATI WA BUNGE LA KATIBA;NI JEMBE LENYE MPINI WA MPINGO.
 
Pole Pole kajiziba mdomo mwenyewe. Zile mbwembwe zote siku hizi hana. Ilifika kipindi karibia kila wiki ana kipindi cha Kuzungumza Channel Ten alafu lazima ukute bandiko lake humu,kumbe yote hayo ilikua ni NJAA tu.

LepoLepo ni Mnafki sana,alikua anapinga sana uwepo wa wakuu wa Wilaya akidai kuwa hawana faida kwa Taifa lakini alipoteuliwa tu hakudiriki hata kunyanyua mdomo

Ila angalau hata huyu ambaye hoja zake zinafikirisha kidogo kuliko yule konda wa Daladala ambaye yeye ni Kuropoka tu na kutafuta attention ya Abiria na mzee mwenye gari.
 
Huenda akawashawishi wenzake kukubali muundo wa serikali tatu maana huyu jamaa ni muumini mzuri wa Serikali ya Tanganyika,Zanzibar na Tanzania.
 
Back
Top Bottom