Hukuwa chaguo lake la kwanza ndo maana haachi kuchepuka

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,313
1,363
Dunia ya mapenzi imejaa confusion

Unayempenda anakuona sio hadhi yake na usiyempenda ndo anakubana Kama lulu.

Unaweza kujitapa katika uzi huu ila niukweli usiopingika mpenzi uliyenaye hata Kama anajifanya anakupenda kiukweli wewe hukuwa his /her first choice kwake ila aliposhindwa kupata alichokitaka ndo akaamua kukubali matokeo akawa wako.

Kila couple unayoifahamu kuna mmoja alicompromize viwango vyake ili muwe wote.

Wewe hushangai kwa mambo yote unayofanya ili mwenza alizike ila kila unavyojitahidi mwenzio haonyeshi hata kutikisika na kuelewa mziki unaouimba

Usijihukumu sana, ukweli haukuwa chaguo lake la Kwanza ila ni destiny tu ndo ziliwaweka pamoja.

Usijichukie mwenza anapochepuka, tambua tu huna kile alichokua anakitafuta cha kumtuliza tuliiii kwenye mahusiano. Ndo maana anakitafuta huko nje.

Usilie, maisha ndo yalivyo

Tunapata tulivyojaliwa na sio tunavyovitaka.

Regards

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom