Hukumu ya Siku ya Mwisho kwa Mfanyakazi wa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya Siku ya Mwisho kwa Mfanyakazi wa Serikali

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Juma. W, Mar 28, 2011.

 1. J

  Juma. W Senior Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  p { margin-bottom: 0.08in; } Hukumu ya Siku ya Mwisho kwa Mfanyakazi wa Serikali


  Jamaa moja alijiriwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania kama Mtunza kumbukumbu katika Wizara fulani. Aliipenda sana kazi yake hasa miaka mitano ya mwanzo ya utumishi wake katika idara yake. Alifanya kazi yake kwa bidii na aliyafahamu mafaili yote katika masijala yake. Watu walifurahi kila siku walipomkuta akiwa zamu, walijua watahudumiwa mara.


  Kadri siku zilivyoenda, majukumu ya kijamii yule bwana yaliongezeka; taratibu huyu bwana akaanza kuisahau kazi yake ambayo ni chanzo kikuu cha mapato yake. Alianza kuchelewa sana kazini na kuondoka kabla ya muda uliopangwa. Akiwa kazini alijishughulisha na mambo mengine ambayo hayahusiani na kazi yake. Kwa kweli huyu bwana alibadilika sana.


  Utendaji wa kazi ulibadilika kutokana na majukumu yake ya kijamii. Alikuwa na familia ya mke na watoto wa wawili, alikuwa kiongozi wa mtaa wake alioishi, alikuwa pia kiongozi katika kanisa lake. Badae ilifahamika kuwa huyu bwana alianza biashara ya saluni za kiume ambazo alilazimika kuzisimamia ili aweza kujiongezea kipato. Ni muhumu sana kwa mfanyakazi wa serikali hasa kwa muda kama wa leo ambao mfumuko wa bei ni mkubwa sana na mishahara ni midogo kuwa na angalau chanzo mubadala cha mapato, la sivyo utaua familia.


  Maisha yalienda na kuendelea. Yule bwana akaanza kufika kazini saa nne. Visingizio vingi sana, mara mtaani pale wezi walimwibia jirani kuku; mara mama mchungaji kasema; mara tulikuwa na kikao cha makada wa chama; nilikatiwa umeme kwenye saluni nikapitia TANESCO. Kwa kweli sababu zilikuwa zinatolewa kila huyu bwana akichelewa.


  Tatizo lilikuwa siyo kuchelewa ila ni kuchelewa kila siku. Lakini tatizo likawa ni kutoa sababu za kuwahi kuondoka, na wakati mwingine kutoroka. Tabia ambazo zilizorotesha sana utendaji wa idara yake na kuathiri maisha ya watu wengi ambao walileta barua zao pale wizarani. Lakini wapo waliotaka taarifa fulani fulani kwaajili ya mipango na maendeleo ya wizara na taifa kwa ujumla. Nao walizipata hizo nyaraka kwa taabu sana kwani huyu mfanyakazi bora wa zamani yuko buzy na "social affairs/family problems n.k". Utendaji ulipungua sana. Mchango wa idara katika maendeleo ya wizara ukawa ni hasi na mchango wa ile wizara katika maendeleo ya taifa ulishuka sana.


  Huyu bwana aliendelea na tabia yake hiyo kwa miaka mingi sana. Kijamii huyu bwana alikuwa "excellent" kwani kanisani alikuwa mzee wa kanisa, kwenye chama chake alikuwa kada mzuri na pale mtaani alipoishi alikuwa anaheshimika sana. Kiujumla hata ukimwona huyu bwana utamtambua kuwa ni mtu mwenye "personality" kubwa. Kumbe utendaji wake kazini kwake ulikuwa ni ubabaishaji mtu.


  Huyu bwana alikuwa mwizi. Aliiba MUDA. Madhara ya WIZI wake yalikuwa makubwa kuliko ya ule wizi uliotokea siku ile alipolazimika kuchelwa kazini kumfuatilia mwizi wa mboga kwenye bustani ya jirani. Maradha ya WIZI wa muda yamekuwa ni makubwa kwani juzi ahuyu bwana alichelewa kupeleka faili la kuombea hela za matibabu ya mfanyakazi mwenzio, hospitali ilikataa kumpa huduma bila pesa. Bahati mbaya sana yule mgojwa katutoka. Madhara ya WIZI wake yamekuwa makubwa kwani mwaka juzi alitakiwa apeleke nyaraka muhimu kwaajili ya nyongeza za mishahara ya wafanyakazi kwa bosi hakuwepo pfisini kwake. Tulishindwa kupata mshahara mpya. Madhara ya WIZI wake yamekuwa makubwa kwani mwaka jana wakati wa bajeti ilibidi barabara ya kuelekea kwetu ipewe hela za kuikarabati kwa kiwango cha changarawe lakini huyu bwana hakuwepo ofisini kuleta lile faili. Mwaka huu hali ni mbaya sana, barabara haipitiki, nakwambia ile ya kwa Babu Loliondo ni nzuri mbona!


  Siku moja huyu bwana aliugua, alituma taarifa haraka ofisini. Alitaka apewe msaada na ofisi. Alilazimika aandike barua akamtuma mwanae ailete ofisini. Barua yake ilipokelewa na ikaingizwa masijala. Ikwawekwa kwenye "outgoing correspondences". Kwa kuwa pale masijala wote walishazoea tabia ya nitafanya kesho nayo ikawekwa kwenye kundi la "to be sent tomorrow". Walisahau kuwa kesho yake ni Jumamosi na Jumatatu ni "public holiday". Uzembe wa kutofanya mambo kwa wakati ulishakuwa tabia ya idara ile, hawakuangalia nini madhara ya uzembe kazini. Kwao wao SERIKALI waliona ndio MBAYA. Inashidwa kulipa mishahara mipya kwa wakati; inatoa mishahara midigo; imeshindwa kuzuia mfumuko wa bei n.k. Walisahau kuwa kuwa mfanyakazi wa serikali unakuwa kwa namna yoyote unachangia utendaji wa serikali iliyopo madarakani.


  Huyo bwana MWIZI wa MUDA akazidiwa sana na ugojwa wake. Familia na majirani wakajitafuta tafuta wakapeta pesa kiasi fulani wakampeleka hospitali. Alichelewa sana kufikishwa hospitali, alifariki dunia.


  Ilinisikitisha sana kwani nilimfahamu sana yule bwana. Nilikuwa naabudu nae kanisa moja. Ibada ya mazishi ilifanyika mchungaji akahubiri atatoa ushuhuda wa alichooteshwa usiku. Kwa kweli wote tuliishiwa nguvu.


  NDOTO YA MCHUNGAJI


  "Nilipata ufunuo nikiwa nimelala, nikaona mambo nisiyoyategemea. Mzee wetu huyu ametenda mambo yaliyomchukiza Muumba wake. Nimeamriwa niyatoe leo hadharani ili wafanyakazi wa serikali hapa kwetu wabadilike. Huyu mzee wetu tulimheshimu, tulimpenda na kumjali sana lakini alikuwa MWIZI".


  Wote tukastuka na kupiga kelele "hehehehe......, hapana baba mchungaji, siyo kweli". Mchungaji aliendelea " alizoea kuiba MUDA, wizi ambao umesababisha misiba katika familia nyingi za nchi yetu. Ameleta HASARA kubwa SANA kwa taifa hili na kuchangia madhara mengi kitu ambacho kimesababisha vifo kwa watanzania wasio na hatia. Amesababisha watu wema kulaumiwa na kulazimisha baadhi ya maamuzi kufanyika bila nyaraka rejea hivyo kuingiza wafanyakazi wenzie na nchi kwa ujumla matatani. Hivi ni vitu vilivyomuudhi sana Muumba. Huyu bwana alipenda sifa na kuonekana katika makanisa na jamii; akapenda heshima; lakini amekuwa analipwa msharaha mkubwa miaka mingi pasipo kufanya kazi. Ni MWIZI wa MUDA; ni MWIZI anaelipwa PESA nyingi toka kwa walalahoi wa nchi yetu bila kufanya KAZI. Leo amepata thawabu yake ni JEHANAMU ya MOTO."


  Alikuwa MZEE wa kanisa "SAWA"; alikuwa kada mzuri "SAWA"; alikuwa mpatanishi mtaani kwetu "SAWA". Lakini alikuwa MWIZI ni MWIZI wa muda. Leo Muumba katupa angalisho kwa hii hukumu, tuache kuiba MUDA. Tutimize wajubu wetu kuiepa huku ya "JEHANAMU ya MOTO".
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  :juggle::juggle::juggle:
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  :focus:
   
 4. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  .....msg inanihukumu mimi civil servant so 'sijaipenda'!!! if that is the case nearly all civil servant tutaenda motoni. muda huu nimeacha AC na computer ON nipo kwenye biashara zangu na secretary nimemwambia 'natoka kidogo'!!. Bila hivyo nitakufa njaa. Nina Masters na miaka 8 kazini lakini mshahara wangu kituko..."THEY PRETEND TO PAY ME, I PRETEND TO WOK"-ngoma droo!!
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ...They Pretend to Pay Me, I pretend to Work..... What comes first? is it work or payment?
   
 6. m

  matunge JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Tutazame pande zote! Employer na Employee! Tunatimiza wajibu wetu?
   
 7. J

  Juma. W Senior Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii kali kwelikweli; inafanana na moja kumwaga ugali na mwingine kumwaga mboga. Mwisho wote wawili mnalala njaa
   
 8. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 875
  Trophy Points: 280
  Aisee Huyo jamaa sio ana pacha wake hapa kwetu kweli... Mbona kama anafanana na kila character!!
   
 9. P

  Pumba Mwiko Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sure mkubwa hapo ngoma droo!Wamemwaga ugali umemalizia kula mbogo.Inatakiwa mtu alipwe kutokana na elimu+Ufanyaji kazi mzuri.Hapa ninapofanya kazi kuna watu hawana shule kwa vichwa na niwavivu bt wanalipwa vzr,wkt najituma mbaya na mshahara kiduchu kulingana na kazi+elimu.inaniuma sana
   
 10. J

  Juma. W Senior Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  :juggle:
   
 11. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hili Kweli ni somo, ila mbona ipo serikalini tu! na mashirika ya umma, mbona kwenye makampuni ya watu binafsi wanaojua kufuatilia mambo sio hivyo!?, watu wanachapa kazi na wanalipwa mshahara stahili, Serikali ibadilike sana, wakubwa sio kukaa tu na kipiga simu, angalia Tanesco! mameneja wengi wao, wamekaa tu sio wabunifu, wateja wengi sana wanasubiri kuunganishiwa umeme tena maeneo amabyo yamepimwa na serikali kwa nini msiende huko na mipango ya kusambaza umeme kwa hawa watu?, na kwa nini msije na mawazo mbadala wa kuzalisha umemem wa kutosha? na je huo unaozalishwa ni asilimia ngapi unapotea njiani kwa miundo mbinu mibovu?.

  TANESCO BADILIKENI, na SIO TANESCO TU, AFYA NK.
   
 12. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  :A S-fire1::A S 109::flame::target::mad2:
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,850
  Likes Received: 2,776
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu hii Serikalini haiwezi kuisha! Mshahara gani huo wanaotulipa? Tukijidai eti sisi wachapakazi tutakufa njaa wapendwa tunaomba mtusamehe!! Wewe fikiria mtu ni mtaalam halafu analipwa 210,000/= kwa mwezi ulishaona wapi hii? Halafu umwambie akae saa zote kazini huo mshahara utamtoa kweli? Hapa ndo maana serikali inachochea ufisadi. Mfanyakazi wa hivyo akipata nafasi ya kuhamisha mzigo hawezi kuzubaa!
   
Loading...