Hukumu yaitikisa Zantel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu yaitikisa Zantel

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 15, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zanzibar Telecom Limited (Zantel), imetikiswa na pigo la kisheria baada ya kukumbana na hukumu ya kutakiwa kumlipa mfanyabiashara wa Dar es Salaam mamilioni ya shilingi.

  Katika kesi Namba ya 305 ya mwaka 2007, Zantel ilishitakiwa na mfanyabiashara Haidari Y. Rashidi wa Kampuni ya Nararisa Enterprises ikitakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 53.4 kutokana na kusitisha mkataba wake wa kuiuzia viyoyozi kampuni hiyo ya simu.

  Hata hivyo, baada ya mvutano wa kisheria katika mahakama nchini, iliamriwa kuwa Zantel inapaswa kumlipa Haidari zaidi ya Sh milioni 800, badala ya maombi ya mshitaki ya Sh milioni 53.

  Gazeti hili limefanikiwa kupata nyaraka za mwenendo wa kesi hiyo ambayo hukumu yake inaelezwa kuwa imeuchanganya uongozi wa Zantel na mawakili wake kutokana na kile kinachoonekana ‘kupaishwa’ kwa malipo hayo kwa zaidi ya mara 15 ya fidia iliyokuwa imeombwa na mdai.

  Hukumu iliyompa ushindi Haidari ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema.

  Uamuzi huo unaelezwa kuunyima usingizi uongozi wa Zantel ambayo hata hivyo iliamua kulipa deni kwa kile kinachotajwa kuwa ni kuheshimu uamuzi wa mahakama, ingawa kuanzia hapo uongozi wa kampuni hiyo ya simu umeelezwa kuwa unahaha kutaka kutenguliwa kwa hukumu husika.

  Baadhi ya watendaji wakuu wa Zantel na mawakili, wanailalamikia hukumu hiyo wakidai kuwa kiasi cha fedha ilichoamriwa kulipa ni kikubwa mno pengine kushinda uwezo halisi wa mahakama iliyotoa hukumu.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Norman Moyo alielezea kutoridhishwa na hukumu hiyo, akidai ni kubwa na yenye maumivu kama mwekezaji.

  “Imetushangaza hata sisi, tunatafakari cha kufanya, lakini kimsingi tunadhani ni hukumu yenye utata. Tumelipa fidia hiyo kubwa kwa sababu ya kuiheshimu mahakama, lakini hatujatendewa haki na hatudhani kama hali hii inaleta picha nzuri kwa mazingira ya uwekezaji…tunatafuta jinsi ya kupata haki yetu,” alisema Moyo.

  Historia ya kesi hiyo inaonesha kuwa Juni 27, 2007, Haidari kupitia kampuni yake ya Nararisa aliingia mkataba na Zantel wa kuiuzia viyoyozi 36 vya thamani ya Sh 73,296,000, lakini hadi kufikia Agosti 3, mwaka huo, siku ya mwisho ya mkataba, nusu ya viyoyozi hivyo vilikuwa havijapelekwa Zantel.

  Kutokana na kushindwa kulipwa fedha kama yalivyokuwa makubaliano ya mkataba, Haidari alilazimika kukimbilia mahakamani kutaka alipwe Sh milioni 53.4 zilizokuwa zimebaki, huku akidai kwamba ili kuipatia Zantel viyoyozi, alilazimika kuomba mkopo wa Sh milioni 48 kutoka Benki ya Eurafrican Bank ambao ulikuwa unaendelea kukua kutokana na kucheleweshewa malipo na hata kufikia deni la Sh milioni 252.

  Lakini madai hayo yalipingwa na Zantel iliyosisitiza kutohusika na suala hilo kwa kuwa mdai alishakiuka masharti ya zabuni, kwa kushindwa kukamilisha ndani ya wakati idadi ya viyoyozi vilivyohitajika.

  Zantel kupitia kwa wakili wake, Juvenalis Ngowi wa Kampuni ya East African Law Chambers, ilipinga madai hayo kwa maelezo kwamba, hayakuwa na msingi na yaliyojaa utata kutokana na mlalamikaji mwenyewe kushindwa masharti ya mkataba.

  Msingi mkuu wa kilio cha Zantel ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni miongoni mwa wanahisa, ni hisia za uonevu wa kutakiwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na kile kilichokuwa kimeombwa na mdai.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  waliarandwe lema ni miongngoni mwa mahakimu majuha kabisa hapa bongo na ana tuhuma za rushwa mara kwa mara
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Case Closed
   
 4. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  AHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA thithiemuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu:bump:
   
 5. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #5
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hizi propaganda ziko one side, kwa anayetaka kujua ishu ilivyo akachukue hukumu asome mambo yalivyokuwa na ni kwanini mahaka iliamuru walipe 800M, hii inainclude Riba ya mkopo wa benki, pesa za kampuni husika pamoja na riba na gharama za case, kwa taarifa tu hii kesi ilifunguliwa 2006 na kuisha 2010 kwa hiyo unaweza ona jinsi riba ilivyopanda kutokana na muda mrefu wa case.
   
 6. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  800M ni kitu gani kwa kampuni za simu?
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ni sawa na sifuri.
   
Loading...